Tafakari ya Pasaka: Tunaonyeshwa kuwa Magufuli hakuyaishi maono yake na kama aliyaishi hayakuwa maono sahihi?

Mimi sijasema lazima afuate ushauri wangu.
 
Tusadie orodha ya hilo genge lilioiba na kudhulumu watu.
 
Unataka uwekeze wewe ??
Mimi ni Mwekezaji wa Siku Nyingi na ninailipa Serikali Kodi. Sipendi na ninachukia mambo ya kujichora wadhalili kwa kusema eti sisi ndio wenye shida. Ukimsikiliza kauli zake ni kama anataka kuturudisha kwenye awamu ya kwenda Nje kuombaomba. Ni dhahiri anaonyesha viatu vya marehemu vinampaya.
 
acha mama amalizie honeymoon, hawahawa watamgeuka na watammisi Magufuli.
Maono ya kujitegenea ndio maono sahihi. Eti Tembo hawali madini.Kwa hiyo, turuhusu watu tu waje wajichimbie na kusepa?
 
Wewe jamaa sijui unafirw.... Lini nchi hii imewahi kujitegemea ???

Sana sana Magu ameendesha nchi kwa kupora, kukopa kopa kama mlevi na kudhulumu watu.

Hupendi misaada wakati mlikuwa mnalilia mpaka pesa za kusomesha wajawazito wakati hataki kuwarudisha shule.

Pesa za Covid haukuwa msaada ule ?? Ziko wapi ???

Akili za kimavi yako.
 
Awamu inaenda na Rais aliepo
Ndo maana Zanzibar Wana awamu nane
Mwinyi alikaa awamu ya mwaka mmoja Tu

Hata Nyerere ni awamu ya miaka 23
 
Kuna Watanzania 8000 mkoani Morogoro ambao wao na familia zao ni waathirika wakubwa wa "mabavu" ya Hayati Magufuli kutokana na kufungwa kwa viwanda wiwili vikubwa.
Hayati inawezekana alikuwa na nia njema na Tanzania,tatizo lake ni kujiona kuwa yeye ndiye mwenye akili kuliko Watanzania milioni 60,hivyo hakutaka kupata ushauri wa msaidizi wake yoyote.
Wafuasi wa hayati inabidi tu mkubali kuwa enzi za Tanzania kuwa "hell on earth" zimepita,sasa ni wakati wa Watanzania kuufurahia Utanzania wao.
 
Utajiri wa kupora vya wengine.
 
Maono ya kujitegenea ndio maono sahihi. Eti Tembo hawali madini.Kwa hiyo, turuhusu watu tu waje wajichimbie na kusepa?
Hapa ndipo nimeona ujuha wako.
Wapi pamesemwa hivyo na nani aliyesema hivyo!!?
Kwa nini mnapenda kuwawekea watu maneno mdomoni!!?
Pole sana kwa kuteseka kwa kuwekwa wazi ukweli wa uhuni wa jamaa yenu.
 
Kuhusu awamu, nadhani issue sio uchaguzi ila ni SURA ya aliyeko Ikulu kwa wakati huo, refer to Zanzibar, uchaguzi wa Zanzibar hufanyika kipindi kimoja na huku bara, je wakati Karume anauawa kule Zanzibar si ilikua kipindi baada ya uchaguzi? Ilikuaje Aboud Jumbe awe raisi wa awamu ya pili ilihali aliingia kipindi ambacho tayari uchaguzi ulikua umeisha fanyika? Labda hilo linaweza kukuchanganya cause mwaka 1975 ulifanyika uchaguzi mwingine ambao ulimuweka mzee Jumbe tena madarakani; jumbe alitemeshwa uraisi mwaka 1984 na mzee Mwinyi akaingia madarakani, je Mwinyi alikua rais wa awamu yapili au ya tatu ya kule Zanzibar? Jibu ni awamu ya tatu, remember mzee Mwinyi hakusimama kwa uchaguzi, katiba ilifatwa na mzee Ali Hassan Mwinyi akaukwaa uraisi, halikadhalika kina Abdulwakili hadi Komando, Karume, Shein na sasa Mwinyi tena. So awamu sio uchaguzi wa tume, ni sura ya nani kakalia kiti.

Kuhusu Wawekezaji, mkuu hivi unajua hata sasa tupo nyuma ya keebord kwasababu ya uwekezaji alioufanya kaka Max Mero? Halafu JF nahisi inakwenda kurudia zile enzi zake, kipindi cha miaka 6 waandishi wa JF wamekua wanaripo vitu vidogo sana, but JF was meant for great thinkers, ulikua ukiwasoma kina mzee Mwanakijiji unapata madini ya maana sana, hivi yule jamaa aliyeripoti issue ya OILCOM na police wakaanza kumchunguza unadhani alikua anapitia kipindi gani wakati kaka Max anahojiwa na police?

Kuhusu uchaguzi wa mawaziri; nahisi hapa mama unamuonea, tuweni wakweli, Magufuli alikua anatumbua kwa kuwadhalilisha sana watu, mama anapiga na kukupa chakula, hadi sasa mawaziri wamebadirishiwa tu wizara, mfano kama Jafo yeye maeneo yake CAG kaonesha kuna upotevu wa fedha, kibaya zaidi (kwa maneno ya mama ) wizara yake Jafo ina historia hiyo hata miaka ya nyuma, hivi unadhani kama hakua mtu wa Magu huyo angefanywaje siku ile? Hakika watoto wa Jafo wangekua na wakati mgumu sana shuleni, watoto wenzao wangewaponda kweli kweli; but again, kikatiba hivi baraza la mawaziri linaundwaje? Makamo anatajwa kweli? Kasome tena, ni raisi akishauriana na Waziri mkuu. Tumuache mama afanye kazi cause hali ilivyo hata sasa tunaandika bila kuogopa ogopa kama enzi za awamu ya 5
 

Baba Padri naona umejitahidi kuonyesha mapenzi yako kwa Magufuli na sio kwa nchi kwenye uzi namba moja. Pia ninakusifu kwa uwezo wa kuandika kwa usahihi na mpangilio wa kuvutia. Lakini napenda ufahamu kuwa Magufuli hakuwa Tanzania, bali alikuwa kiongozi kwenye nchi ya Tanzania, kwa sasa bado Tanzania ipo, ila Magufuli hayupo. Hakuna lolote litasimama kwakuwa Magufuli hayupo, na hata likisimama sio kwakuwa Magufuli hayupo.

Kama kuna mazuri uliyaona kwa Magufuli, nina uhakika na mabaya yake uliyaona, labda kama umeongozwa na uRomani wako kumtetea, na kukwazika na huyu kwa uislamu wake. Hakuna viatu vyovyote ambavyo huyu mama anawajibika kuvivaa toka kwa Magufuli, kama ambavyo Magufuli hakuwajibika kuvaa vya mtangulizi wake yoyote, tena huku akiongea kwa kejeli kuwa kila zama na kitabu chake. Kwa sasa ni zama nyingine, acha mama afungue kitabu chake. Nisingependa kuongea mengi ya mapungufu ya Magufuli, lakini itoshe kusema acha tubaki na amani yetu, kwani Mungu kaamua kufanya mabadiliko bila damu kumwagika.
 
Kila zama na kitabu chake,usimwamshe aliyelala utalala wewe.Anaeweza kuyasoma mazingira yake na kuishi kulingana na mazingira anayofaida zaidi.
 
Kuna watu walitamani Watanzania tuendelee kuishi kama digidigi kwenye nchi yetu wenyewe. Huenda ni wanufaika lakini wamesahau matusi ya mwendazake kwa raia kutuita wanyonge huku wao wakila na kusaza na kujenga empire zao.
We can breath now.
 
Umenigusa sana! Kimsingi wanyonge wamepigwa tobo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…