Pole ndugu,
Bleeding kwa mimba iliyo chini ya miezi saba mara nyingi husababishwa na abortion ingawa tatizo lolote la kwenye njia ya uzazi laweza kusababisha bleeding. abotion ziko za aina nyingi kutegemeana na status ya shingo au njia ya kizazi (cervix) na kuwepo au kutokuwepo na uterine contractions (ikiambatana na maumivu ya tumbo).
Kuna threatened abortion, hii ni ile ambayo mimba haijatoka lakini inatishia kutoka, ambapo cervix inakuwa imefunga, lakini damu zinatoka huwa si nyingi sana, tumbo linaweza likawa linauma au lisiume.
Pia kuna incomplete abortion, hii ni kwamba abortion imetokea lakini kuna sehemu fulani ya kiumbe au kondo la nyuma imebaki ndani kwenye tumbo la kizazi. hapa bleeding huwa inakuwa nyingi, cervix huwa imefunguka na unaweza kushika sehemu ya kiumbe au kondo unapompima mama na tumbo linauma.
Kuna complete abortion ambapo mimba imetoka yote, damu haitoki tena, njia imefunga na tumbo limeacha kuuma.
Kuna aina nyingine kama missed abortion ambapo kiumbe kimefia tumboni lakini hakuna kitu kilichotoka, njia imefunga na damu mara nyingi huwa haitoki au ikitoka ni kidogo sana, na tumbo haliumi. Pia kuna septic abortion nk.
Matibabu inategemea na aina ya abortion.
Mkeo nadhani anaweza kuwa na threatened abortion (mimba inatishia kutoka), anaweza pia kuwa na aina nyingine za abortion kutegemeana na status ya cervix au tatizo lingine.
Kitu cha Muhimu sana kwa sasa ni kufanya mpango wa haraka aende hospitali kwa njia ambayo haitamtikisa sana ili akachunguzwe ijulikane ni aina gani ya tatizo linalomsumbua ili apate matibabu sahihi, sisi hapa tunakupa ushauri kwa hisia lakini akionwa hospitali tena haraka itasaidia kusaidiwa kwa uhakika. Bleeding sio jambo dogo, tafadhali usimtibu nyumbani hizi measures tunazokushauri ni za kufanya wakati haraka una-arrange kumpeleka hospitali.
Kitu cha kumsaidia kwa sasa kama ni threatened abortion ni kama alivyoshauri King'asti kwamba apate complete bed rest, wakati mnapanga mipango ya kumpeleka hospitali, umuangalie sana kiasi cha damu kinachotoka (uendelee kumonitor bleeding), mpatie dawa za maumivu, ningeshauri paracetamol, wengine huwa wanatoa dawa za kufanya kizazi kisi-contract kwa ajili ya kuzuia mimba isitoke, kama salbutamol ingawa kwa mimba ndogo uwezo wake wa kufanya kazi bado ni debetable. Hospitali watakupa pia dawa kama duphaston ambazo hufanya kazi ya kuzuia mimba isitoke kwa wale akina mama ambao corpus luteum yao imeshindwa kufanya kazi mapema kabla placenta haijaanza kutengeza hormone ya progesterone ambayo ndiyo hu-maintain pregnancy. Duphaston hufanya kazi ya progesterone. Na matibabu mengine utayapata kutegemeana na tatizo.
Pole na kila la kheri.