Tafsiri ya Mtaala: STAR TV

ngoshwe

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2009
Posts
4,131
Reaction score
937
Leo Tuongee Asubuhi Star TV mada ni mustakabali wa Elimu. Uchambuzi unafanyika kuhusu maendeleo ya Elimu, mwalikwa (Mwl. Chacha) anaonekana kiasi kupingana na makala ya Bw. Kitila Mkumbo ya hivi karibuni ambayo inakubaliana kuwa Tanzania ina mtaala. Mfafanuzi anadai kuwa hatuna "planned Curricula" lakini tuna "muhtasari" mbalimbali ya elimu ambayo inatafsiriwa kama mtaala. Anadai hata mtaala alioeleza Waziri wa Elimu upo wa mwaka 2005, unatofautiana na mmoja wa mitasari (wa Elinu ya Uraia wa mwaka 1993) ambao uliandaliwa na Taasisi ya Ukuzaji wa Mitaala Tanzania lakini Huu mtaala unaodaiwa upo ulitolewa na Taasisi ya Elimu na kuthibitishwa na Wizara ya Elimu na Utamaduni na sio Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ambayo imejumuisha elimu mbalimbali ikiwemo Mafunzo ya Ufundi.
Mwalimu Chacha ana hoji "je, kama Taasisi ya Ukuzaji wa Mitaala ndio ilihusika kuandaa mitaala siku za nyuma,iweje sasa Taasisi ya Elimu ionekane inatoa mihtasari!?. Je hiyo Taasisi ya Ukuzaji Mitaala Imekufa!?
Tatizo lipo kwa Msimamizi wa Mada mtangazaji wa Star TV "Ivona Kamuntu" ambae inaonekana nae upeo wake kwenye kile anachojadili upo chini sana na staili yake ya kuuliza maswali na kutoa maelezo sio ya kiuandishi makini . Hii inapelekea kupoteza uvuto wa kipindi.
 
Yahya Mohammed kwani hayupo? Au yule Dotto asimamiae Tuongee Jumapili ndio wanaweza kudadavua mambo shauri ya upeo wa elimu zao pia!
 
Yahya Mohammed kwani hayupo? Au yule Dotto asimamiae Tuongee Jumapili ndio wanaweza kudadavua mambo shauri ya upeo wa elimu zao pia!

Sifahamu. Hivi vyombo vyetu vya habari havina ubunifu, mambo yanayohitaji taaluma wao wanapachika mtu yeyote tu ambae hata haelewi kile kinachozungumziwa.
 
Nimemsikiliza huyu mtangazaji kweli ameshindwa kuhimili watu aliowaita inaoneka kama hajimudu. Ila sishangai inawezekana katumwa na magamba atetee hoja pia ujumbe alioundika kwenye facebook haueleweke kabisa. Ndo hivyo atajifunza tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…