Elections 2010 Tafakari !!!!!!!!!!!!!!!!!!

mayenga

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2009
Posts
4,118
Reaction score
1,970
Nikiwa kati ya WATU waliohudhuria mikutano ya kampeni hasa ya urais,nimeona
mengi,nimesikia mengi,ahadi kemkem,tamu,nzuri na zenye kuvutia na kama
JK,SLAA au LIPUMBA mmoja wo akishinda na kutekeleza ahadi zake basi TANZANIA
itakuwa kama Boswana au kama sio kuifikia Afica kusini. Sina sababu ya
kuzitaja ahadi kwani wengi wenu mwazijua.

Ni saa 12:30 za jioni siku ya ijumaa,natoka ofisini kwangu JMOO nakwenda
posta ili kupanda gari la kuelekea mbezi nyumbani kwangu(mbezi ya
kimara).Abiria ni wengi kama kawaida,wezi wamo,ila kuna magari ya kwenda
mbezi ya buku(elfu moja) naingia na muda si mrefu gari inajaa na
kuondoka,wote tumekaa,foleni ni kama kawaida kwani inaanzia faya na uku gari
ikiwa imewekwa radio moja ya chama tawala.Watu tupo kimya na aliyesimama ni
konda tu.

Mara hiyo radio ikaanza kutangaza sera za mgombea uras wa chama
tawala,ahadi nyingi,kile mara iki najua mwazijua sina shida ya kuzitaja ila
ni moja tu ambayo nitaitaja ambayo imenipelekea kuandika UJUMBE huu kwenu,ni
ile ya KUNUNUA BAJAJI 40 KWA WAMAMA WAJAWAZITO,hapo ni saa 1:30 za jioni na
hatujavuka magomeni.

Mara baada ya huyo mgombea kutaja iyo ahadi,nikasikia sauti kuoka nyuma
ya gari ikisema "ZIMA RADIO YAKO AU BADILISHA STESHENI"ni sauti ya kike tena
mwanamama mjamzito.Dereva alizima radio,tukawa kimya kila mtu nahisi alikuwa
anajiuliza kwanini huyu mama kasema radio izimwe au ibadilishe
stesheni,ukimya ulitawala kama dk 15.Tukiwa tunaanza foleni ya ubungo pale
mahakama ya ndizi au bigbrother, na ikiwa ni saa 2:07 za usiku,nikasikia
sauti ya mwanamama mwingine(sio mjamzito) ikisema "KAMA MIMBA ZINGEKUWA
ZINABEBWA KWA ZAM HUYU KIKWETE ASINGETAMKA MANENO HAYO"nikashtuka nikageuka
nyuma nikakutana uso kwa uso na yule mama mwenye mimba,mimba yake ilikuwa ni
kama ya miezi nane tena ilikuwa kubwa(namaanisha tumbo ni kubwa sana).

Tukiwa tupo stand ya mkoa na gari likiwa limesimama na ni saa 2:45 usiku
kumbuka nimetoka posta saa 12:30 za jioni.Yule mama mjamzito akasimama
akaanza kusema "MIMI SITOMPA KURA KIKWETE KWA JAMBO ILI,NILIKUWA NIMPE ILA
KWA JAMBO KAMA HILI SIWEZI KUMPA"huku akilia na kutokwa na machozi,yule mama
mwingine aliyesema "kama mimba zingekuwa zinabebwa kwa zam huyu kikwete
asingetamka maneno hayo" akaanza kumbembeleza yule mama mjamzito akimsii
akae.Nilimtazama kila mtu ndani ya gari sura zilibadilika zikawa sura za
majonzi.

Nikatoka kwenye daladala(kimawazo) nikaleta taswila ya BAJAJI nikamuweka
yule mama nyuma na mimi nikawa dereva,nikafikiria umbali wa kilometa 50 toka
kijijini kwetu kule kanyigo kuja hospital,barabara imejaa mashimo,nikawaza
tumbo la yule mama akiwa yuma na uchungu na babaji ikiwa inayumba kwenye
mabonde ya barabara,"NILILIA" nilishutushwa na honi nyingi za magari ambazo
zilikuwa zikilipigia daladal letu kwa kutotembea, kwani kila mtu alikuwa
kwenye mawazo ya yule mama(naisi) na dereva alijisahau kwa kumuonea huruma
yule mama.Nilikuwa karibu na dereva nikamuuliza vp?,akajibu "WE ACHA TU"uku
akitoa leso na kufuta machozi na kuanza kuendesha gari.

Ni saa 3:07 usiku tupo kimara tunaanza foleni ya kimara stopover,watu
wote wapo kimya akuna aliyeshuka mpaka sasa na konda kaka kwenye mlango
ameinama,kila mtu kainama,uku wengine wakivuta mafua,na yule mama mjamzito
akionekana ana asira na uku machozi yakimtoka yenyewe.Nikajiuliza ina maana
watu wote tunakwenda mbezi?,pia huyu mama vp mbona kabadilisha kila mtu
ndani ya daladala? Katumwa nini?.Nikasikia sauti ya baba mmoja kutoka
katikakti ya gari akisema shusha konda hapo,konda akasema wapi?,baba akajibu
hapo hapo,Mmmmmmmmm?,"Samahani konda nilikuwa nashuka bucha nimejisahau"
alisikika yule baba akisema,Mmmmmmmmm?.Ndipo nilipoona kila mtu karudi
katika hari yake ya kawaida na wengine wakashuka hapo kama watu sita
hivi.Nikajiuliza je walikuwa wanawaza nini? Mpaka wapitishwe kituoni?.Je
walikuwa katika taswila kama yangu?,au uchovu wa kazi?

Kati ya wale walioshuka pale njiani(sio kituoni) baba mmoja akasema
akimwambia yule mama mjamzito "POLE SANA MAMA NA MIMI NAKUHAIDI SITOMPA KURA
KIKWETE"akatelemaka.Tunavuka stopover na ni saa 3:30 usiku,kila mtu kaanza
kusema lake"KIKWETE HANA AKILI"alisikika baba mmoja,"KIKWETE NI MGONJWA"
alisikika dada mmoja,"WANAIGEUZA NCHI YA FAMILIA KWANI HAPA TUNATAWALIWA
KIFALME" alisikika kaka mmoja.Ni saa 3:45 nashuka kibanda cha mkaa na
niliposimama nikwaambia abilia "HUYO NDIO RAIS WENU HATA AKIWA CHIZI SI
MLIMCHAGUA WENYEWE" nikajibiwa na konda "SHUKA UKO NA NENDA ZAKO",Mmmmmmmm
hata konda?

Nikiwa njiani nakwenda kwangu nikawa natafakari "JE YALE MACHOZI YA MAJI
YALIYONDONDOKA NDANI YA DALADALA LEO"je ni ya bure tu?,na je "IPO SIKU
YATALIPWA"?,na je "IPO SIKU YATAGEUKA KUWA NI MACHOZI YA DAMU"? nisingependa
ilo tafakari langu la mwisho litokee.

Je wewe unatoa machozi gani au maneno gani?,je machozi ya furaha? Au ya
uzuni kama yule mama mjamzito?au maneno ya kumtukana rais wako kama wale
watu kwenye daladala.Kazi kwako. Nikipata nauli kabla ya UCHAGUZI nitakwenda
kanyigo nimuulize babu "JE BABU UMESHAWAHI KUONA KICHUGUU CHA SENENE"?.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…