Tafakuri Maisha / Kifo

Tafakuri Maisha / Kifo

Shayu

Platinum Member
Joined
May 24, 2011
Posts
608
Reaction score
1,655
Huu ni wakati wenu ambao mnaishi kwa sasa duniani. Kumbukeni mabadiliko yako ndani yenu. Mnabadilika kutoka utoto kwenda ujana na uzee. Utakapokuwa mzee, hautokuwa kama ulivyokuwa kijana. Unajua kwa hakika kifo kinakuita. Na hakuna atakayeishi milele.

Kitu kimoja tunapaswa kuzingatia duniani tunapita. Kama majani makavu yadondokayo kutoka katika mti sote tutapita. Tupendane tuishi kwa amani miongoni mwetu.

Na katika kila kitu chetu tuifanye busara ituongoze. Maisha hayasimami na muda nao hausimami. Sote wakati wetu ukifika tutafutika na kizazi kipya kitachipukia.

Utakapokufa utaacha watoto pengine familia na mke au wajukuu kadhaa. Kila mtu na siku yake ya kufa.

Lakini tuna tumaini tutakaowaacha baada ya sisi kufa wataendelea vyema katika maisha yao.
Kama mzazi utatumaini watoto wako utakapokufa wataendelea kupendana na kuwa kitu kimoja. Familia haitagawanyika.

Kwasababu hakuna kitu bora katika maisha ya mwanadamu kama familia iliyosimama imara. Utakapoona watoto wako wa kike na wakiume wakiwa wamoja. Na wakiwa wana afya njema ya kimwili na kiakili. Na wakiwa na furaha pia.

Kitu gani bora atakachokiacha binadamu baada ya kufa, kama familia iliyosimama yenye umoja na upendo?
Utakapokuwa na watoto wanaokuheshimu kama baba, Hufikirii kwamba utakapo kaa kwenye kochi, glassi ya maji itapita vyema kooni?

Binadamu; Kuna wajibu mkuu kama ule wa kulea watoto katika nidhamu na maadili ya hali ya juu?
Naongea na nyinyi nyote kama binadamu wenye busara na wenye kuelewa maneno yenye hekima.
Muda haukamatiki, uzee una karibia. Na hakuna atakaye epuka kipindi hiki labda achukuliwe mapema na kifo { Maanani} amchukue.

Je kuna kitu bora zaidi ya nidhamu? Embu fikiri kidogo. Nidhamu huleta order katika matendo ya binadamu. Na kumfanya atende katika usahihi. Nidhamu humfanya mtu kuchunga mdomo wake, na kuchagua maneno ya kuongea. Maneno ya mwenye nidhamu ni matamu kama asali.

Nawashauri tutafute nidhamu ni nzuri kwa roho zetu. Hakuna chenye thamani kama nidhamu. Itakupatia heshima na hekima. Nidhamu itajenga nyumba yako na familia yako iwe imara.

Ninaweza kuongea kuanzia sasa hivi hadi asubuhi ni hayo tu, ninayowaacha nayo. Natumaini yatatafuta nafasi mioyoni mwenu na kuwajenga. Na mtasimama imara kwa yaliyo sahihi kwenu, kwa familia zenu na kwa Taifa kwa ujumla.


Alamsiki.
 
Back
Top Bottom