Millionaire Mindset
Member
- Apr 19, 2018
- 83
- 115
Hivi unajiskiaje unapoambiwa umefeli au umeshindwa? Au pale unapopata habari kwamba mtoto wako, ‘jembe lako unalolitegemea’ amefeli yaani amezungusha “O”?. Ninaanza kuhisi jinsi mapigo yako ya moyo yanavyoanza kwenda mbio bila sababu, bila kusahau kijasho chembamba kilichoanza kuchungulia kikihakikisha je, unachokisoma ni kweli au la! Usijali tuko kwenye somo tu, tunawekana sawa.
Tangu nianze kufuatilia ligi za mpira wa mguu, sijawahi kuona mchezaji kapewa kadi nyekundu na kutolewa kwenye mchezo, halafu akakata tamaa na kusema “Mimi sichezi tena mpira” sijawahi! Kama wewe mwenzangu umewahi kuona au kusikia hilo, basi tujulishe wana jamvi. Au je, timu ikishindwa michezo miwili au mitatu, inamaanisha timu hiyo haifai kwenye ligi? Haiwezi kuongoza ligi? Haiwezi kuchukua ubingwa?
Kwa nini moyo huo wa wachezaji wa soka na timu za soka, tusiuhamishie kwenye ligi ya MAISHA?. Kwenye ligi ya maisha kuna maluweluwe mengi sana ya kushangaza, mtu anaanzisha biashara lakini baada ya kupata hasara mara mbili tu, kashafunga, hataki tena kufanya wala kusikia habari za biashara hiyo. Wanafunzi nao, akisha feli mtihani mara moja tu, basi anaachana na habari za shule, hataki kusikia habari za shule, na anajiingiza kwenye makundi ya ajabu ajabu. Sijui ka-utaratibu haka tumekatoa wapi; na wala sijui ni nani aliyekufundisha kuwa kufeli kunamaanisha “STOP!”, “GIVE UP!”
Tafsiri halisi ya “kushindwa” au “kufeli” siyo hiyo; kwa sababu ingekuwa ni hiyo sidhani kama ungekuja kuwasikia akina Diamond, akina Mbwana, akina Moh, akina Bakhresa n.k. Kama ulikuwa hujui, fuatilia maisha yao ujue walifeli na kupigwa chini mara ngapi kabla hawajaufikia huo umaarufu na ukwasi walionao.
Maisha na yenyewe yako hivyo hivyo, umezaliwa toka tumboni mwa mama yako na kukutana moja kwa moja na changamoto za maisha. Umaskini, magonjwa, njaa, manyanyaso, dhiki na changamoto nyingine nyingi zilikuvaa. Kwa kifupi kwenye maisha “PEPA LINAANZA KWANZA, HALAFU KUJIFUNZA BAADAE”
Na ndiyo maana shule kama taasisi inapata taabu sana kuutoa ujinga kwa wanafunzi ili wakatatue matatizo na changamoto za maisha. Kwa sababu shuleni, kujifunza kunaanza kwanza halafu pepa linakuja baadae, kitu ambacho ni tofauti kabisa na formula ya maisha. Kwenye maisha ni lazima kwanza ufanye mtihani, ukifeli ndipo unapojifunza. La sivyo, watoto wachanga wanaozaliwa, wangekuwa wananyakuliwa kwanza, ili wakapate shule halafu baadae ndipo warudishwe kukutana na changamoto za maisha hapa duniani, lakini hilo halitokei.
Ninachojaribu kukushirikisha hapa ndugu yangu ni kwamba, maisha yenyewe yamekubali kitu kinachoitwa “Kufeli” na ndiyo maana maisha yamekiweka kitu hicho kama sehemu ya kanuni yake au mfumo wake. Sasa kama wewe unataka ufaulu au ufanikiwe pasipo kufeli au kushindwa, maana yake unapingana na kanuni ya maisha, yaani hutaki kuishi au?
Kuanzia sasa, amini kuwa kufeli ni sehemu ya kujifunza na kama hujawahi kufeli katika eneo fulani unalotafuta kubobea, basi maana yake ni kwamba hauna “Uthubutu”, hutaki kuchukua changamoto zilizo nje ya uwezo wako, yaani uko kwenye “Comfort zone”. Na kama kila siku uko pale pale unapopawezaga yaani “Comfort zone” maana yake haukui wala kuongezeka katika eneo hilo.
Ngoja basi tujifunze kwa mifano kwenye kipengele hiki. Unapoumwa maana yake ni kwamba seli zako zimefeli kuwasiliana na kushirikiana kwa usahihi, au kuna kitu kimeongezeka kwenye mwili wako ambacho kimefeli kuwa na mahusiano mazuri na seli zako za mwili. Na ndiyo maana mwili unakupatia taarifa kwa njia hiyo ya kuugua, na unaanza kutafuta namna ya kurekebisha tatizo hilo.
Unapogombana na rafiki yako tafsiri yake ni kwamba mmefeli kuhusiana vizuri, kuna vitu unavitaka lakini yeye havitaki au vice versa, kwa hiyo asili “Nature” itautumia ugomvi ili kutoa taarifa kuwa uhusiano wenu hauko vizuri, kwa hiyo mjirekebishe, wala hakuna habari za mkosi au kurogwa hapo!
Ukiilewa kanuni hii ya asili(kufeli/kushindwa), basi utagundua kuwa, kufeli au kushindwa katika eneo fulani ni njia rahisi ambayo Asili (Nature) huitumia kumtaarifu mhusika au kitu husika kuwa, kuna sehemu fulani kanuni za asili hazijafuatwa, basi kinachotakiwa ni kujirekebisha na kukifanya kitu hicho kwa kufuata kanuni hizo, kwa sababu karibu vitu vyote ulimwenguni vina kanuni na taratibu zake.
Serikali ina kanuni zake na taratibu, raia akizivunja wote tunajua kitakachotokea, Kampuni zina kanuni na taratibu zake, mfanyakazi akizivunja, wote tunajua kitakachotokea. Jamii zina kanuni na taratibu zake (zile tunazoziita miiko, mila na desturi) mwana jamii akizivunja, wote tunajua kitakachotokea. Kila kitu kina kanuni na taratibu zake, cha msingi ni kuvielewa vitu hivyo kwa kutafuta maarifa na siyo kukata tamaa au kuachana navyo.
Usifikiri kufeli kuna kutafsiri wewe kuwa mjinga, mpuuzi, mbumbumbu n.k hilo si kweli, bali kufeli kunatoa taarifa kwako kwamba, njia uliyoitumia kufanya kitu hicho ulichokifanya haikuwa sahihi, hivyo basi tafuta njia nyingine mbadala na sahihi ya kukifanya kitu hicho.
Sasa inashangaza sana, kama baada ya kufeli unaanza kumtafuta na kumlaumu huyo unayemwangalia kwenye kioo(taswira yako), badala ya kutumia muda huo kuyasaka maarifa kokote kule yaliko, ili uweze kukifanya kitu chako kwa ufanisi tena. “You are wasting a huge bunch of time, for no reason”
Kuanzia sasa, kitu kikikushinda au ukilisikia neno “Umefeli”, sitaki nikuone umetununia huku mtaani watu tusiokuwa na hatia bila sababu, bali nikuone umechangamka na kukusanya nguvu mpya, maarifa mapya na namna mpya ya kulitatua tatizo lako. Full stop!
Kuna jamaa aliwahi sema kuna makumbusho kubwa sana hapa ulimwenguni ambayo haionekani kwa macho. Kwenye makumbusho hayo, kuna biashara kubwa sana ambazo hazijawahi kufanyika, zote zilifia kwenye mawazo ya watu, kuna vipaji vikubwa sana, yaani hata hivyo tunavyoviona na kuvisifia vikasome. Lakini vipaji hivyo hatujawahi kuviona wala kuvisikia, vimefia akilini mwa watu na mioyoni mwao.
Kwenye makumbusho hayo kuna viongozi wakubwa sana wa serikali lakini hatujawahi kuwaona, wengi wamefia mioyoni mwa watu na akilini mwao. Kuna uvumbuzi mkubwa sana ambao pengine ungefanyika, Tanzania ingekuwa nchi ya dunia ya kwanza, lakini kuna kajamaa kamoja kameua, uvumbuzi huo akilini mwake na kamegoma kabisa kutushirikisha. Mungu anakuona!
Tangu nianze kufuatilia ligi za mpira wa mguu, sijawahi kuona mchezaji kapewa kadi nyekundu na kutolewa kwenye mchezo, halafu akakata tamaa na kusema “Mimi sichezi tena mpira” sijawahi! Kama wewe mwenzangu umewahi kuona au kusikia hilo, basi tujulishe wana jamvi. Au je, timu ikishindwa michezo miwili au mitatu, inamaanisha timu hiyo haifai kwenye ligi? Haiwezi kuongoza ligi? Haiwezi kuchukua ubingwa?
TUMEMEZESHWA TAFSIRI ISIYO SAWA YA “KUFELI”
Haya sasa ngoja ustaajabu ya Musa ndugu msomaji; huku mtaani tuna wachezaji wanaoshindwa mechi moja na kuachana kabisa na habari za mpira mpaka wanakufa, na tuna timu zinazoaga mashindano eti kisa zimeshindwa mechi mbili tu! Mfululizo “POOR SOULS!”. Inawezekana na huyu anayesoma makala hii sasa, naye ni mmoja wapo. Mungu anakuona!Kwa nini moyo huo wa wachezaji wa soka na timu za soka, tusiuhamishie kwenye ligi ya MAISHA?. Kwenye ligi ya maisha kuna maluweluwe mengi sana ya kushangaza, mtu anaanzisha biashara lakini baada ya kupata hasara mara mbili tu, kashafunga, hataki tena kufanya wala kusikia habari za biashara hiyo. Wanafunzi nao, akisha feli mtihani mara moja tu, basi anaachana na habari za shule, hataki kusikia habari za shule, na anajiingiza kwenye makundi ya ajabu ajabu. Sijui ka-utaratibu haka tumekatoa wapi; na wala sijui ni nani aliyekufundisha kuwa kufeli kunamaanisha “STOP!”, “GIVE UP!”
Tafsiri halisi ya “kushindwa” au “kufeli” siyo hiyo; kwa sababu ingekuwa ni hiyo sidhani kama ungekuja kuwasikia akina Diamond, akina Mbwana, akina Moh, akina Bakhresa n.k. Kama ulikuwa hujui, fuatilia maisha yao ujue walifeli na kupigwa chini mara ngapi kabla hawajaufikia huo umaarufu na ukwasi walionao.
MAISHA NA KUFELI
Umeamka asubuhi unawahi shule siku ya kwanza kabisa, na pindi unapoingia tu darasani, mwalimu wa somo anawapatia mtihani wakati hamjawahi hata kusoma au kufundishwa kitu chochote kile. Yaani hata kusoma “A” hujui ndugu msomaji, lakini ndiyo hivyo, mwalimu kasha kupatia pepa. Naomba unijibu hapo kinachotarajiwa ni nini? Kufeli au siyo? Naomba uniambie, kuna kitu kingine hapo kinachotarajiwa nje na kufeli?Maisha na yenyewe yako hivyo hivyo, umezaliwa toka tumboni mwa mama yako na kukutana moja kwa moja na changamoto za maisha. Umaskini, magonjwa, njaa, manyanyaso, dhiki na changamoto nyingine nyingi zilikuvaa. Kwa kifupi kwenye maisha “PEPA LINAANZA KWANZA, HALAFU KUJIFUNZA BAADAE”
Na ndiyo maana shule kama taasisi inapata taabu sana kuutoa ujinga kwa wanafunzi ili wakatatue matatizo na changamoto za maisha. Kwa sababu shuleni, kujifunza kunaanza kwanza halafu pepa linakuja baadae, kitu ambacho ni tofauti kabisa na formula ya maisha. Kwenye maisha ni lazima kwanza ufanye mtihani, ukifeli ndipo unapojifunza. La sivyo, watoto wachanga wanaozaliwa, wangekuwa wananyakuliwa kwanza, ili wakapate shule halafu baadae ndipo warudishwe kukutana na changamoto za maisha hapa duniani, lakini hilo halitokei.
Ninachojaribu kukushirikisha hapa ndugu yangu ni kwamba, maisha yenyewe yamekubali kitu kinachoitwa “Kufeli” na ndiyo maana maisha yamekiweka kitu hicho kama sehemu ya kanuni yake au mfumo wake. Sasa kama wewe unataka ufaulu au ufanikiwe pasipo kufeli au kushindwa, maana yake unapingana na kanuni ya maisha, yaani hutaki kuishi au?
MAFANIKIO NA KUFELI
Kama unataka kufanikiwa katika eneo lolote lile la maisha, basi achana uchuro na ubovu waliokujaza akina “FULANI” kuanzia nyumbani kwenu mpaka shuleni, kwamba kufeli ndiyo mwisho wako, utawasikia tu maneno yao; mara ooh! “ukifeli maana yake wewe ni mjinga”, “ukifeli shule basi na maisha yamekushinda” na utumbo mwingineo waliokujaza.Kuanzia sasa, amini kuwa kufeli ni sehemu ya kujifunza na kama hujawahi kufeli katika eneo fulani unalotafuta kubobea, basi maana yake ni kwamba hauna “Uthubutu”, hutaki kuchukua changamoto zilizo nje ya uwezo wako, yaani uko kwenye “Comfort zone”. Na kama kila siku uko pale pale unapopawezaga yaani “Comfort zone” maana yake haukui wala kuongezeka katika eneo hilo.
KANUNI YA ASILI (Natural Law)
Kila kitu kwenye asili, ili kizidi kustawi na kuendelea lazima kitengeneze mahusiano mazuri na asili yenyewe (Nature). Ukishindwa kujiandamanisha kwa usahihi na asili, lazima utakutana na matatizo na kufeli au kushindwa ni mojawapo ya matatizo hayo.Ngoja basi tujifunze kwa mifano kwenye kipengele hiki. Unapoumwa maana yake ni kwamba seli zako zimefeli kuwasiliana na kushirikiana kwa usahihi, au kuna kitu kimeongezeka kwenye mwili wako ambacho kimefeli kuwa na mahusiano mazuri na seli zako za mwili. Na ndiyo maana mwili unakupatia taarifa kwa njia hiyo ya kuugua, na unaanza kutafuta namna ya kurekebisha tatizo hilo.
Unapogombana na rafiki yako tafsiri yake ni kwamba mmefeli kuhusiana vizuri, kuna vitu unavitaka lakini yeye havitaki au vice versa, kwa hiyo asili “Nature” itautumia ugomvi ili kutoa taarifa kuwa uhusiano wenu hauko vizuri, kwa hiyo mjirekebishe, wala hakuna habari za mkosi au kurogwa hapo!
Ukiilewa kanuni hii ya asili(kufeli/kushindwa), basi utagundua kuwa, kufeli au kushindwa katika eneo fulani ni njia rahisi ambayo Asili (Nature) huitumia kumtaarifu mhusika au kitu husika kuwa, kuna sehemu fulani kanuni za asili hazijafuatwa, basi kinachotakiwa ni kujirekebisha na kukifanya kitu hicho kwa kufuata kanuni hizo, kwa sababu karibu vitu vyote ulimwenguni vina kanuni na taratibu zake.
Serikali ina kanuni zake na taratibu, raia akizivunja wote tunajua kitakachotokea, Kampuni zina kanuni na taratibu zake, mfanyakazi akizivunja, wote tunajua kitakachotokea. Jamii zina kanuni na taratibu zake (zile tunazoziita miiko, mila na desturi) mwana jamii akizivunja, wote tunajua kitakachotokea. Kila kitu kina kanuni na taratibu zake, cha msingi ni kuvielewa vitu hivyo kwa kutafuta maarifa na siyo kukata tamaa au kuachana navyo.
KUFELI NA MAARIFA
Kufeli au kushindwa kitu fulani au eneo fulani kwenye maisha yako ni taarifa siyo tafsiri.Usifikiri kufeli kuna kutafsiri wewe kuwa mjinga, mpuuzi, mbumbumbu n.k hilo si kweli, bali kufeli kunatoa taarifa kwako kwamba, njia uliyoitumia kufanya kitu hicho ulichokifanya haikuwa sahihi, hivyo basi tafuta njia nyingine mbadala na sahihi ya kukifanya kitu hicho.
Sasa inashangaza sana, kama baada ya kufeli unaanza kumtafuta na kumlaumu huyo unayemwangalia kwenye kioo(taswira yako), badala ya kutumia muda huo kuyasaka maarifa kokote kule yaliko, ili uweze kukifanya kitu chako kwa ufanisi tena. “You are wasting a huge bunch of time, for no reason”
Kuanzia sasa, kitu kikikushinda au ukilisikia neno “Umefeli”, sitaki nikuone umetununia huku mtaani watu tusiokuwa na hatia bila sababu, bali nikuone umechangamka na kukusanya nguvu mpya, maarifa mapya na namna mpya ya kulitatua tatizo lako. Full stop!
NDOTO NA VIPAJI VILIVYOZIKWA
Kufeli au kushindwa, isiwe ndiyo sababu ya kuachana au kuikatia tamaa ndoto yako au kipaji chako. Bali iwe ni chachu ya kutafuta maarifa mapya, ili kuyatumia kukifanya kitu chako hicho kwa upya na kwa uzuri zaidi.Kuna jamaa aliwahi sema kuna makumbusho kubwa sana hapa ulimwenguni ambayo haionekani kwa macho. Kwenye makumbusho hayo, kuna biashara kubwa sana ambazo hazijawahi kufanyika, zote zilifia kwenye mawazo ya watu, kuna vipaji vikubwa sana, yaani hata hivyo tunavyoviona na kuvisifia vikasome. Lakini vipaji hivyo hatujawahi kuviona wala kuvisikia, vimefia akilini mwa watu na mioyoni mwao.
Kwenye makumbusho hayo kuna viongozi wakubwa sana wa serikali lakini hatujawahi kuwaona, wengi wamefia mioyoni mwa watu na akilini mwao. Kuna uvumbuzi mkubwa sana ambao pengine ungefanyika, Tanzania ingekuwa nchi ya dunia ya kwanza, lakini kuna kajamaa kamoja kameua, uvumbuzi huo akilini mwake na kamegoma kabisa kutushirikisha. Mungu anakuona!
Hitimisho
- Tafsiri tuliyomezeshwa na watu wanaotuzunguka juu ya kufeli, siyo tafsiri sahihi
- Kufeli ni kanuni ya asili (Natural law), ambayo asili huitumia kurekebisha mambo mbali mbali
- Kufeli hakumtafsiri mtu ya kuwa ni mjinga, mbumbumbu n.k. wala kufeli hakutafsiri maisha, malengo au ndoto ya mtu kuwa ndiyo mwisho wake, bali kufeli ni taarifa ambayo asili(Nature) inampa mtu, kuwa atafute njia mbadala na sahihi ya kufanya kitu hicho anachokifanya.
- Kuna ndoto na vipaji vikubwa vimezikwa kwenye makumbusho isiyoonekana, usikubali kipaji chako au ndoto yako ikaishia huko.