Kwa kweli google translate ni msaada kiasi lakini haiwezi kutafsiri. Kuna lugha kadhaa ambako matokeo ni afadhali kwa mfano kutoka Kiingereza kwenda Kifaransa, kijerumani au kihispania. Pale nimeona matokeo ya kitu kama 95 % sahihi - ambayo inaleta lugha baya hata kama inaeleweka kimsingi.
Kimsingi mashine inachukua tafsiri neno kwa neno. Kwa lugha ndogo kama Kiswahili badi hawakuandaa bado nafasi nyingi kwa kila neno; tena wanahitaji mifano na sentensi nyingi sana za kulinganisha. Katika mfano wako inaonekana ya kwamba "at" imechukuliwa kama tangazo ya saa (at 5 o'clock) kwa hiyo wameingiza "saa yake" badala ya "kwake".
Kwa lugha inayotumia misemo na nahau yaani lugha ya picha ni tena hatua nyingine kubwa.
Kwa Kiswahili naona: google inaweza kusaidia wakati mwingine - mara nyingi haisaidii!