Tafadhalini sana,naomba msaada

kasitile

Member
Joined
Feb 22, 2011
Posts
32
Reaction score
0
Pole na majukumu wakuu!

Naomba msaidie/kunipa ushauri kuhusu hili

Mwaka 2011 mama yangu mzazi (ana miaka 50) alipata tatizo la kutokwa na damu mfululizo kwa muda wa miezi 6.Ilikuwa hivyo kwa sababu alificha tatizo.Lakini baada ya kutambua hilo,alienda hospitali na kupatiwa dawa,ambazo zilitatua tatizo.Lakini sasa tatizo limerudi tena.

Naomba kujua tatizo hili linasababiswa na nini hasa?nini madhara yake?na tiba yake ya kudumu.Nauliza hivi kwa sababu hata mara ya kwanza hospitali hatukupata maelezo ya kutosheleza,na kwa kuwa alipatiwa dawa ambazo zilisaidia sana,kwa hilo sikufuatilia sana.Najua mwisho wa siku ni kwenda hospitali,lakini kama mnavyojua,hospitali zetu za kijijini,na huduma za afya kwa ujumla zilizvyo.Kujua tatizo ni nusu ya kutatua tatizo.

Natanguliza shukrani.
 
angeenda kucheki mambo ya uzazi.mpeleke ocean road hospitali.mambo ya kubleed bleed sio mazuri,mengine huwa mwanzo wa cancer
 
kasitile, Pole kwa tatizo la mama,

Swali kuu hasa ni kutambua kuwa je mama aliona ukomo wa siku zake("kutumikia") yaani Menopause?
 
Last edited by a moderator:
Ushauri wangu ni kuwa aende kwenye hospitali kubwa kuonana na madaktari bingwa wa matatizo ya wanawake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…