Tafakuri juu ya shirikisho la serikali tatu.

Tafakuri juu ya shirikisho la serikali tatu.

Shayu

Platinum Member
Joined
May 24, 2011
Posts
608
Reaction score
1,655
Hoja yangu ni kwamba sikatai mfumo wa serikali tatu ikiwa mazingira yanaruhusu. Tatizo ambalo tunalokabiliana nalo ambalo litafanya mfumo wa serikali tatu au shirikisho kuwa mgumu kufanyika ni udogo wa zanzibar.

Ili kufanya mfumo wa serikali tatu ufanye kazi ni lazima tutafute equilibrium. Balance ya hizo serikali tatu.

Kwasababu bila kupata equilibrium hii, Serikali hizi tatu hazitofanya kazi. Ni muhimu uwepo wa order na harmony Katika mfumo.

Tunataka kuanzisha mamlaka tatu hapa. Mamlaka ya Tanganyika. Mamlaka ya zanzibar na Mamlaka ya shirikisho. Hii ina maana tunataka Kumuibua Tanganyika awe kama seperate entity na mamlaka ya shirikisho iwe mamlaka ya kati ambayo inapata mamlaka yake kutoka pande mbili za muungano.

kwa udogo wa zanzibar mamlaka ya shirikisho haitapata equal power kutoka Both part za muungano. Influence ya Tanganyika ni kubwa kuliko ile ya zanzibar na ni lazima ita Collide tu na ile ya serikali ya shirikisho.

Matokeo ya hii kitu ni muungano kuvunjika na strifes na disorder kuingia katika nchi. - Ili serikali ya shirikisho ifanye kazi na kuwe na balance ni lazima ipate nguvu sawa Kutoka katika kila upande.

Jambo hili haliwezekani kutokana na udogo wa zanzibar. Serikali ya shirikisho haitaweza kufanya kazi tukiiibua tanganyika. Jambo litakalo tokea ni ku colapse kwa muungano.

Huwezi kuwa na maraisi wawili wanaochaguliwa wa Tanganyika na wa shrikisho muungano ukabaki kutakuwa na collision of the power. Ni muhimu kuzingatia hili.

Upande mmoja wenye mamlaka na influence kubwa ni busara kuuacha bila serikali yake. Nawaombeni muungano huu uliopo ubaki hivyo hivyo.

Matatizo ya muungano uliopo tunaweza kuyatatua ndani ya muungano huu huu.

Lakini pili tuna matatizo ya uongozi katika taifa letu ambayo ndio chanzo kikubwa cha haya tunayoyaona sasa hivi. Matatizo ya mfumo sio makubwa kama matatizo ya ubovu wa viongozi.
 
We can customize hizo federations nyingine na kuja na yetu nzuri tuitakayo na sio lazima kufuata kila kitu ktk hizo federations zilizopo AMA zilizowahi kutokea,

Ikiwa hizo zilibuniwa na binadam , walio na fikra Kama watanzania wengine nadhani hata sisi we can have own mode na Kama itaonekana kuwa na ufanisi then inakuwa mfano wa kuigwa.
 
Andrew Nkumbi

Kwanza nikuulize, je kwa sasa una amini kuna muungano?

Pili, kwasasa inawezekanaje ku strike balance, ni kwa gharama za nani na kwanini.

Tatu, kama znz walipewa wajumbe 15 wa tume, kwanini hatukufikiri ku balance strike

Nne, kama znz wanaweza kuwa na 2/3 ya kuzuia jambo kwanini tudhani ni wadogo

Tano, tutaweza vipi ku contain znz na udogo wake bila kuathiri mambo yetu. Ni kwanini haikuwezekana kuwazuia kwa katiba ya 2010 na kwanini tuone udogo eneo jingine, tusione ukubwa wake eneo la pili.

Sita, mfumo wa sasa ambao ni mzuri kwa mujibu wako kwanini una matatizo na unadhani njia gani za kumaliza matatizo hayo ukitueleza moja baada ya jingine

Saba, tunawezaje kukabaliana na chuki za wznz ambazo zinatokana na kukosekana Tanganyika

Nane, tunawezaje kuwa muungano ambao upande mmoja wa viongozi hautambuliki na upande mwingine

Halfu tutajadiliana kuanzia hapo
 
Last edited by a moderator:

Kiongozi, Nguruvi3,

Katika comment yangu hapo juu, nimejaribu ku comment kwa ujumla( maana mzima ya muungano) juu ya Mada nzima ya Mtoa mada. Ingawa yeye amejaribu kuwa specific ktk hii ya kwetu ya Tanganyika na Zanzbar, Mimi nilitoka nje kabisa na kutaka kuleta View Nyingine kabisa ambayo niliamini inaweza kusaidia hapo mbele ktk mjadala huu Kama utaendelea kwa maana ya kwamba mwisho wa siku tutaangukia ktk hii tuitakayo ya 3,

Binafsi na kili kuwa Muungano wa sasa ( uliopo) huenda sijauelewa vyema sura Yake ama inaniwia vigumu kukubali kama ninavyoisikia ukielezewa, huenda Mimi ndio nimeamua hivyo( kuamini) kuwa hata huu uliopo kwetu haujawahi kuwepo kwingine popote duniani ( nahisi tu sina hakika) na ninaamini kabisa kuwa Ni jina tu Muungano ila ni kitu tofauti kabisa na Miungano iliyozoeleka duniani.

Hivyo kwa lugha Nyingine Rahisi nasema Hakuna muungano , kwa maana iliyozoeleka ya Miungano duniani, ila Kama sote tukiuita Ni muungano ( Kama ilivyozoeleka) basi ndio moja Kati ya customized version( kwangu Mimi) ambayo sio nzuri na yenye ufanisi kiufupi ' sikubaliani na uwepo wake kwa asilimia kubwa sana'

Hata huu wa sasa Mpya Tunaoutaka, kwangu Mimi naona ni Kama customized version pia maana sina hakika Kama upo ktk dunia ya Leo muungano Kama huu Tunaoutaka ( mpya). Sijui Kama nauelewa vibaya pia ila ndio version nzuri ninayoikubali kwa asilimia kubwa sana.
Sasa ktk general comment yangu, nilikuwa na favor hii version mpya kwa kuamini kabisa kuwa ni customized version ya aina Nyingine za Miungano iliyopo, Kama nilimwelewa vibaya Mtoa mada( samahani Kama ni hivyo) niliona Kana kwamba mada Yake inataka tusiwe na muungano huu mpya Tunaoutaka wa nchi 3 ( hivi ndivyo nilimuelewa) na ni kasisitizia customized version ( niliamini hii ya sasa) kuwa ni nzuri kwaajili yetu maana tumejiamulia na hatuna haja ya kuiga hizo zilizopo. Huku ndipo nilitaka hasa kuelekeza comment yangu.

I am the defender of 3,

NB: Samahani kiongozi maswali huenda sijayajibu AMA nimeyajibu ndani, ila nilitaka kuweka picha vizuri juu ya comment yangu na msimamo wangu kwa kuamini kuwa hata huu Tunaoutaka ni Customized version
 
Last edited by a moderator:
Hivi tatizo ni Muungano au muundo wa Serikali? na utata wake uko wapi?
 
Andrew muungano wa ufalme wa uingereza unafanana na wetu usiseme hakuna muungano kama huu. Ni muundo unaofaa kwa aina za nchi zetu.
 
Hivi tatizo ni Muungano au muundo wa Serikali? na utata wake uko wapi?

Inavyoonesha tatizo ni Muungano. Na kwa kupuuza hilo ndio maana mkanganyiko wa muundo unasumbua! Hakuna pande inayotazama Muungano kwa Sura ya Umoja, Udugu na Ushirikiano katika kujenga nguvu-uimara katika Kujitegemea! Pande zote mbili zinafikiria nitapata nini kwanza kumzidi kete mwenzangu!

Naweza sema kuwa Hakuna nia ya Muungano ila tu Unafiki wa kutumia Muungano kulinda hila za pande hizi mbili! Kama haja ya Muungano ingetoka ndani ya fikra na mioyo yetu, kusingekuwa na wa kusema mimi nataka uzanzibari wangu utukuzwe naye huyu utanganyika wangu uhimidiwe, hali kuwa kuna Utanzania.
Anaita sasa!
 
Andrew muungano wa ufalme wa uingereza unafanana na wetu usiseme hakuna muungano kama huu. Ni muundo unaofaa kwa aina za nchi zetu.

Nadhani utakuwa umenielewa vibaya, Binafsi sijakataa kuwa hakuna muungano Kama huu Bali nimetumia kauri ya KUHISI ( Bila kuwa na uhakika).

Scotland na England Kabla havijaungana na kuwa United Kingdom mwaka 1707, nchi hizo mbili zilikuwa na Mfalme mmoja toka mwaka 1603, ila kila moja ilikuwa na Bunge lake. Na kuungana kwao ilifanyika kwa kuunganisha mabunge Yao na kuwa Bunge moja.

Sasa napata shida kufananisha na huu wetu maana, wetu umelenga kuwa na Mabunge matatu, la Zanzbar, la Tanganyika na la Tanzania( unaona utofauti wa Kwanza hapo)
Ktk muungano huo wa England na Scotland, Wales ilihesabika Kama ni sehemu ya England ndani ya muungano huo. Ambapo Leo hii Ufalme wa uingereza unahesabika Kama ni Kati ya Scotland, Wales na Nothern Ireland.Ina maana kwamba Scotland na England waliunganisha Mabunge Yao na kuwa Bunge moja chini ya Mfalme mmoja na kisha kuanza kuzitawala Wales na Ireland ambazo Leo hii ni mamlaka ya sehemu ya muungano na Muda wowote wanaweza kuamua kujitawala Kama nchi.

Kwa Mantiki hiyo bado huu wetu ni tofauti sana na UK, maana wetu unataka maraisi 3 na sio mmoja, Mabunge 3 na sio moja.

Also, Kama ingekuwa inaungana Zanzbar na Tanganyika na miongoni mwa hizi mbili, Pemba na Unguja zikajumuishwa ndani ya Zanzbar na Kagera na Kigoma zikajumuishwa ndani ya Tanganyika na tukawa na bunge moja na Rais mmoja mfano Mwinyi maana aliwahi kuwa rais pote, na kisha baadaye, kagera na Kigoma, Pemba na Unguja ziamue kujitenga AMA ziamue kuwa mamlaka huru na zikahesabiwa ktk Muungano Kama mamlaka huru na hata zikiamua kujiondoa ziko huru, hapa ndipo tungesema Muungano wetu unafanana na ule wa Ufalme wa Uingereza

Sijui Kama tuko sawa hapa kiongozi. Inawezekana Mimi ndio naelewa vibaya.
 
Jinga la falsafa nimekupata.
 
Inavyoonesha tatizo ni Muungano. Na kwa kupuuza hilo ndio maana mkanganyiko wa muundo unasumbua! Hakuna pande inayotazama Muungano kwa Sura ya Umoja, Udugu na Ushirikiano katika kujenga nguvu-uimara katika Kujitegemea! Pande zote mbili zinafikiria nitapata nini kwanza kumzidi kete mwenzangu!

Naweza sema kuwa Hakuna nia ya Muungano ila tu Unafiki wa kutumia Muungano kulinda hila za pande hizi mbili! Kama haja ya Muungano ingetoka ndani ya fikra na mioyo yetu, kusingekuwa na wa kusema mimi nataka uzanzibari wangu utukuzwe naye huyu utanganyika wangu uhimidiwe, hali kuwa kuna Utanzania.
Anaita sasa!

Jingalafalsafa, kwa mantiki hii, does it mean hata hii ya serikali tatu ni Kama kuoneana SONI tu kwa kuwa tumekuwa wote kitambo?

Na kwa Mantiki hii inamaanisha kila upande haumtaki mwenzie Bali anakosekana mmoja mtu asiye mnafiki wa kuweka hii wazi?

Kama Majibu ya Maswali yangu ni Ndio, basi hata Mimi nimo kwenye Basi la Mtazamo huu wa Kwamba hapa Kila mmoja anatamani kuchukua 50 zake sema tu ni UNAFIKI NDIO upo Kati Yao wote, kuna kitu hawataki kukiweka wazi tu hapa ( huu ni ukweli mchungu)
 
Mkuu Andrew Nkumbi, hauko mbali sana na nilichosema.

Nilichomaanisha hasa ni kuwa kila upande unamtaka mwinzie, lakini si kama ndugu yake bali kama mtumwa wake! Ndio maana wananchi hawakupewa kabisa nafasi ya kujadili kuuvunja au kuuendeleza muungano. Huu ni urafiki wenye HILA ndani yake! Kinachotokea sasa ni mgongano wa kimasilahi kati ya pande hizi!

Mbaya zaidi miongoni mwa pande hizo nazo kuna makundi yaleyale yanayotaka kutumia kete ya muungano si kama udugu bali kufanyana watumwa!

Hii ni michezo wanayopaswa kucheza watoto primary. Leo inachezwa bungeni. Upeo mdogo wa kufikiri, Fikra mfu, wanatazama hatua moja mbele wanapuuza 10 mbele alikosimama watoto wao! Ni ulimbukeni na upunguani uliopitiliza!
 
Last edited by a moderator:
Kiongozi, JingalaFalsafa, naona sasa moyo wangu unaanza kuwa mweupe maana siku zote haya mambo nilikuwa nashindwa ni jinsi gani mtu unaweza ukayaweka ili watu wayaelewe nashukuru kumbe siko peke yangu ktk Mtazamo huu.

Ni kweli, hesabu za siasa zinawaelemea wanasiasa wetu, hii issue naamini asilimia kubwa walio ktk mchakato huu hawajaiona , na itawawia vigumu sana kuiona na kuielewa

Tatizo kubwa la wanasiasa wetu ambao ndio tumewapa mamlaka ya kutusemea AMA kutuamlia mambo, ni uwezo wao wa kufikiri na kitu hiki kinalipeleka Taifa letu gizani zaidi

Tuko pamoja kiongozi
 
Njema Mkuu wangu Andrew Nkumbi. Tupo pamoja!

Anaita sasa!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom