Tafsiri ya historia ya tafsiri ya Biblia kwa lugha ya Kiswahili

Tafsiri ya historia ya tafsiri ya Biblia kwa lugha ya Kiswahili

Idd Ninga

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2012
Posts
5,497
Reaction score
4,775
Wengi wamekuwa wakisoma Biblia ya Kiswahili bila ya kufahamu hasa ni nani alioandika Biblia kwa lugha ya Kiswahili kutoka katika moja ya lugha zile tatu za mwanzo mwanzo ambao ndizo zilizotumika kama maandishi ya Biblia.

Hapo zamani Biblia ilikuwa imeandikwa katika lugha tatu ambazo ni lugha ya Kiebrania, Kigiriki na Kiaramu, lakini kadri miaka ilivyozidi kwenda na wafundishaji wa Biblia kuzidi kusambaa sehemu mbalimbali za ulimwengu zenye wazungumzaji wa lugha tofauti tofauti, mawazo ya kuandika Biblia katika lugha nyingine yalizidi kuzaliwa kulingana na mahitaji ya watu katika eneo husika.

Pamoja na kwamba Kiswahili ni lugha ya watu wa Afrika lakini wapo baadhi ambao siyo waafrika lakini wameweza kuonyesha uwezo wao mkubwa katika kufanya mambo makubwa katika lugha ya Kiswahili ambayo yanatumika hadi leo.

Tukitazama hata mtu wa kwanza kufanya tafsiri ya kwanza ya kitabu kitakatifu cha Qurani,alikuwa anaitwa Shekhe Mubaarak Ahmadi ambae alifanya tafsiri nzima ya Quran kwa lugha ya Kiswahili ikiwa ni tafsiri ya kwanza kabisa katika lugha ya Kiswahili.

Tafsiri ya kwanza ya Biblia ya Kiswahili ilianza kufanyika mnamo mwaka 1844 mwezi Juni na Dr Ludwig Krapf alieanza kuingia katika bara la Afrika mwaka 1837 akitokea katika nchi ya Uingereza na kuingia Afrika chini ya shirika la wamisionary lililojulikana kama Church Missionary Society, huku safari yake ya kwanza ikianzia nchini Ethiopia.

Akiwa nchini Ethiopia Dr Ludwig alifanya kazi kwa kipindi cha mwaka mmoja tu na baadae kuhamishiwa nchini Kenya,ambako alianza kufanya kazi na missionary yake katika mji wa Mombasa ambako ndiko alipokutana na waswahili na yeye ukjifunza Kiswahili,na baada ya kujifunza Kiswahili na kukifanyia utafiti aligundua kIswahili ni Lugha rahisi ndipo alioamua kuandika tafsiri ya Biblia katika lugha ya Kiswahili.

Dr Ludwig alifanya Tafsiri ya kwanza akisaidiwa na Aly Bin Mohedin wa Mombasa, katika tafsiri hizo za mwanzo, Ludwig alitafsi Biblia katika lahaja ya Kimvita,akitafsiri agano jipya katika Injili ya Luka na Yohana.

Miaka miwili baadae mke wake na watoto wake waliugua sana na mauti yaliwakuta wakiwa nchini Kenya na Kuzikwa Mombasa.

Mwaka 1846,Church Misionary Society ilimleta mtu mwingine, John Rebman ili afanye kazi na Ludwig ambao walifanya kazi pamoja kwa muda mrefu hadi mwaka 1861.

Rebman aliifanyia marekebisho tafsiri ya Ludwig katika injili ya Luka katika mwaka 1876, lakini pamoja na juhudi zote alizofanya Ludwig lakini tafsiri yake haikuchapishwa.

Mwaka 1883, Edward Steere alichukua maandishi yake Krapf ili ayalinganishe na tafsiri yake aloifanya katika lahaya ya Kiunguja.

Idd Ninga.
iddyallyninga@gmail.com
 
Back
Top Bottom