Tafakari ya Pasaka: Tunaonyeshwa kuwa Magufuli hakuyaishi maono yake na kama aliyaishi hayakuwa maono sahihi?

Tatizo watanzania hatueleweki tunataka nini
 
Stalin baada ya kifo chake alirithiwa na Nikita Khrushchev., Siku mmoja akiwa ana hutubia Kamati Kuu huku akipinga sera nyingi ya mtangulizi wake, Mjumbe mmoja bila ya kujitambulisha alikereka na akamundikia ki note cha kumshutumu na kumlaumu, "we Nikita ulikua msaidizi wa Stalin,

"kwa nini hukusema haya kipindi hicho Stalin akiwa hai?" Khrushchev akakisoma na akaomba Mjumbe aliye andika anyooshe mkono juu amtambue ili amjibu .Hakuna mkono uliyo nyooshwa, Khrushchev akasema "kinacho kushinda wewe kunyoosha mkono leo , ndo hicho hicho kilicho nishinda mimi kusema enzi hizo"
 
Hii dunia hakuna mtu ambaye hawezi achwa kokosolewa hata afanye nini hivyo tuyachukilie mambo kama asili yetu wanadamu inavyotaka
 
Kakonko TPA
Bashite
Sabaya
Byakanwa
Wabunge wote waliopitisha bila kupingwa na wakuregenzi wake.
Walihousika na kifo cha Akwilina
Mwenyewe Alichota pesa za korosho kusini
Tusadie orodha ya hilo genge lilioiba na kudhulumu watu.
 
Hivi mnaomtetea Magufuli mnadhani utetezi wenu utasaidia kufufuka kwake? Mbona mnajitoa ufahamu utadhani mmekalia kitu hapo mlipo? Yaani mlitaka Samia afuate kila kitu cha Magufuli halafu bado aitwe Rais wa Tanzania Mh. SAMIA SULUHU HASSAN? Kwa taarifa yenu na genge lenu na hata nyie mnajua madhaifu ya Magufuli ni mengi kuliko mazuri yake.
 
Nataka kusema hivi. Nchi hii inaenda kuaribika. Sina la kusema zaidi Ila muda utaongea.
Risala ndefu lakini isiyokuwa na content.

Mleta mada haelewi hata katiba inasema nini pale inapotokea kiongozi ambaye yupo madarakani amefariki.

Rais Samia, kikatiba ni Rais kamili, na siyo Rais kwa niaba ya marehemu. Kikatiba halazimiki kubakia na mteule yeyote wa marehemu, wala halazimiki kufuata vipaumbele vya marehemu. Mh. Rais Samia, wakati wa Serikali ya hayati Magufuli alikuwa msaidizi wake, lakini kwa sasa yeye ni Rais mwenye wasaidizi wake kuanzia Mpango na wengine wengi.

Watanzania wengi wenye uelewa wanafahamu kuwa utawala wa marehemu ulikuwa na mapungufu mengi. Wakati tukiyakumbuka mazuri ya marehemu na kudhamiria kuyaenzi, tuna wajibu mkubwa na wa lazima wa kusahihisha mapungufu yake.

Uongozi wa marehemu, kwa kiasi kikubwa ulitawaliwa na propaganda nyingi zisizo halisia za mafanikio, ilihali Mh. Rais Samia anataka kuusimamia uhalisia ambao utadhihirika mbele ya sisi sote. Dhamira yake hiyo imeonekana wazi kwa hatua yake ya kwanza ya kutaka kulinda uhuru wa vyombo vya habari.

Nchi haijengwi kwa fikra za mtu mmoja tu. Hayati Mwalimu Nyerere aliwahi kusema, "awamu ya kwanza imekaa kwenye uongpzi kwa miaka mingi. Tulifanya mazuri na makosa mengi. Tusifanye makosa, sisi ni malaika? Kila awamu inayoingia madarakani inafanya mazuri na makosa. Inayofuata inayachukua mazuri ya awamu iliyotangulia na kuyaendeleza. Na yale mabaya wanayaacha"
 
Sidhani kama kuna mwenye hamu na hivyo viatu vya marehemu maana havikulisogeza Taifa mbele. Kwa kiasi kikubwa tumerudi nyuma.
 
Stori uliyosimuliwa hapo kale ilikuwa feki,unayoyaona sasa ndio uhalisia wenyewe.
Mbona bado sana. Kuna mambo mengi yatafunuliwa kwetu kuhusu janja janja katika utendaji wa Rais Magufuli. Makamu wa Rais, Dk. Mpango ameahidi kumuonesha Rais Suluhu namna wizara mbalimbali zilivokuwa zinahamisha/kuazima fedha na kutumiwa tofauti na maelekezo ya bajeti.
 
Sidhani kama kuna mwenye hamu na hivyo viatu vya marehemu maana havikulisogeza Taifa mbele. Kwa kiasi kikubwa tumerudi nyuma.
Kwa hiyo huyu ndo atalisogeza Taifa Mbele? Kwa nini hakulisogeza pamoja naye? Serikaii walikuwa wanaongoza pamoja mbona hayo maono hatukuwahi kuyasikia?
 
Hayati aliibomoa hii nchi kupita kiasi na wizi wake
Huyu "kazi iendelee" yeye alikuwa wapi wakati Nchi inabomolewa? Sio yeye huyu waliyenadi naye Ilani? Hebu tueleze ni jambo gani hasa alipata kuifnayia Nchi hii unaloweza kumkumbuka nalo na ambalo linakutia matumaini kuwa ataipeleka Nchi kunakotakiwa?
 
Kama Nchi haijengwi kwa maono ya mtu mmoja huyu yeye ana maono kutoka kwa watu wangapi? Hayo maono ya kukusanya kodi kwa kubembeleza umemshirikisha wewe? Ikiwa hayo maono sio yake ni lini kumeitishwa Kura ya maoni na Watanzania tukaazimia kuwa sasa tukusanye kodi kwa kubembeleza au kuwa wawekezaji waje na marafiki zao kadri wanavyoweza ili wawe na imani na biashara wanazofanya?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…