Tetesi: TAHADHARI: App Zinazoweza Kuiba Taarifa za Benki, Email na Password Zako

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2016
Posts
20,743
Reaction score
25,564

UKIANGALIA katika simu yako ni dhahiri Application nyingi ulizopakua ni za bure. Wote tunapenda App za bure.

Mara nyingi App za bure zina gharama ya faragha (privacy) wakati wa kuziingiza katika kifaa chako.

Wengi wetu tumekuwa hatusomi vigezo wakati tunapoingiza App hizo ndani ya simu zetu, huwa tunabonyeza tu ‘agree to continue’ bila kusoma.

Lazima usome kuwatambua waliotengeneza na ujue ni vitu gani unawaachia mikononi mwao kama vile namba za simu, meseji zako, maeneo (locations) na vitu vingine kibao.

Utafiti wa hivi karibuni uliofanywa na wataalam waliobobea wa kituo cha ESET umebaini uwepo wa Application 29 zilizopo Google Play Store ambazo ni VIRUS aina ya TROJAN

Virusi hao ambao hutumia majina tofauti-tofauti wana uwezo wa kuingilia application zingine zilizopo katika simu yako na kutuma taarifa zote kwa hackers (wadukuzi).

App hizo ambazo zina virus ndani yake, pia zina uwezo wa kutengeneza Fake Logins Page ( Phishing) ambapo ukijichanganya tu, basi taarifa zako za siri kama bank details, email, password (nywila au neno la siri) zako za mitandao ya kijamii huchukuliwa na kutumwa kwa wadukuzi.

 
Shukrani kwa somo....Kwa huku Tanzania wadau bado wamelala....
 
Tumejipanga wasiombe poo kwa kuibiwa wao. Maana benki ni negative balance hadi benki itaka kuuza nyumba wao wa hack tu kutupunguzia pressure
 
 
Ndio maana sisi ambao hatujiamini lazima tuwe na smartphone kwaajili ya maswala ya michepuko, internet&camera alafu tunakuwa na kasimu kadogo ka kuvunjia chawa kwaajili ya mawasiliano ya muhimu +miamala ya kifedha.
 
Mimi labda ziwepo app za kuniongezea ela benki, lakini za kuniibia sina cha kuibiwa bank, account iko nehi.
 
Tutajie app hizo
 
wazee wa cleaners na boosters lazima waliwe hapo. Mtu simu ina ram 8GB, ram <1GB hapo bado processor ndogo halafu anataka iwe na great performance
 
Haya ma app ya kiboya siwekagi mimi sijui cleaner mara booster.

Kama simu yako uwezo mdogo ni mdogo tu. Solution usijaze app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…