Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 33,679
- 49,841
Nazungumza na wale wenye miaka 35+
Jaribu leo utoke peke yako, na uende kwenye mazingira tulivu, kama yanaruhusu kupata kinywaji au kula matunda yoyote fanya hivyo.
Jitafakari ulipotoka, mpaka hapo ulipo sasa.
NB. Hakuna mtu atakayeuza nyumba yake ili kutatua changamoto zako.
Jaribu leo utoke peke yako, na uende kwenye mazingira tulivu, kama yanaruhusu kupata kinywaji au kula matunda yoyote fanya hivyo.
Jitafakari ulipotoka, mpaka hapo ulipo sasa.
- Jiulize haya maswali; leo hii nikifungwa gerezani ni nani atakuwa karibu na mimi au na familia yangu? Jaribu ku 'screen' kuanzia ndugu zako, mwenzi wako, watoto wako, marafiki zako n.k
- Hivyo hivyo, jiulize tena; leo hii nikiwa kitandani najiuguza kwa muda mrefu labda miaka miwili nikiwa siwezi kuinuka wala kujisaidia, ni nani atakuwa karibu na mimi? Jaribu tena ku 'screen' kuanzia ndugu zako, mwenzi wako, watoto wako, marafiki zako n.k
- Hivyo hivyo, jiulize tena; leo hii nikiondokewa/kufiwa na mtu muhimu sana kwangu/nguzo yangu, ni nani atakuwa karibu na mimi? Jaribu tena ku 'screen' kuanzia ndugu zako, mwenzi wako, watoto wako, marafiki zako n.k
NB. Hakuna mtu atakayeuza nyumba yake ili kutatua changamoto zako.