Shayu
Platinum Member
- May 24, 2011
- 608
- 1,655
Nitaanza andiko langu na maneno kutoka kwa raisi wa zamani wa marekani, John Adams. Ni muendelezo wa makala zangu juu ya msingi muhimu zaidi katika ujenzi wa taifa lolote. Msingi wa maadili. Mimi si mtu wa kwanza kuliona hili na wala sitokuwa wa mwisho. Kea miaka mingi wanafalsafa na viongozi wengi wamezungumza nami naendelea kuzungumza umuhimu wake. Kwasababu ili taifa liwe moja ni lazima tulizingatie.Kuna vitu ambavyo vinafanya taifa liwe moja na vingine hutawanya taifa. Uongozi wa haki ni moja wapo. Pale wananchi wanapoongozwa kwa haki taifa mara zote huwa moja.Kabla sijaenda mbali John Adams; Raisi wa zamani wa marekani alisema." We have no government armed with the power capable of contending human passions unbridled by morality and religion. Avarice, ambition, revenge or gallantry would break the strong cords of our constitution as the whale goes through a net ...our constitution was made only for a moral and religious people. It is wholly inadequate to the government of any other"l. Tunajifunza katika historia bila maadili hakuna taifa litakalo simama na ni vyema na sisi tukajifunza kutokana na historia. Mambo yote mazuri ambayo binadamu anapaswa kuyapata yatapatikana kwenye taifa lenye maadili na si vinginevyo. Amani na maendeleo vitapatikana tu kwenye taifa lenye maadili ya kutosha.Hakuna kiongozi mwenye uwezo wa kutawala taifa lilokosa maadili na kuleta Order. Kwahiyo jukumu la kujenga taifa bora na watu bora ni letu wote. Ni muhimu kujenga maadili ya taifa letu wakati bado mapema, mambo yakiwa hayajaharibika na taifa letu kushindwa kutawalika. Kwa wale wanaofikiri kupata madaraka ya kuongoza taifa hili ni nafasi ya kujilimbikizia mali wamelishindwa taifa hili. Kwasababu hatua ya kwanza ya utawala wowote kuwa wa kikandamizaji ni kujilimbikizia mali kwa viongozi ndio chanzo cha uovu katika nchi. Malengo yetu kama taifa sio kupata Mali tu bali kuna vitu ambavyo vimetuunganisha na kufanya umoja wetu. Na viongozi wanawajibika kutawala taifa hili kwa haki. Viongozi wakianza kujilimbikizia mali maskini hawatapata kitu. Na watu watakosa Uhuru wao. Akili za viongozi wetu lazima ziwe kwenye kuongoza tu. Wajitoe kwenye kujilimbikizia mali.Elimu yetu pia lazima ilenge kumjenga binadamu wa taifa hili kuwa bora.