Tafadhali nisaidieni kujua huu ugonjwa unaonisumbua mkononi mwangu

Ngalikivembu

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2010
Posts
1,959
Reaction score
876
Habarini ndugu zangu,

Jukwaa hili ni mara yangu ya kwanza kuposti uzi huu. Sijawahi kuandika zaidi ya kusoma tu yanayoandikwa. Leo nimeona nije hapa niweke wazi huu ugonjwa unaonisumbua kwa mwezi mmoja sasa.

Napata maumivu makali sana kwenye mkono wangu wa kushoto kuanzia kifundo cha katikati ya mkono hadi begani na sehemu kidogo ya bega langu.

Maumivu haya yanaleta mchanganyiko huu, mara nasikia baridi sana sehemu hiyo yote. Mara wakati mwingine nasikia ubaridi kiasi kwamba napata maumivu makali mno yakushindwa kulala na wakati mwingine kukaa.

Sijajua ni ugonjwa gani huu. Sijawahi kujigonga wala kuanguka. Wala siendeshi pikipiki. Awali nilifikiri huenda nimelala vibaya na hivyo kuulalia mkono wangu.Lakini kumbe hata mchana tu utakuta maumivu yanaanza.

Nimejaribu kuchua ua kupaka dawa aina ya diclofenac fluid lakini hakuna unafuu. Sasa naomba kama kuna mtu mwingine pia amewahi kukutana na maumivu kama haya anisaidie.Lakini pia madaktari mliopo hapa nisaidieni.

Kama nimeeleweka kwenye maelezo yangu nashukuru sana ndugu zanguni.
 
Pole sana ndugu hujasema una miaka mingapi? Kwa utaalamu wangu ninahisi hizo ni dalili ya ugonjwa wa Stroke Kiharusi jaribu uende hospitali haraka unakaa mwezi mmoja pasipo kwenda Hospitali? upo mji gani wewe?

Ngoja madocta wakuje MziziMkavu come this way
Bibie huajmbo ram?

Mama mkwe wangu hujambo lakini farkhina?
 
Last edited by a moderator:
Au gesi?

Nenda hosp za wachina, wazuri kwa masuala ya viungo
 
Unatumia muda gani kwenye laptop au simu kwa kuscroll?
 
Nipo tu MziziMkavu, naendelea kujitahidi kufanyia kazi ushauri mbalimbali unaotupa hapa though nimeshindwa kabisa kupunguza tumbo, mazoezi nafanya lkn uzito nao unazidi kuongezeka tu


 
Last edited by a moderator:

Hiyo ni Rheumatoid Arthritis au baridi yabisi. Kwa upande mwingine una kama dalili za gout
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…