Ibara number 41 ya katiba ya JMT inazungumzia uchaguzi wa raisi. Ninaomba wanasheria mtusaidie kupata ufafanuzi kifungu cha saba.
(6) Mgombea yeyote wa kiti cha Rais atatangazwa kuwaamechaguliwa kuwa Rais iwapo tu amepata kura nyingi zaidikuliko mgombea mwingine yeyote.
(7) Iwapo mgombea ametangazwa na Tume ya Uchaguzikwamba amechaguliwa kuwa Rais kwa mujibu wa ibara hii, basihakuna Mahakama yoyote itakayokuwa na mamlaka yakuchunguza kuchaguliwa kwake.
Ufafanuzi ninaoumba ni kama tangazo la tume juu ya raisi litakuwa na kinga ya kutokuchunguzwa na mahakama yoyote hata pale ambapo maamuzi ya tangazo hilo hayajazingatia matakwa ya Ibara hii ya 41 mfano kama kifungu cha 6 ama chochote kikiwa kimekiukwa.
Kifungu cha saba kinasema wazi "Iwapo mgombea ametangazwa na tume ya uchaguzi kwamba amechaguliwa kuwa raisi kwa mujibu wa ibara hii (ya 41)". Vipi kama kilichotangazwa hakiko kwa mujibu wa ibara hii? Bado tangazo hilo ni legally binding?
Swali lingine, ni chombo gani kinatakiwa kuhakiki compliace ya tume ( iliyopewa nguvu hiyo kwenye) ili kujiridhisha kwamba inachokitangaza kimefanyika inline with stipulations za ibara hii ya 41?
Vipi ikitokea msemaji wa tume, on insanity, corruption, Rebellion, conspiracy, au threat grounds akamtangaza mtu kuwa raisi bila taratibu na mahitaji ya ibara hii ya 41 kufuatwa, bado itakuwa ni lawful, binding and enforceable announcement?
NAOMBA TUJADILIANE NA KUELEIMISHANA KWA HOJA. Na ni vizuri tukiwa tunarejea mfano wa kifungu cha sita hapo juu..