WAPEKEE_
Member
- May 23, 2024
- 21
- 28
SISU - Ni neno la asili ya Ki-finland, lisilo na tafsiri ya moja kwa moja, lakini lenye dhima ya kuonesha ujasiri na maamuzi magumu yasiyofikirika.
Sifa hii ya SISU hujidhihirisha wazi pale ambapo matumaini yote hupotea.
Vita ya pili ya dunia ilikuwa inaelekea kumalizika na Ujerumani kinara wa vita , ilikuwa dhahiri kwamba wamepoteza vita kilichobaki ilikuwa ni kusalimu amri.
Mbaya zaidi , mshirika wao wa karibu , Finland, alikuwa amewasiliti dakika za mwisho wakiwa wamemsaidia kupambana na URUSI, baada ya kuamuliwa kuyaondoa majeshi ya Nazi kwenye ardhi yake kama masharti ya mkataba wa amani na umoja wa sovieti, URUSI (USSR).
Sasa kipindi hiki Ujerumani chini ya Hitler na majeshi ya Nazi , yalikuwa yanafyeka kila mji, kijiji, na njia zote za FINLAND , wakati wa kurejea nyumbani , na hapa ndipo , moja ya msafara wa kijeshi unakutana na mzee mmoja wa kifinland mchimba dhahabu, anaenda zake kujitafutia tumaini lake la mwisho kwasababu , alikuwa amepoteza kilakitu ikiwemo familia yote kwasababu ya vita.
Anakutana na moja ya kikosi njiani chenye roho mbaya, kinamzuia na kutaka kuchukua dhahabu zake, na anakifyeka chote, mkuu wa kikosi anagundua hilo na hapo rasmi wanaamua kumsaka ili kummaliza kabisa,
Farasi wa mzee anakanyaga bomu na kupasuka vipande , lakini mzee hakufa, anajiwasha moto akiwa ameloa petroli , mzee hakufa, wanamkamata na kumyonga juu ya nguzo ndefu na mzee anajiokoa bilakufa pamoja na wanajeshi kujiridhisha kabisa kuwa amekufa. Mzee anazama chini ya maji kwa dakika nyingi na hakufa.
Akiwa amemfyeka adui mkuu juu ya ndege ya kijeshi, ile ndege inapata bonge la ajali na kuanguka ardhini na mzee anapona.
Matukio ya mzee huyu kujiokoa katikati ya kifo yanatisha balaa, na kumbe mzee alikuwa Komando wa Kifinland aliyewafyeka Warusi kiasi warusi wenye roho mbaya walikuwa hawataki kabisa kumsikia Komando huyo na kumbatiza jina IMMORTAL ( YAANI ASIYEKUFA, SI BINADAMU WA KAWAIDA)
Mzee anafanikiwa kufika kwenye benki ya Finland na kuuza dhahabu zake zote alizochimba na kuzilinda kwa damu na machozi.
MOVIE : Inaitwa SISU , hutajutia kuitazama.
SOMO : Kuna wakati kwenye maisha, Kufa ni kusalimu amri ndoto zako zifike mwisho, ila kama ukiamua kugoma kufa kwa kukata Tamaa, utajikuta unakuwa sio kiumbe wa kawaida kwa namna utakavyo pona katikakati ya bonde la kifo.
“USIKUBALI KUFA KABLA HUJATIMIZA NDOTO ZAKO, WEWE NI IMMORTAL, KOMANDO KWENYE UWANJA WA VITA” : WAPEKEE_ @mrchambuzi .