Tafakuri kuishinda nafsi Nguvu iliyosahaulika

Tafakuri kuishinda nafsi Nguvu iliyosahaulika

Shayu

Platinum Member
Joined
May 24, 2011
Posts
608
Reaction score
1,655
Leo nakuja na kitu tofauti kidogo lakini naamini kile nitakachoandika kitasaidia baadhi ya watu ambao wanapenda kupata mabadiliko ndani yao. Mabadiliko haya ambayo yatamjenga na kumkuza kikakili na kuwa na mtazamo tofauti kuhusu maisha na ubinadamu.

Mada yetu ya leo nitaongelea kuhusu kitu kinachoitwa ''KUISHINDA NAFSI'' binadamu ameumbwa na matamanio , moyo wa binadamu umejaa hila, choyo, wivu na kila aina ya vitu ambavyo binadamu hakupaswa kuwa navyo kwakuwa vinamuadhiri kiafya na kiroho. Kazi ya dini na falsafa ambayo kwa miaka mingi nimekuwa nikisoma nikuondoa hizi chembe chembe mbaya katika binadamu na kumjenga binadamu kuwa kiumbe bora zaidi kuliko alivyo sasa.

Matatizo mengi tuliyonayo katika dunia hii yanatokana na binadamu kushindwa kuishinda nafsi, kushindwa kuzuia matamanio yake na hivyo kujikuta akiangukia kwenye makosa kila wakati. kushinda nafsi ni nidhamu ambayo kila mmoja wetu ni muhimu na ni lazima kupambana ili kuwa na uwezo huo, Binadamu hawezi kujitawala pasipo kushinda nafsi yake mwenyewe. Amani ya dunia haitoweza kupatikana pasipo binadamu kuweza kushinda nafsi zao. Kushinda nafsi ni kujitawala. Ni Kwa kushinda nafsi zetu tu ndio tutakapoweza kutenda haki na haki italeta amani miongoni mwetu.

Binadamu kamwe hatoweza kukua kiakili kama ataongozwa na matamanio yake na hisia zake badala ya fikra. Kwahiyo kazi ya falsafa na dini ni kufanya ''lower nature'' yaani matamanio , hisia, kuondoka na binadamu kutawaliwa na higher nature yaani reason and spirit.

Tofauti tuliyonayo kati yetu na wanyama ni akili, nje ya akili wote ni wanyama tu. Binadamu akiruhusu matamanio, hisia na uchu kumtawala hatokuwa tofauti na mnyama. Uzoefu unaonyesha binadamu anaweza ku improve na kuwa kiumbe bora zaidi ya alivyo sasa.

Matatizo mengi tuliyonayo katika dunia hii yanatokana na ujinga wa kushindwa kutawala nafsi zetu. Kwahiyo amani haitoweza kupatikana. Binadamu ambaye anashindwa kutawala nafsi yake hajakamilika ni lazima afanye juhudi zote ili ashinde nafsi yake.

Sisi binadamu ni zao la mawazo yetu, mawazo yetu yanatujenga na kutubomoa. Mawazo mazuri hutujenga kuwa watu bora na mawazo mabaya ni kinyume chake. Kwahiyo mtu ambaye mwili wake una harmony ni mtu yule ambaye anaweza kujitawala na mawazo yake yana uhusiano mzuri na anaongozwa na fikra.

Kuiba ni kushindwa kutawala nafsi; ni ukosefu wa self control (nidhamu), kumchukua mke wa mtu vile vile. kwahiyo kwa kufanya mambo haya ni dhahiri tunaharibu mahusiano yetu na dunia haitaweza kuwa na amani. Tutaheshimu wengine na mipaka yetu pale tu tutakapoweza kushinda nafsi zetu na kila mtu kutimiza wajibu wake.

Kwahiyo tutajenga jamii zetu vizuri na nchi yetu ikiwa tu watu wetu watakuwa na uwezo wa kushinda nafsi zao. Kushinda tamaa zao na kufanya yale tu ambayo yanaendana na fikra sahihi.

Binadamu anapofanya mambo haya sio yeye anayefanya ndani ya binadamu kuna vitu viwili kila wakati vinapingana lower nature yake ambayo humshawishi kufanya mambo mabaya na higher nature ambayo ni reason tunaposhindwa kufuata reason na kufuata tamaa zetu kila wakati binadamu huwa tunatumbukia kwenye uharibifu.

Nimesoma sana na kutafakuri kila nilichosoma na kutafakuri kinaniambia ukweli huu binadamu ni lazima ashinde nafsi yake na tamaa za mwili na aongozwe na fikra ikiwa anataka kuwa binadamu bora na mwenye amani ya roho, ikiwa anataka kuhifadhi nafsi yake dhidi ya uharibifu.

Vita vyote na vurugu na fujo vinatokana na ujinga wa hali ya juu wa binadamu, vinatokana na ujinga uliopitiliza wa kushindwa ku control nafsi kama alivyosema plato kwenye kitabu chake cha ''THE REPUBLIC'' Alipoulizwa ni nani afaaye kuwa kiongozi wa wengine alisema; Ni yule awezaye kutawala Nafsi yake kwakuwa asiyeweza kutawala nafsi yake hutawaliwa na kila aina ya tamaa na hivyo hataweza kutawala wengine kwa haki atawagandamiza ili kutimiza matamanio yake ya mwili, uchu wa mali na starehe za dunia.

Ikija kwenye vita mtu yule awezaye kutawala nafsi yake ni mpambanaji hodari na mwenye akili zaidi ya wengine. Lack of self control always brings shame. Self control brings power and honor.

Kwasababu ili uwe na uwezo wa ku control the self ni lazima uwe na uwezo wa focus attention kubwa ku control all of your action watu wa namna hii always huwa na akili nyingi kichwani. Mawazo yao hukusanywa na kuongozwa katika mkondo sahihi na wenye manufaa.
Kwahiyo swali la nani awe kiongozi wetu ni yule mwenye busara na self control ya hali ya juu.

Uwezo huu kila mtu anaweza kuwa nao lakini inahitaji jitihada ili kufanikiwa na kamwe hatutaweza kutenganisha ''busara na nidhamu'' yaani Wisdom and self control. The fruits of wisdom and self control is joy and gladness. Lack of self control always brings shame. Any fool lack self control.

Mwisho napenda kusema hakuna nguvu kubwa ambayo amepewa binadamu na mungu na anashindwa kuitumia kama nguvu ya kuishinda nafsi utakapoishinda nafsi yako wewe ni mtu mwingine katika dunia hii you are a '' POWER''
 
Back
Top Bottom