Uchaguzi 2020 Tafakuri ya kina kuhusu uchaguzi

Uchaguzi 2020 Tafakuri ya kina kuhusu uchaguzi

lutemi

JF-Expert Member
Joined
Dec 24, 2013
Posts
1,748
Reaction score
1,388
kabla hujaenda kushiriki kuchagua au kuchaguliwa fikiria.

Kuchaguliwa
Wewe utasimama kwa niaba ya watu wote. Je unajua watu wataweka tumaini kwako? Je unaakili timamu? Kumbuka watu wakifa kwasababu yako utadaiwa.
Watu watahitaji uwe mfariji wao....wafariji
Mshauri wao.....washauri.
Mwonyaji wao.....waonye.
Kwa ujumla wewe unaenda kuwa sehemu ya maisha yao kwa miaka mitano ambayo ni umri wa mtu toka kutungishwa mimba mpaka kuanza shule.
Una mambo mawili kuchukua Baraka kwa Mungu au laana itakayokutafuna milele.


Kuchagua.
Tunapoenda kuchagua ngazi zote tuende na akili timamu isiyofunikwa na midadi (emotions)
Kabla ya kuchagua jiulize hivi Nina akili timamu? Nimefikiria vya kutosha? Kwa kitendo cha kuweka tu vema kinaenda kuathiri wengi , ikianza na wewe mwenyewe,watoto wako familia yako na taifa kwa ujumla.
Jihoji kwa makini sana
Walimu miaka mitano umenufaika na nini?
Wafanyabiashara
Wakulima
Wachimbaji migodini
Kumbuka unaenda kuchagua mtu ambae hathamini maisha yako, utu wako ,Uhuru wako maana Yake unayafuata mateso miaka 5 tena.

Nina omba sana uchaguzi huu sisi tuwe waelimishaji wa familia zetu ili tusigubikwe na mihemko kwa vitu vinavyopita kama kanga T-shirt au Madera.
Ndimi Mdogo wenu mtanzania halisi.
 
Cha kufanya tu ni kutomchagua mgombea yeyote wa ccm la sivyo inchi itabaki maskini siku zote.
 
Cha kufanya tu ni kutomchagua mgombea yeyote wa ccm la sivyo inchi itabaki maskini siku zote.
Wasaliti je? Maana wapo pande zote wachaguliwa na wanaochagua
 
Back
Top Bottom