Tafakuri, hivi vitu vinavyoweza kukuonesha wewe ni mtu wa aina gani

Tafakuri, hivi vitu vinavyoweza kukuonesha wewe ni mtu wa aina gani

Manyanza

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2010
Posts
16,464
Reaction score
35,629
1. Vitu unavyopost vinaonesha wewe ni mtu wa aina gani, kumbuka kuweka safi ukurasa wako kila wakati

2. Page na magroup unayo follow yanaonesha wewe ni mtu wa aina gani, rafiki zako wanaona vitu unavyo like. Jitahidi kutunza heshima yako kwa ku like na ku follow vitu vyenye staha.

3. Kabla huja accept friend request, jitahidi kuwa una view kwanza status ya mtu anayekuomba urafiki na angalia vitu anavyopost, itakusaidia kujua mtu huyu anaweza kukusaidia mambo gani.

4.Umepost jambo, marafiki zako wana comment, ukiamua ku reply usiruke wengine. Mtu anapoona umeruka comment yake na umeenda kujibu ya mwingine anajisikia dhaifu moyoni mwako. Kama comment ni nyingi na zile za awali ulishaanza ku reply, basi weka general comment ukisema asanteni nyote.

5. Usizoee kupost mambo serious ya maisha kama vile mahusiano ya kimapenzi kabla hujajua kama yanamaanisha. Watu wanafuatilia na wanajua umeshapost watu wangapi ukisema ni wapenzi wako, hii inaweza kukuathiri baadae unapokuja kuwa serious katika mahusiano au kufanya uliyenaye kuwa anakosa furaha au kuwa na wasiwasi baadaye.

6. Kama unaona mtu amepost au amecomment kitu ambacho unadhani kinaathiri maisha yake, mfano anasema flani amefariki au kuna mtu kafumaniwa na unajua sio kweli, sio lazima umtukane kwenye comment, mfuate inbox umweleze kwa heshima.

7. Ku tag mtu kwenye post yako inamaana kuwa jambo hilo au alihusika kulifanya au linaweza kumsaidia maishani mwake. Kwa nini unamtag mtu wakati umepost nyumba yako imefika kwenye lenta?

8. Mtu hujawahi kuonana naye, anakuomba umtumia picha zako za aibu, unamtumia za nini?

9. Sio kila aliyeweka picha ni ya kwake kweli, wengine wanatumia fake pictures kufanya uhalifu, fanya tathmini kabla hujazama na kuanza kutoa taarifa zako kwa mtu usiyemfahamu.

10. Ukiona mtu kapost jambo likakupa hasira, mfano mambo ya kisiasa au mahusiano, usijibu ukiwa na hasira, jipe muda na umjibu baadaye ukiwa umetulia, hii itakusaidia kutoandika jambo ambalo utajuta baadaye.
 
Back
Top Bottom