Tafakuri: Nini hatma ya elimu Tanzania?

Tafakuri: Nini hatma ya elimu Tanzania?

Kashindi

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2011
Posts
349
Reaction score
250
Wana jamvi na wadau Wa elimu hapa nchini kila mtu macho masikio, na akili yake kwa muda Fulani vilijaribu kuelekezwa kwenye matokeo ya kidato cha nne yaliyotangazwa hivi karibuni, huku ikionyesha kuwa ufaulu umeongezeka kwa 15.19%.

Niipongeze serikali kwa juhudi ndogo iliyofanywa na kuleta Matokeo makubwa Sana. Matokeo hata Mimi binafsi nayaita ya kisiasa kwa sababu upangaji Wa alama za ufaulu na madaraja ya masomo yaliyo anzishwa Kama A, B jumlisha na B ya kawaida huku kukiwa na alama E. haujashirikisha wadau muhim Wa elimu kama walimu na hata viongozi Wa chama cha walimu Tanzania.

Akiongea Leo katika kipindi cha Tuongee asubuhi kinacho tangazwa na radio one, katibu Wa chama cha walimu Tanzania bwana Ezekiel Oluochi ameonesha kutoridhishwa na upangaji wa alama na madaraja ya ufaulu yaliyotangazwa na serikari.

Mimi Kama mwalimu mwanafunzi Wa chuo Kikuyu cha Dar es salaam nasikitika kwa kuona kuwa hatma ya elimu ya Tanzania iko mashakani kwani waliofaulu kwa viwango vya chini au waliofeli na kufaulishwa ndo wanaweza kuwa walimu Wa kufundisha watanzania hapo baadae.

Je wewe kama mdau Wa elimu mkereketwa na mpenda maendeleo Wa nchi nini Una maoni gani kuhusu matokeo haya?

Je unaiona wapi Tanzania kielimu?

He kwa mfumo juu harakishi Wa upangaji matokeo tuna waandaa Watanzania katika solo LA ajira?

Tafadhali matusi hayatakiwi kama huwezi changia pita mtu.
 
Kulikuwa na haja kubwa ya kubadili madaraja katika elimu, kuweka madaraja yanayo fanana katika ngazi zote za elimu (kuanzia chuo kikuu mpaka kindagate), hii inasaidia kujua mwenendo halisi wa elimu kwa ujumla baada ya hapo mambo mengine yanaendelea.
Kwa kubadili madaraja ni sawa kama kuna kitu cha kuangalia zaidi ni ufaulu wenyewe umekaa vipi.
 
Back
Top Bottom