Tafsiri ya sentensi hizi za Kiingereza

Lolipop

JF-Expert Member
Joined
Oct 30, 2013
Posts
349
Reaction score
81
Salamu kwenu wadau!
Leo nilikuwepo sehemu fulani nikakuta watu(wanafunzi) wanafanya mashindano ya kiingereza. Sasa kuna sehemu ya kutafsiri kwa kiingereza hizi sentensi za kiswahili. Mimi mwenyewe yamenipiga chenga nikaona nilete kwenu great thinkers mnisaidie. Sentensi zenyewe hizi hapa
1. Baba mimi ni mtoto wako wa ngapi?
2. Alitambaa kwa magoti mpaka yakachubuka
3. Huyu ndiye mwanamama aliyenizaa
4. Ingekuwaje kama mimi ningezaliwa mwanamke?

Ninaomba tafsiri yake au maana inayoendana kwa lugha ya kingereza sentensi hizo.
Nawasilisha!! Karibuni!
 

Sasa aliyekuambia kutafsiri ndo kuwa great thinker nani

ebu fanya kuingia tu google transilation.. Tehhh
 
Kujua kubadili hayo maneno kuwa kiingereza ndo mtafakuri mkubwa??tanzania hii kuna watu wakiongea jambo la kipumbavu kwa kiingereza wanaonekana wa maana kwel
 
kiswahili kina maneno machache yenye maana finyu tofauti na kiingereza kwahiyo sio kila neno la kiingereza lina neno lake la kiswahili...ntajaribu 3,4
3.this is my birthmother au this is my mother
4.what if i was a woman aor what if i was born a woman
 
2. he walked on his kneel thus he got scrached
 
Hii nchi kazi ipo,unapofanya ukalimani cha muhimu ni kujitahidi usipoteze maana ya ujumbe uliokusudiwa na si kila neno la kiswahili liwe na neno lake upande wa Kiingereza.Mwenye masikio na asikie.
 

Ndugu jinsi ulivyotafsiri hizo sentensi zako inaonesha DHAHIRI kwamba kama ilivyo kwa watanzania wengi: hakuna lugha kati ya hizi mbili tuijuayo.

Kama ungekuwa huo ni mtihani wa lugha swali juu ya tafsiri basi hapo ungekuwa umepata "Alpha Blonde" yaani BONGE LA SIFURI/ZERO.

Kama ulienda shule SIYO hizi za kisiasa za BRN ungetumia maarifa kwa kukumbuka "Conditional Sentences" ulizojifunza kidato cha pili na tatu. Na pia ungekumbuka "Wish Sentence".

Tanbihi: Hakuna lugha iliyobora au toshelevu kuliko nyingine. Kama ingekuwa vinginevyo, lugha ya kiingereza isingekuwa na msamiati wa kisayansi, kisheria unaojitosheleza. Kigiriki,Kilatini na Kifaransa ndizo lugha zilizotoa msamiati wa kisayansi,kisheria kukisaidia kiingereza kiwezekueleza dhana za kisayansi na kisheria.

Lugha hizo pia zina upungufu wa msamiati katika nyanja nyingi tu. Kwa maana nyingine,lugha zote si kamilifu ila zinategemeana.Kwa mfano, istilahi hizi za kitabibu katika lugha ya kiingereza zimetokana na lugha za Afrika "Dengue", " Chemi-stry" na mengine mengi.
 
Hii nchi kazi ipo,unapofanya ukalimani cha muhimu ni kujitahidi usipoteze maana ya ujumbe uliokusudiwa na si kila neno la kiswahili liwe na neno lake upande wa Kiingereza.Mwenye masikio na asikie.

Tatizo la sisi watanzania ni pale kila mtu anapogeuka mtaalamu wa kila jambo. Mtu akiweza kutamka "was, were..." basi anajigeuza mtaalam wa tafsiri/ mkalimani na mwalimu wa lugha ya kiingereza.

Kila mtu tabibu, mtu ukimwambia naumwa ataanza kukuambia dawa za kununua na kuzitumia. Kila mwenye elimu ya kidato cha sita,chuo anajigeuza mwalimu wa shule za sekondari,chekechea nk.

Kwa hiyo, ni wazi kuwa tuna matatizo ya mfumo wa elimu hapa nchini.Elimu imevurugwa kupindukia, haya tuyaonayo ni kidogo na ni machache tu.
 
Thibitisha madai yako!
 
1. Father, what number baby born on your children list am I?
2. S/he crawled on her/his knees until they get bruised.
3. This is the woman who bore me.
4. What would happen if I were born a woman?

Hopefully kuna mawasiliano.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…