Pre GE2025 Tafakuri: Haya Majiko ya Gesi wanayogawa Wabunge kila kona yanatoka wapi?

Pre GE2025 Tafakuri: Haya Majiko ya Gesi wanayogawa Wabunge kila kona yanatoka wapi?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Master Legendary

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2013
Posts
576
Reaction score
876
Wanajamvi sijui kama na nyie mnaona au ni mimi tu,nimekuwa nikifuatilia kwa muda sasa naona Wabunge wanagawa sana Majiko ya Gesi majimboni mwao.

Ninachojiuliza ni kwamba wanaigana au wanakubaliana kuwa ndiyo zawadi nzuri au kuna maelekezo au kuna sehemu wamepata majiko hayo kwa fadhila au ni nini kinaendelea.

Kuna mmoja nimesikia amegawa majiko hayo na vitu vingine vyenye thamani ya Milioni 230, najiuliza Wabunge wanalalamika mishahara na posho ndogo haya mapato yanatoka wapi?

Tujenge utamaduni wa kujiulizauliza jamani siyo vibaya tunaweza kuona kitu,tahadhari na uoga ni vitu viwili tofauti kwenye kichaka chenye nyoka.
 
Mbona walipewa wazi mwaka jana wakati wa budget ya nishati wakagawe huko majimboni.
 
Tanzania ndio nchi pekee pesa za kampeni na uchaguzi zinatolewa mapema ,tena bila ya ukakasi ila mtumishi anadai stahiki zake anapigwa kalenda .
 
Makamba akiwa wizara ya Nishati aligawa mitungi 100 ya gas kwa kila mbunge ili tu bajeti ya wizara yake ipitishwe.

Rushwa ni jambo la kawaida maana hata vyombo vya kupambana na rushwa ndio vinaongoza kwa kupambania kula rushwa.
😂
 
Wanajamvi sijui kama na nyie mnaona au ni mimi tu,nimekuwa nikifuatilia kwa muda sasa naona Wabunge wanagawa sana Majiko ya Gesi majimboni mwao...
Mambo madogo mkuu, kuna watu wameiba mabilion wanatafuta pa kuziweka na sisi wa tz tulivyo wajinga tunashangilia pewa majiko , we are stupid as Tanzanian, remember 24
 
Back
Top Bottom