Tafuta hela, kutafuta taarifa za watu ni umaskini

Tafuta hela, kutafuta taarifa za watu ni umaskini

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
76,107
Reaction score
160,001
Watu wako busy sana na kufuatilia maisha na taarifa za watu. Muda ni rasilimali adhimu tena adimu. Muda ukikuacha huwezi kuupata tena.

Kwanini unahangaika na maisha ya watu? Jali muda wako na uuheshimu. Muda unaourumia kwa umbea, majungu, na uzandiki , utumie kuzalisha mali na kuboresha maisha yako.
 
Nadhani lengo la kutafuta taarifa lizingatiwe. Taarifa ni mali/pesa.
 
Kuna watu wanaitwa "chawa" hawa umbeya na kufatilia vya watu ndio kunawapa kula...sijui tuwafikiriaje
 
Kukosa hizo hizo hela/shughuli ndio hupelekea watu kutaka kujua ya watu.

Ili mtu ajiridhishe kukosa kwake anatafuta habari za mwingine mwenye nacho zaidi yake na akitie dosari ili yeye asienacho ajione bora.

Mfano utakuta mtu anajifanya kutaka kujua kwanini fulani ana hela nyingi halafu anajipa jibu kuwa ni freemason kujipa hitimisho kuwa bora ya yeye maskini lakini 'hajauza roho yake'.
Ila mtu huyo huyo akipata fursa hata ya uongo ya kuwa freemason ndio wa kwanza kwenda.
 
Back
Top Bottom