Watu wako busy sana na kufuatilia maisha na taarifa za watu. Muda ni rasilimali adhimu tena adimu. Muda ukikuacha huwezi kuupata tena.
Kwanini unahangaika na maisha ya watu? Jali muda wako na uuheshimu. Muda unaourumia kwa umbea, majungu, na uzandiki , utumie kuzalisha mali na kuboresha maisha yako.
Source:#3 Aisee mnajua hizi stori pombeni huku mvua inanyesha huwa zinanoga sana yaani unashikwa masikio kizembe ila pia yasemwayo yapo me tatizo langu nijue wamiliki wa haya mabasi miamba route za Mbinga - Songea - Tunduru - Masasi - Lindi - Kilwa - Dar pia Makambako to Moro - Dar na kweli...
Kukosa hizo hizo hela/shughuli ndio hupelekea watu kutaka kujua ya watu.
Ili mtu ajiridhishe kukosa kwake anatafuta habari za mwingine mwenye nacho zaidi yake na akitie dosari ili yeye asienacho ajione bora.
Mfano utakuta mtu anajifanya kutaka kujua kwanini fulani ana hela nyingi halafu anajipa jibu kuwa ni freemason kujipa hitimisho kuwa bora ya yeye maskini lakini 'hajauza roho yake'.
Ila mtu huyo huyo akipata fursa hata ya uongo ya kuwa freemason ndio wa kwanza kwenda.