Tafakuri kuhusu mchakato wa ajira za walimu na matakwa ya NETO na ushauri wangu kwa serikali Tanzania

Joined
Mar 23, 2023
Posts
93
Reaction score
108
UTANGULIZI

Madai ya NETO kuhusu serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwaajiri walimu wote wa 2015-2023, Kufuta usaili kwa kada ya elimu yanaonesha presha kubwa kutoka kwa wahitimu wa elimu na maumivu ya mchakato wasasa.

Presha hii ni ujumbe wa wazi kuwa watu wengi wanahitaji ajira na wengi wao bado hawana kazi. Ikiwemo mimi mwenyewe

Hata hivyo, mimi napenda kua honest madai haya mengi sio specific, measurable, and achievable kwa utekelezaji wa haraka isipokua changamoto za usaili kutokana na vikwazo vya kisheria, bajeti, na muda.

Hii ina maana kwamba, hata raisi awe nani, haiwezekani kutimiza takwa hili ndani ya muda mfupi (2025), huhu ukweli lazima tukubaliane nao ila sina mahana tusidai Ajira zetu ila nimeangalia objectives za NETO wao wanataka immediately relief kwa kutumia matakwa ambayo mengine tulipaswa KUYAFANYA kua Long term demands

Japo kua Madai ya ajira zilizo sitishwa 2015-2020 ni ya MSINGI sana .

KWA NINI NETO WANASISITIZA MABADILIKO?

NETO
wanataka nafasi ya pili kufikiriwa kwa ajira kwa sababu wengi wao:

Hawakuitwa kwenye usaili wa mahojiano (oral interview) baada ya kufaulu mtihani wa maandishi (written aptitude) na kuachwa kwasababu hawakua ndani ya maksi za ushindani kwa ratio ya nafasi za Kazi.

Hihi inauma sana Ndugu zangu unapata 76 ila dashboard inasoma NOT SELECTED FOR ORAL INTERVIEW

Wanaamini kuwa usaili ukifutwa , basi wao watapata ajira moja kwa moja na kupata njia nyingine ya ziada kupata kazi za selikali. Inawezekana ila pia lazima tujue sio mwaka huhu labda kuanzia mwakani.


Hata hivyo, kuna changamoto za msingi kuhusu ombi hili la kuzani usaili unaweza futwa mwaka huhu na kuwapo wao nafuu
:

1. Usaili Hauwezi Kufutwa Moja kwa Moja , ila Njia nyingine ya kuajiri walimu inaweza kupendekezwa, lakini bado itahitaji mchakato wa kisheria kupitia Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Sekretariate ya Ajira ili kutoa tamko rasmi lenye sababu za MSINGI kama alivyo tumia mamlaka hayo kukasimisha kwa TAMISEMI 2010-2011 kwa kusema waombaji ni wachache na nafasi ni nyingi hivyo akuna haja ya usaili mpaka waombaji mtakapo kua wengi na nafasi ni chache.

Lakini pia Hii ni ngumu kutekelezwa kwa haraka kwa sababu:

Wasailiwa waliopitia usaili tayari wamepewa ajira, hivyo kubatilisha mchakato ni ngumu sana kwa mwaka huhu

Sheria inalinda waliopo kwenye kanzidata, hivyo wao lazima waajiriwe kwanza kabla ya mabadiliko ya mfumo mpya ndani cha kipindi cha mwaka mmoja


2. Kuajiriwa Bila Usaili Ndani ya Mwaka Huu Haiwezekani*

Sheria inahitaji kila mtu kupita katika mchakato sawa wa ajira. Kama kutakuwa na ajira mpya, lazima wote wapitie mchakato sawa bila upendeleo.


Means, kama utaratibu wa rondamly selection au direct selection utatumika kama kipindi cha TAMISEMI basi inabidi uwe hivyo kwa wote , na kama kupitia usaili basi kwa wote, hivyo basi, kwa mwaka huhu akuna namna mtu atalamba ajira bila kupitia mchakato sawa na wengine labda mwakani au kwasababu zinazokubalika kisheria au vile president ataona inafaa.

Kama NETO wanataka mabadiliko haya yafanyike ndani ya mwaka huu ili wawe benefited mwaka huhu, ni vigumu kwa sababu hata mabadiliko ya sera yanachukua muda mrefu.

3. Mfumo wa Taifa wa Ajira Unalindwa na Sheria, Mabadiliko hayawezi kufanywa kiholela kwani:

Serikali haiwezi kuajiri watu kwa nusu mchakato huku wengine wakiajiliwa kwa mchakato kamili ndani ya mwaka mmoja labda kuwe na sababu za MSINGI za kisheria

Mchakato huu unasimamiwa na Tume ya Utumishi wa Umma (PSRS), ambayo haina mamlaka ya kutoa ajira nje ya mfumo wake wa kisheria ulio fafanuliwa kwenye SHERIA NA KANUNUNI ZA UENDESHAJI MCHAKATO WA AJIRA SEKRETARIATE YA AJIRA

Kwa hiyo, kutarajia kuwa walimu wote wa 2015-2023 waajiriwe moja kwa moja ni unrealistic and unachievable kwa muda mfupi. Labda kama selikali itatoa ajira zote na kufanya mchakato wa usaili usiwe mahana this Year. Unless tungoje mwakani hata kama awe nani.

MWISHO USAILI LAZIMA HUWEPO AKUNA SABABU ZA MSINGI ZA KUFUTA USAILI TUTAKE TUSITAKE LABDA KUBORESHWA KWA MAZINGIRA YA USAILI

MSONGO WA MAAMUZI SERIKALI INAYOKABILIA NAO

Kwenye akili yangu nawaza mambo matatu:

Ikiwa serikali itaamua kuongeza nafasi za ajira za walimu kiasi cha kugusa walalamikaji nje ya mfumo wa kisheri, itakumbana na changamoto kuu tatu:

1. Idadi Ndogo ya Walioitwa Usaili wa Mazungumzo (Oral Interview) Ikiwa ajira zitaongezwa, bado kuna tatizo la rasilimali na muda wa kufanya usaili mpya au kuitisha waombaji wapya. Serikali italazimika kufanya maamuzi magumu kuhusu:

Kuwaita watu wapya kwenye usaili.

Kuanzisha mchakato mpya wa ajira, jambo ambalo linahitaji bajeti kubwa.

Kushughulikia hili bila kuathiri mchakato wa uchaguzi mkuu wa 2025. Kitu ambacho hata ningekua President ningumu kumeza



2. Malalamiko ya Wengi Walioshindwa Kufika Oral Wengi wa waliofaulu mtihani wa maandishi lakini hawakuitwa kwenye oral wanahisi kutotendewa haki.

Ikiwa serikali itaongeza nafasi chache, bado kundi hili halitapata suluhisho la moja kwa moja kwa sababu:

Waliopo kwenye kanzidata watapewa kipaumbele kabla yao kwa mujibu wa sheria

Mfumo wa ajira hautaweza kubadilishwa haraka

3. Uteuzi Bila Kupitia Usaili* Kuchagua waombaji moja kwa moja bila usaili ni kwenda kinyume na sheria za ajira kwani wengine wamesha pitia mchakato kamili . Ikiwa hii itafanyika, itasababisha:

Migogoro ya kisheria.
Na itabidi ifanyike kwa walimu wote mpaka kada walizo kwisha kupangiwa kazi

Malalamiko kutoka kwa waliofanya usaili na kupata ajira kupitia mfumo rasmi.
Political interested na kashfa za rushwa zitakua kubwa haijawahi kutokea


Kwa hiyo, hata kama serikali itaongeza nafasi za ajira, haitawezekana kuajiri watu bila kufuata mfumo wa kawaida kwa mwaka huhu ili kutengeneza usawa wa kisheria na uhalali wa kimchakato vinginevyo ngumu ilo lazima tulijue.

USHAURI KWA NETO: KUWA NA MATARAJIO YANAYOWEZEKANA

Badala ya kutaka kufuta usaili au kuajiriwa moja kwa moja , NETO inapaswa kuzingatia mfumo wa kisheria na kuwasilisha madai yanayoweza kutekelezeka kwa muda mfupi na mrefu ili kuwezesha member wake kupata nafasi kwa mwaka huhu kwa kuomba nafasi za kazi kuongezwa. Na madai ya ajira za 2015-2020 yakiendelea

1. Kufanya Maboresho ya Sheria za Ajira Sheria inaweza kubadilishwa ili kuweka kipengele kinachosema:

Waliopata alama za juu kwenye written aptitude lakini hawakuitwa kwenye oral, wapewe nafasi ya kusailiwa moja kwa moja ( Re selected for Oral Interview) ikiwa nafasi za ajira zinaongezeka ndani ya mwaka mmoja, na waliopo kwenye kanzidata wamekwisha ili Incase government itakua tayali kuongeza ajira


2. Kutumia Mamlaka ya Rais Kwa kuwa kubadili sheria ni mchakato mrefu, njia ya haraka ni kwa Rais kutoa tamko rasmi (decree) la kuwaruhusu waliofaulu mtihani wa maandishi lakini walikosa nafasi kupata usaili wa oral ikiwa ajira zimeongezeka ndani ya mwaka huo huo ukiwa kama pendekezo la dharula hasa kama Gavornment itaongeza nafasi nyingi zaidi.


3. Kuwa na Msimamo wa Kisheria na Kitaasisi NETO inapaswa kuelewa kuwa:

Kuajiri bila usaili hakutowezekana ndani ya mwaka huu labda mwakani. Lakini tifauti za kimichakato zinaweza kua hatari hasa akifika raisi mungine na kuto kubali kundi fulani lililopata ajira bila mchakato rasmi uliokamilika kwa wote kwasababu:

Haki za waliopo kwenye kanzidata haziwezi kupuuzwa.*

Mabadiliko madogo yanaweza kufanikishwa haraka kuliko mabadiliko makubwa yasiyotekelezeka.


SULUHISHO BORA LINALOWEZEKANA HASA KWA SELIKALI


Serikali inaweza kufanya maboresho yafuatayo ili kupunguza malalamiko ya NETO na wengine waliokosa nafasi ya oral interview bahada ya kuongeza ajira :

1. Kupendekeza Mfumo wa Pili wa Uteuzi Ikiwa ajira za walimu zitaongezwa ndani ya mwaka mmoja, basi wale waliofaulu written aptitude lakini hawakuitwa oral waingizwe moja kwa moja kwenye usaili wa oral ili kupunguza gharama na kuwafanya na wao wapate haki yao bila kwenda nje na utaratibu wa kitaifa

Njia hii inahakikisha kuwa kila mtu anafuata mchakato sawa wa ajira.


2. Kuweka Kigezo cha Pili kwa Kanzidata Ikiwa nafasi mpya za ajira zinapatikana baada ya walio kwenye kanzidata kuajiriwa kabla ya kuisha mwaka mmoja, basi waliofaulu aptitude test lakini hawakuitwa oral wapatiwe kipaumbele cha kuitwa oral interview kupambania nafasi mpya ila wao wasiwe na KANZIDATA.

Hili litahakikisha kwamba kila mtu aliyefaulu anapata nafasi sawa kwa mujibu wa sheria.


Hii inaweza kuwa njia ya haraka kuliko kusubiri mabadiliko ya kisheria kwa miaka mingi.



MUHIMU

Ikiwa Teachers wanataka mafanikio ya kweli, ni lazima waelewe uhalisia wa mfumo wa ajira. Kuajiri walimu wote wa 2015-2023 ndani ya mwaka huu haiwezekani .

Kwa maneno rahisi: Mabadiliko ya haraka ni yasiyowezekana, lakini maboresho yanawezekana!


SIONGEI HAYA KAMA NINA-DEGRADE MADAI YA WENZETU

Lakini naongea haya kuonesha ni kipi ambacho kinaweza kupatikana kwa sasa na kipi ambacho hakiwezi kupatikana kwa haraka hata kwa nguvu ya wapinzani. Pia nazungumza haya kwa ajili ya mediation—kwa upande wa sekta binafsi, na sisi jobless na serikali.

Nafahamu walimu wengi hawapendi kusikia haya, lakini huu ndio ukweli. Mfumo wetu wa kisheria na kijamii ulivyo sasa hauruhusu mabadiliko yote kufanyika mara moja. Kama huwezi kuukubali ukweli huu, basi utalazimika kusubiri hadi 2026, ambapo mazingira ya kisheria na kisera yanaweza kuwa tofauti. Kwa hiyo, sisemi kuwa walimu wasifuatilie haki zao za maslahi, lakini pia wasitegemee kuwa kwa kufutwa kwa usahili fulani, basi moja kwa moja watanufaika mara hiyo hiyo mwaka huhu.

Kuna umuhimu wa kutambua tofauti kati ya MAHITAJI YA MUDA MFUPI NA MAHITAJI YA MUDA MREFU.

MAHITAJI YA MUDA MFUPI NA MUDA MREFU

Ni kweli kuwa serikali yetu inaweza kuajiri walimu wengi zaidi. Hata hivyo, ili hilo litekelezeke, lazima tukubali kama taifa—kwa upande wa serikali, sekta binafsi, NETO, na wananchi kwa ujumla—kwamba kuna makosa ambayo tumeyafanya kama taifa. Lazima tuyakubali na tuyarekebishe ili kuleta mfumo mpya wa ajira ya hasa kwa walimu, wenye kupunguza ukame wa ajira kwao, huku tukitafuta suluhisho la haraka kwa wale wanaoumia sasa.


MAOMBI YANGU KWA SERIKALI

Katika hili, kuna ombi moja kwa serikali:
U

Kwa uhalisia, sekta binafsi ya elimu inapaswa kutazamwa kama mshirika, si kama mpinzani wa serikali vinginevyo selikali ijiandae kuajili walimu wote. Serikali inapaswa kushirikiana na wadau wa elimu binafsi na kuunda mfumo ambao utasaidia kuajiri walimu kwa mishahara mizuri na kwa ulinzi wa kisheria. Hii inaweza kufanikishwa kwa njia zifuatazo:

1. KUTOA MOTISHA KWA TAASISI BINAISI ZA ELIMU


Serikali inaweza kuwapa unafuu wa kodi au ruzuku ili ziweze kuajiri walimu kwa mishahara bora na kwa mkataba wa haki.


2. KUSAINI MAKUBALIANO KATI YA SERIKALI NA SEKTA BINAISI YA ELIMU

Kupitia makubaliano haya, taasisi binafsi zitalazimika kuzingatia viwango vya mshahara na mazingira ya kazi ya walimu.


3. KUANZISHA AU KUPISHA MSWADA WA TANZANIA TEACHERS BOARD HARAKA

Bodi hii iwe chombo cha kusimamia taaluma ya ualimu na kutoa leseni kwa walimu, ili kuwafanya walimu waajiriwe kwa heshima na kulindwa kisheria katika sekta zote na wale wasio walimu wasifanye kazi zetu.



KUIMARISHA SHERIA ZA AJIRA KWA WALIMU

Kwa sasa, walimu wengi wanakabiliwa na hali mbaya kazini, huku wengine wakifukuzwa kiholela kwenye sector binafsi walimu wanaishinkama wanafunzi wasio kutambua . Ni jambo la kusikitisha kuona mwalimu anapoteza kazi ghafla kwa sababu tu ya mabadiliko ya sera katika shule au kwa kuwa amepinga jambo fulani au mgongano wa ki maslahi na wamiliko . Hili si sawa! Serikali inapaswa kuhakikisha:

1. SHERIA ZA ULINZI WA AJIRA KWA WALIMU


Zinapaswa kuimarishwa ili hakuna mwajiri anayeweza kuwafukuza kiholela.


2. MCHAKATO WA HAKI KWA WALIMU

Unapaswa kuwa wa haraka na wa haki, ili walimu wasihangaike wanapodhulumiwa kazini.


3. MKATABA WA KITAIFA WA WALIMU

Unapaswa kutungwa, ukieleza mshahara wa kiwango cha chini, haki za walimu, na mazingira bora ya kazi.
Except kwa shule changa

4. MIKATABA YOTE YA AJIRA YA WALIMU WENYE LESENI KATIKA SEKTA BINAISI LAZIMA IWASILISHWE SERIKALINI


Serikali iwe na nakala ya mkataba wa mwalimu yeyote anayeajiriwa katika sekta binafsi ili kuhakikisha haki zake zinalindwa.

ULINZI WA AJIRA YA WALIMU KATIKA SEKTA BINAISI

Kabula mwajiri hajavunja mkataba wa mwalimu au kumfukuza kazi, serikali lazima iwe imejulishwa rasmi. Hii itahakikisha kuwa hakuna mwalimu anayefutwa kazi kiholela au kunyimwa haki zake. Kwa sasa, walimu wanakuwa kama DIGIDIGI—wanakimbizwa na kufukuzwa kazini bila sababu za msingi, bila uangali uhhzi wa serikali. Hali hii lazima ikomeshwe mara moja!

MAHITAJI YA MIKATABA YA AJIRA KWA WALIMU

Serikali inapaswa kuanzisha masharti muhimu kwa taasisi zote za elimu ambazo zinapanga kuajiri walimu:

1. MIKATABA YA AJIRA YA WALIMU LAZIMA IPITIE NA KUIDHINISHWA NA SERIKALI

Hii itahakikisha kuwa mikataba inaendana na viwango vya haki za walimu, huku ikiwezesha mazingira bora ya kazi na ufanisi katika elimu na kutoa security kwa walimu wote


2. GOVERNMENT MUST BE NOTIFIED DURING CONTRACT CHANGES

Hii itasaidia kudhibiti mifumo ya unyanyasaji, ambapo mwalimu anaweza kuachishwa kazi kiholela na bila taarifa ya kutosha.


3. TIMELY TERMINATION OF CONTRACTS

Muda wa kuachishwa kazi au kusimamishwa kazi lazima ujulishwe serikalini mapema.

KUJITOLEA NA INTERNSHIP KWA WANAOPATA MAFUNZO KATIKA TAASISI ZA ELIMU

Pia, ni muhimu kwa serikali kuona muhimu wa kujitolea na internship kwa wale wanaopata mafunzo katika taasisi za elimu. Watu hawa wanapaswa kuwa na fursa ya kujifunza na kukuza ujuzi, lakini pia wawepo na utaratibu wa kuwalinda ili wasiwekewe mzigo wa ajira ya kutojulikana au dhuluma, badala ya kuwa sehemu ya timu ya kudumu.


KUMALIZIA

Kwa hivyo, masharti haya yataongeza kiwango cha ulinzi kwa walimu, wakiwa katika sekta binafsi au umma, na kuboresha mazingira ya kazi kwa manufaa ya kizazi kijacho cha walimu. Serikali lazima ichukue jukumu la kulinda haki za walimu, kuhakikisha kuwa hakuna mwalimu anayeachishwa kazi kiholela, na kwamba mazingira yao ya kazi ni salama, yenye haki na stahili.

Licha ya changamoto zote, kama taifa, tujitahidi kuelewa kuwa mabadiliko haya ni ya manufaa kwa jamii nzima, na yanahitaji ushirikiano kutoka pande zote: serikali, walimu, na wananchi kwa ujumla. Tutakapokubali ukweli na kufanya juhudi za pamoja, tutaleta mfumo mpya utakaojenga taifa letu kwa manufaa ya kizazi kijacho.


ALL IN ALL, SERIKALI INAPASWA KUIMARISHA MASLAHI YA WALIMU NA KUHAKIKISHA WANAPATA ULINZI WA KISHERIA.

Kwa sasa, walimu wanafukuzwa kama watoto. Mwalimu amekwenda usahili wake kwa siku moja tu, tayari anafukuzwa. Hili si sawa. Walimu ni nguzo ya taifa letu, na kama kweli tunataka maendeleo, basi lazima tuwalinde kwa vitendo, si kwa maneno tu.



BY JOSEPHAT NDUMBARO
DAR ES SALAAM, TANZANIA

careermasteryhuborg@gmail.com

AHSANTE
 
Sijasoma mada ila usaili ni lazima hata kama mtahiniwa asipotaka.
Utumishi shikilieni hapo hapo, msiachie.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…