Tanzania Nchi Yetu Sote
JF-Expert Member
- Mar 12, 2017
- 505
- 872
Unaweza usiwe na nguvu sana lakini ukiwa vizuri kwenye uwezo wa kustahimili mambo magumu unayopitia, unaweza kufanikiwa.
Kila binadamu anapitia changamoto mbalimbali kulingana na mazingira yake, umri wake, kipato chake na hata kazi yake anayoifanya ila tunatofautiana namna ya kustahimili changamoto hizo.
Waliofanikiwa ni watu ambao wameweza kubadili changamoto zilizopo katika jamii na kuzifanya kuwa fursa. Yes, namaanisha ability to convert problems into solutions
Binadamu anaonekana shujaa pale tu ambapo ametatua tatizo fulani na kulitatua na siyo kulikimbia.
Acha kulalamika. Fanya kitu. Uwe na pa kusemea. Kila siku unashinda unalalamikia familia yako na Serikali yako wewe umefanya nini?
Tafuta eneo moja ambalo utalisimamia na kulifanya identity yako. Mtu ni kazi. Kama huna kazi (Simaanishi kazi ya kukaa ofisini na kuvaa tai tu) tutashindwa kukupa heshima yako. Hatuheshimu weupe wako wala huo mwanya wako na six packs zako, tunaangalia nafasi yako katika jamii. Wewe ni nani, huduma gani unaitoa kwa jamii, kitu gani ambacho wewe usipokuwepo hakifanyiki. Wewe ni nini?
Ukisema jina Cristiano Ronaldo mentally kila mtu anaona yule mcheza soka maarufu. Yaani hakuna Cristiano Ronaldo bila football.
Uza hata urembo barabarani tukujue kama muuza urembo, fungua basi hata mgahawa tuje kula kwako tukujue kama mama lishe, fuga hata kuku basi ili uwe unatuuzia mayai na nyama, lima mpunga, karanga, korosho na bustani basi ili tuwe tunanunua kwako. Fungua hata saluni basi tuje kushave na kupamba nywele zetu hapo.
Siyo lazima uwe Rais eti ndio uwe na msaada kwa jamii, unaweza kuwa na msaada hata kama wewe ni muuza karanga. Kikubwa heshimu kazi, jenga nidhamu ya pesa (usidharau pesa ndogondogo) na weka malengo. Yaani unafanya kazi hii ili nini? Kama unalima mbogamboga ili ununue bajaji au ujenge hakika utafanikiwa lakini kama unalima tu ulimradi umelima basi utaishia kulima miaka nenda rudi mpaka unazeeka hutakuja utoke kimaisha.
Kila kitu ni malengo Sheikh. Usifanyefanye tu bila future utaishia kuwa mtumwa wa watu. Yaani kila siku wewe ni kutembeza kahawa mtaani ukipata pesa inaishia baa kesho tena unaanza upya.
Ukiwa na malengo ni rahisi kuvumilia magumu ya leo ili kuyapata mazuri ya kesho.
WORK SMART