jamani kwa muda sasa nimekua nikisoma na kusikia walimu wengi wakilalamika juu ya chama cha walimu. Yawezekana madai yao yana msingi, hata hivyo nina maoni binafsi;
1. Kusema walimu wenye vyeti na diploma ni vibaraka wa CWT na hawana pa kwenda, ni kuwatukana wazee wetu ambao kwakweli hata mtoa mada wamemfikisha hapo anapoona ni pa juu sana SHAHADA.
2. Nyerere alianza safari ya ukombozi na wa nchi akiwa na hao wa elimu ya chini. Shahada zilipoongezeka kwa zama hizi na ufisadi ukaongezeka, hatuna jambo kubwa la kujivunia kwa wingi wa shahada nchini isipokua kitakwimu. Wenye shahada wameongezeka lakini ndo kwanza nchi yetu bado ina mgao wa umeme na hata maji. Shahada zimeongezeka lakini vifo vya mama wajawazito na watoto chini ya miaka 5 bado viko juu. Tunashada nyingi lakini watoto wetu wanafeli kwa wingi usioelezeka.
3. Walimu mkianza kugawanyika kwa kufuata elimu zenu uwezekano wa kusonga mbele ni mdogo sana maana wote mnahudumiwa na wizara zilezile. Wenye shahada ingieni kwenye hicho chama shikeni mkiongoze wenyewe, msiiende kugombea nafasi mkiwa mmeweka shahada zenu mbele haitawafaa kitu. Amini nawambieni mkijitenga na wa cheti wakasalia pekee yao chama chao kitakua na nguvu maana ni wengi na pili watajiona wamedhalilishwa na wasomi. Mtakua na maadui wawili serikali na chama cha walimu wenye cheti.
3. Kuhusu CWT hapa nitaongea kwa uzoefu kidogo niliouona kwenye hiki chama, kuna wilaya hiki chama ovyo kabisa lakini lazima tukubali yapo maeneo walau kuna jambo unaweza kusema wanafanya kitu. Mfano nimeshuhudia CWT ikimshitaki DED kwa niaba ya mwl aliyekua amefukuzwa kazi kimakosa, nimejionea mwenyewe CWT ikiwasaidia wanachama wake kwa masuala ya kisheria, kifedha mara nyingi, na hata walimu wamepageuza kimbilio lao. Imefikia pahala walimu wanaenda kushtakiana CWT na si kwa DED.
4. Walimu wote shikamaneni mkianza kugawanyika mambo mengi mtafanyiwa ya ajabu.
5. Ukweli usiopingika CWT inahitaji sura mpya katika wilaya nyingi na mikoa mingi na hata taifa. Jitahidini vijana walimu muingie humo sasa, mfanye mapinduzi ya chama kiwe na sura ya kupigania haki za walimu si kama kilivyo sasa kwa sura ya jumla. Watoeni Msulwa na wengine maana ni watu wa serikali wapo kwa maslahi ya aliteyewatuma kazi na si walimu. Muda umefika kwa chama kuanza harakati za kudai mambo yanayowahusu walimu wote na si kudai madai ya hamisho na madaraja ambayo kimsingi si ya walimu wote.
Tuendelee kujadili.