Tafsiri sentensi hizi za 'tenses'

1. Wimbo ulikuwa unaimbwa. The song was being sung (Past continuous state of time)

2. Wimbo ulikuwa ukiimbwa. The song had had been sung (participle state, past continuous)
Tafsiri sentensi hizi za 'tenses' kwenda kiingereza ujishindie Kitabu chetu cha JIFUNZE KIINGEREZA KWA KISWAHILI. Ni mojawapo ya vitabu vilivyovunja rekodi ya mauzo ndani ya muda mfupi sokoni.
 

your apology well received mkuu
 
HILI NDO JIBU SAHIHI

1. the song has been singing
2. the song had been sung
 
HILI NDO JIBU SAHIHI

1. the song has been singing
2. the song had been sung
1. The song has been singing - Wimbo umekuwa u-na/ki-imba. Mkuu tangu lini nyimbo zikapata uwezo wa kuimba?

2. The song had been sung (hali timilifu) - Wimbo ume(sha)imbwa.

Zote ni tofauti na sentensi tunazopaswa kutafsiri. HAKUNA JIBU SAHIHI HAPO !!!
 

your apology well received mkuu
Usipokee apology pekee mkuu (utafikiri kweli kulikuwa na kitu nimekukosea) bali uzingatie pia na ushauri niliokupa hapo juu. Mijadala haipo kwa ajili ya kupata mshindi na mshindwa bali KUELIMISHANA. Ushauri huu utakusaidia sana!
 
Usipokee apology pekee mkuu (utafikiri kweli kulikuwa na kitu nimekukosea) bali uzingatie pia na ushauri niliokupa hapo juu. Mijadala haipo kwa ajili ya kupata mshindi na mshindwa bali KUELIMISHANA. Ushauri huu utakusaidia sana!

sawa boss
 
The song was singing!!!..
The song had sang!!..
The song was singing - Wimbo ulikuwa ukiimba, Wimbo ulikuwa unaimba.

The song had sang - Wimbo ulikuwa umeimba

Sentensi hizi ni tofauti na za mleta mada mbona?
 
FUATA SENTESI INAVYOTAKA USIHOJI MASWALI NDIYO NYIE MNAFELI MTIHANI UNAULIZWA UJIBU NAWE UNAHOJI
Hata sielewi kwa nini unatoka povu. Sijajua kosa langu ni nini mkuu. Sentensi tunazopaswa kutafsiri ni hizi:

1. Wimbo ulikuwa unaimbwa.
2. Wimbo ulikuwa ukiimbwa.

Tafsiri yako ya "The song has been singing" ni ya sentensi ipi kati ya hizo juu?

Na tunapotafsiri kitu ni lazima tuzingatie pia misingi ya kisemantiki na kuhakikisha kuwa sentensi angalau inaleta maana. Sasa mkuu "The song has been singing - Wimbo umekuwa ukiimba" ina maana yo yote kisemantiki? Nyimbo huwa zinaimba?
 
The song was singing - Wimbo ulikuwa ukiimba, Wimbo ulikuwa unaimba.

The song had sang - Wimbo ulikuwa umeimba

Sentensi hizi ni tofauti na za mleta mada mbona?
English language have got no one to one correspondence between sounds(phonology),semantic,morphology as well as syntax with with Kiswahili,the fact is that Kiswahili is not amongst of Endo European languages like,German, France and Latin, where English emanated!!!...
 
Mkuu, maelezo mengi ya nini? Swali ni rahisi tu. Ni kutafsiri hizi sentensi mbili kwenda Kiingereza.

1. Wimbo ulikuwa unaimbwa.
2. Wimbo ulikuwa ukiimbwa.

Sasa maelezo yako haya ya Historical Linguistics yanasaidia nini? Ungetoa maelezo ya Translation Theory pengine yangesaidia kidogo.
 
Hahahahaha saw Mkuu!!..
 
1. Wimbo ulikuwa unaimbwa.
2. Wimbo ulikuwa ukiimbwa.

Nisipokosei sentensi ya pili isiwe na nukta maana inataka kuendelea.
Sentensi ya kwanza: Nilifika mahali. Wimbo ulikuwa unaimbwa.

Sentensi ya pili: Nilifika mahali. Wimbo ulikuwa ukiimbwa ... wakati nyumba iliporomoka.

Kwa Kiingereza haiwezekani kuitofautisha hali hizi mbili kwa kifupi jisi ilivyo kwa Kiswahili.
Sawa?
 
Ina maana unataka kusema kuwa SHIMBA YA BUYENZE yuko sahihi kama alivyoainisha katika comment # 3? [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Ina maana unataka kusema kuwa SHIMBA YA BUYENZE yuko sahihi kama alivyoainisha katika comment # 3? [emoji23][emoji23][emoji23]

Ndiyo, we shujaa wa sarufi! Niliongeza tu ya kwamba nisingetegemea kuona maneno "wimbo ulikuwa ukiimbwa" peke yao, lazima kuna habari zinazofuata.
Sawa?
 
 
umejieleza vzr lkn napingana na ww kwa sentensi ya pili...hii sentensi kwa maoni yangu iko ktk past perfect progressive aspect...the action was going on and it was interupted by other action in the past.so itakuwa the song had been sung...kimsingi sentensi hii haijakamilika hivyo tunaweza kuikamilisha kwa kusema...the song had been sung before i arrived..yaan wimbo ulikuwa ukiimbwa kabla sijawasili
 

Asante mkuu. Maelezo yako yana tija na inawezekana ukawa sahihi. Lugha ya watu hii ati!

Lakini ungeniambia nitafsiri yako ya "The song had been sung before I arrived" kwa Kiswahili ningesema "Wimbo ulikuwa umeshaimbwa kabla sijawasili" (Wakati uliopita hali timilifu)

Na "Wimbo ulikuwa ukiimbwa kabla sijawasili" kwenda Kiingereza ningesema "The song was being sung before I arrived" (Wakati uliopita hali endelevu)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…