Tafadhali Usininukuu; Kwa Kutanguliza Ubinafsi Wetu....

Tafadhali Usininukuu; Kwa Kutanguliza Ubinafsi Wetu....

maggid

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2006
Posts
1,084
Reaction score
1,246
Ndugu zangu,

"Na hakika, kwa kutanguliza ubinafsi wetu, tunawaandalia watoto na wajukuu wetu, mazingira magumu ya kuishi kwa amani katika nchi yao.

Katiba Mpya ijayo, iwe ni kwa Tanzania ya leo, kesho na keshokutwa. Ni urithi wa maana na wa kistaarabu tutakaowaachia watoto na wajukuu zetu.

Na Tume Huru ya Uchaguzi, ni DHAMANA ya kipekee ya Amani na Utulivu tutakayowaachia Watanzania wa vizazi vijavyo.

Maana, katika nchi zetu hizi, mara nyingi watu huanza kuchinjana kutokana na kukosa imani na wenye kuhesabu kura; hivyo, Tume ya Uchaguzi. " Tafadhali Usininukuu.

Maggid Mjengwa,
Iringa.
http://mjengwablog.co.tz
 
Umenena na wanasikia kwa usikivu mzuri kabisa. Issue ni kwamba, unadhani wataafiki na kutekeleza matakwa ya maono ya mbali kama uonavyo wewe?
Hasha...nina wasi nao (watendaji/watekelezaji).
 
Back
Top Bottom