wakati wa utawala wa Ali Hassan Mwinyi kulikuwa na Mawaziri Wakuu na Makamu wa Raisi watatu. Katiba yetu kabla ya mfumo wa vyama vingi ilikuwa inaelekeza kwamba, ikiwa Raisi wa Muungano atatokea Zanzibar, basi Waziri Mkuu atakuwa Makamu wa Kwanza wa Raisi, na Raisi wa Zanzibar atakuwa Makamu wa Pili wa Raisi ktk serikali ya muungano. Kwa msingi huo, Joseph Sinde Warioba, John Samuel Malecela, na Cleopa David Msuya walikuwa mawaziri wakuu na makamu wa kwanza wa raisi.