Kweli mawakala wa CHADEMA wametuangusha sana. Mimi nilipiga kura kituo cha Kentony 'A" hapo maeneo ya Africa Sana- Mwenge. Nilifika kituoni kama dakika mbili kabla ya kituo kufungwa- So, nilikuwa wa mwisho kabisa.
Wakati naingia kituoni, nilikuta mzozo mkubwa kati ya jamaa mmoja na askari polisi wawili, mgambo na wasimamizi wa kituo. Kisa ? Kumbe jamaa alikuwa wakala wa CHADEMA lakini alifika kituoni saa 9.45 mchana.
Kwa hiyo walimkatalia kushiriki kuhesabu kura....... Haya yatakuwa yametokea katika vituo vingapi ?????????