Tafadhali tukumbushane Makamu wa Rais wa Tanzania tangu 1962

Tafadhali tukumbushane Makamu wa Rais wa Tanzania tangu 1962

Frank Higno Fuime

Senior Member
Joined
Dec 20, 2020
Posts
104
Reaction score
153
Habarii wandugu,

Poleni na majukumu ya mwanzoo wa wiki nimeonelea leo tuwakumbuke watu waliowahi kuwa makamu wa raisi wa Tanganyika 1962-1964 na baadae Tanzania 1964 mpaka sasaa.

Wajuvii wa siasa na historia ya nchi watuambiee upi ulikua msingii wao hasa au Ni vivuli tu watu wasiopaswa kusema lolote.

Karibuu
 
1. Karume
2. Aboud Jumbe
3. Ali Hassan Mwinyi
4. Dr Omar
5. Dr Shein
6. Dr Gharib Bilal
6. Bi Samia Suluhu
 
Mawaziri wakuu wote toka Muungano mwaka 1964 hadi 1994 walifahamika pia kama Makamu wa Kwanza wa Rais. Kwa upande wa Rais wa Zanzibar akawa ni Makamu wa Pili wa Rais wa JMT

Mawaziri wakuu hao

1.Rashid Mfaume Kawawa
2.Moringe Sokione
3.Dr.Salim Ahmed Salim
4.Jaji Joseph Warioba
5.John Samuel Malecela
6.Cleopa David Msuya.

Cleopa David Msuya na Dr Salmini Amuor Juma Ndio Makamu wa Kwanza na wa Pili wa mwisho kwa nafasi zao.

Katiba ilikuja kubadilishwa mwaka 1994 baada ya ujio wa Vyama vingi hoja na hofu ya CCM ni kuwa je Zanzibar ikitawaliwa na Rais toka upinzani itakuwaje kwa kuwa ndiye atakaye kuwa Rais wa Zanzibar na Makamu wa Rais wa pili wa Muungano.

Nafasi ya Umakamu wa Rais ikatengenezwa na Rais wa Zanzibar akaondolewa kwenye Nafasi ya kuwa Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Muungano badala yake atakuwa Mjumbe tu wa Baraza la Mawaziri la Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwa kama Waziri asiye na Wizara Maalumu.

Dr. Omar Ally Juma ndiye aliyekuwa Makamu wa Rais katika utaratibu mpya ambao tupo nao hadi leo na
Fredrick Sumaye ndiye aliyekuwa Waziri mkuu wa kwanza kwenye utaratibu mpya ambaye sio Makamu wa Kwanza tena wa Tanzania.
 
wakati wa utawala wa Ali Hassan Mwinyi kulikuwa na Mawaziri Wakuu na Makamu wa Raisi watatu. Katiba yetu kabla ya mfumo wa vyama vingi ilikuwa inaelekeza kwamba, ikiwa Raisi wa Muungano atatokea Zanzibar, basi Waziri Mkuu atakuwa Makamu wa Kwanza wa Raisi, na Raisi wa Zanzibar atakuwa Makamu wa Pili wa Raisi ktk serikali ya muungano. Kwa msingi huo, Joseph Sinde Warioba, John Samuel Malecela, na Cleopa David Msuya walikuwa mawaziri wakuu na makamu wa kwanza wa raisi.
 
Back
Top Bottom