Jamani ndugu zangu wa Dodoma Mjini hasa wale mnaoishi maeneo ya Uzunguni Kilimani, nimepata lalamiko toka kwa rafiki yangu mmoja ananiambia hapo uzunguni kuna jamaa TAPELI MITAA HIYO kuweni makini naye, jamaa yangu anadai katapeliwa na huyo ndugu pesa yake.
Inasemekana huyo tapeli ni mgeni hayo maeneo na anadai anakaa nyumba mojawapo za waheshimiwa hapo ila haonyeshi ni nyumba ipi anakaa, jamaa ni nyeusi ana pua ndefu ndefu. Jamaa yangu ametapeliwa wiki ya tarehe 7, Alhamisi October 2021 maeneo ya uzunguni. Huyo jamaa anajifanya ana shughuli nyingi kiasi kwamba akija kwenye biashara yako huagiza bidhaa na anajifanya kasahau pesa nyumbani ukimpatia bidhaa huondoka akiahidi analeta pesa mapema, ukimpa humuoni tena kurudi na ukimpigia simu huwa anasema anakuletea ila huwa harudi kabisa anapotea mtaani.
Namba anazotoa kuwasiliana naye ni hizi
Mitaa mingine ya Dodoma kuweni makini na huyu jamaa, nimeahidiwa akionekana jamaa atampiga picha ili nije niwawekee picha yake humu ili mumtambue kwa sura yake huyu muhuni. Samahani kwa niliowakwaza kwa namna nilivyoiwasilisha hapa