Tafsiri binafsi=maana ya mfuasi/wafuasi

Tafsiri binafsi=maana ya mfuasi/wafuasi

Idd Ninga

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2012
Posts
5,497
Reaction score
4,775
Kikawaida MFU ni mtu aliekufa (kwa lugha ya kuonyesha hadhi ya kiumbe) ambae anaweza akawa katika hali mbili.
moja akiwa hai na ya pili akiwa maiti.
katika ile hali ya kuwa maiti,mfu anakuwa ni bora kwa kuwa si uwezo wake bali wa aliemuumba.
ila mtu anakua na hasara zaidi pale anapokuwa mfu alie hai.
kwa maana,hatumii fikra zake,akili zake,mawazo yake,elimu yake,ujuzi wake bali hutumia nguvu zake.
mfu alie hai,hawazi kwa kichwa chake.
yeye husubiria mwenzake aweze ndipo yeye hutenda tena kwa kuasi.
ndio maana akaitwa mfuasi,yani MFU alie ASI.
Siku zote wafuasi hupenda sana kufata upepo na hawana msimamo.
wao ni kama bendera.
wafuasi ndio wala hasara huku wanaowaongoza wakitazama faida.
wafuasi hawana tofauti na wale wanyama wahamao kutoka mbuga ya Serenget na kuvuka mipaka na kuingia katika nchi nyingine.
"WAFUASI HAWAJIJENGEI MAZINGIRA YA KULA FAIDA,BALI HUWAJENGEA WENZAO MAZINGIRA YA KUNUFAIKA.
 
Jifunze nami kingereza kwa kiswahili kwa bei cheee, kwa mwezi. Masomo ni online na ni kwa miezi miwili 2,Tunasoma kwa video, pich, audio no kupitia WhatsApp peke,Nipigie sasa na utokwe na aibu ya kutojua kingereza fasah ingali wew ni msomi, many a bias hara ama mtendaji wa serikali,Piga 0753093869,baada ya kuhitimu tutakupatia ajira ukitaka, katika mataw yetu yotee... Mfano wa masomo yetu:

Somo la 1

(SECTION A; TENSES IN THE ACTIVE VOICE )

(A)Simple Tenses ,:

1. Simple Past Tense ( ‘li’)
- Wakati huu huongelea jambo lililofanyika na kukamilika mara moja wakati uliopita.
Mifano ; tulikuja ,walitembea, alicheza.
- Wakati huu huashiriwa na silabi ‘li’ ambayo hufanya tutambue kuwa tunaongelea jambo lililofanyika mara moja na likamalizika kufanyika katika wakati uliopita. Hii silabi ‘li’ ni lazima iunganishwe na kitendo moja kwa moja kabla ya kitendo. Mfano ; ‘Tuliimba’, tofauti na ‘Tulikuwa tunaimba’ ambapo ‘li’ imefuatiwa na kifungu ‘kuwa’ na sio kitendo. Katika maneno ‘tulikuwa tunaimba’, kitendo ‘imba’ kimetanguliwa na ‘na’ na sio ‘li’ kwa hivyo maneno hayo hayapo katika wakati huu wa Simple Past Tense, ‘li’.

Kanuni za kutumia Simple Past Tense ‘li’

a) Sentensi za taarifa/kutoa taarifa
Katika wakati huu, huwa tunapoelezea jambo tunatanguliza mtendaji wa jambo, (I/We/You/They/He/She/It) kisha tunafuatisha kitendo moja kwa moja kikiwa katika umbo la wakati uliopita.
Mfano ; - kitenda ‘enda’ ni ‘go’. Umbo lake la wakati uliopita, yaani ‘-lienda’ ni ‘went’. Tutatanguliza mtendaji wa jambo kisha tufuatishe neno ‘went’.

Sentensi za mifano;
- Juma alienda. ………. Juma went.
- Tulienda. ……… We went.
- Basi liliondoka. ……. The bus left.
- Nilicheza. ……. I played.
- Uliimba. ….. You sang.
- Walikimbia. ….. They ran.
- Maria alipika. ……. Maria cooked.
NB : Hatuweki kitu chochote katikati mwa mtendaji na kitendo.

b) Kuuliza maswali katika Simple Past Tense

- Maswali katika wakati huu huanzia na neon ‘did’. ‘Did’ ikitumika ni lazima kitendo kiwe katika umbo la kawaida kwa sababu ‘did’ ina ‘li’ ndani yake hivyo ‘li’ nyingine haihitajiki. Ina maana hiyo ‘did’ tayari imeshawakilisha wakati uliopita.
- ‘Did’ hufuatwa na nafasi inayouliziwa swali.
Mifano ya tafsiri :
- ‘Did Juma _______ ?’ …….. ‘Je, Juma ali______?’
- ‘Did they _______ ?’ ………. ‘Je, wao wali______ ?’

Sentesi za mifano :

1. Did Juma go?
Je, Juma ali enda ?

Jibu ; ( Hapana, hakuenda)…..( Kukanusha)
No, he didn’t go.
Au ; ( Ndio, alienda)…. Kukubali
Yes, he went.

2. Did she cook?
Je, alipika?

Jibu ; ( Hapana, hakupika)…..Kukanusha
No, she didn’t cook.
Au ; Ndio, alipika….. (Kukubali)
Yes, she cooked.

** katika kitabu kuna michoro ambayo inaonyesha tafsiri ya moja kwa moja ya kila kipengele cha sentensi kutoka kiswahili hadi kingereza ila hapa hatujaionyesha.

NB ; Tukiongeza neno ‘did’ katikati mwa jibu la kukubali, huwa ni kuweka msisitizo kama vile ambavyo kwa Kiswahili huwa tunaandisha sauti ili kuweka msisistizo ila sasa kwa Kingereza sauti haipandishwi ila msisitizo upo pale pale.

Mifano ; 1. Did Juma go ? …… Je, Juma alienda?
- Yes, he did go. ….. Ndio, alienda! (KWA MSISITIZO)

2. Did they cook? …….. Je, walipika?
- Yes, they did cook. …… Ndio, walipika! (KWA MSISITIZO)

NB ; Tunapokanusha sentensi kwa kutumia ‘did not’/ ‘didn’t’ , huwa hatutumii kitendo kikiwa katika umbo la wakati uliopita maana ile ‘did’ inakuwa imeshawakilisha wakati uliopita (‘li’ ambayo kinume chake ni ‘haku’) kwa hivyo hatuhitaji wakati uliopita kwa mara ya pili. Tukitumia umbo la wakati uliopita pia kwa kuuliza swali lililoanzia na ‘did’ pia tunakuwa tumeweka ‘li’ mbili katika sentensi, jambo ambalo sio sahihi.

Mifano ; 1. She didn’t went yesterday. ( Badala ya ‘She didn’t go yesterday.’)
Haku lienda jana. ( Badala ya ‘Hakuenda jana.’)

Au; 2. Did she went yesterday?
( Badala ya ‘Did she go yesterday?’)

- Je, yeye ali lienda jana?
( Badala ya ‘Je, yeye alienda jana?)
 
Back
Top Bottom