SoC01 Tahadhari: Biashara za mtandaoni ni chanzo cha umaskini

Stories of Change - 2021 Competition

my nation

Member
Joined
Jul 15, 2021
Posts
71
Reaction score
96
Mtoa mada ##JURUDYIZA##

Wapendwa hakuna jipya chini ya jua asilimia kubwa ni ubatili mtupu.

Kwa sasa watu wengi wanajikita kutafuta utajiri wa haraka bila kujua harakaharaka haina baraka Na ujue tu kwamba Sayansi na teknolojia kwetu Afrika bado inanufaisha wachache tena nao wananufaika kwa kuhadaa wengi wasiojua au wale wanaokurupuka kufanya maamuzi.

Biashara za mtandao kwa sasa zimewaliza wengi wanaotamani kufanikiwa zaidi kwa kutumia njia za mkato na biashara hizo ni hadaa sana na wao wanao zihubiri asilimia kubwa hawajanufaika bali nao ni walaibu tu wakiamini ipo siku watatoka tu mwishowe huwa hawasimulii tena hasara wanazozipata.

Ndugu zangu mimi ni mhanga mkubwa, nimefanya biashara mbalimbali japo si zote ila nakupa mfano wa chache nilizo na uzoefu.

Kwa ukweli wangu naamini mtaunga mkono kama kweli ninyi ni wakweli na uhalisia ni kwamba kwenye biashara za mtandao mifumo yake ni migumu kukutajilisha na huwezi kupata utajiri kiurahisi. Mfano wa biashara hizo ni kama zifuatazo:-

Forex na mfano wa hizo, hapa najua wapo wengi wanatamani kufanya biashara hizo na baadhi yao wanajigamba wana mafanikio makubwa, Du hapana nasema hapana! Naamini kabisa kati ya watu 100 wanaofanikiwa ni watu 3 hadi 5 na huo ni mtazamo wangu tu ila najua hata watu hao ni wengi sana na hii inaniuma sana.

Kwenye mfumo huo wa FX wanaofanikiwa naamini kabisa ni wale walioutengeneza mfumo huo wa biashara ukianzia na mifumo yao ya kufanyia biashara iwe MT4 au MT5 kute huko ni sehemu ya kuteketezea fedha.

Kwa mfano mtu anaweza kuweka USD 200 lakini ndani ya dakika 20 akawa amepata hasara ya hela yote sasa hiyo ni biashara kweli! Hapana mtamaliza hela zenu bure ni bora hiyo USD 200 zaidi ya TSH 400,000/= ukafanyia biashara nyingine au huu ni uongo? Hata biashara ya nyanya huwezi kupata hasara hiyo yote kwa mpigo ni biashara kweli hiyo au balaa!

Mimi naamini kabisa hakuna biashara ya kukupatia faida kwa mkato na ukawa tajiri zaidi ya kujituma na kuwa mbunifu katika biashara ndogo unayoanza nayo wewe mwenyewe kuliko hizi zinazohamasishwa na vijana.

Wengine wamegeukia kubashiri michezo mbalimbali kwa kuangalia dau linalowekwa, ndugu yangu nako huko usithubutu utamaliza pesa zako tu, kupatia timu zote hasa kwenye JACKPOT sio mchezo ndio maana wanaobashiri wanaweza kuwa 100000 lakini asipatikane hata mmoja, kwenye hii michezo hakuna cha odd ndogo wala kubwa wengi wanalia na faida inaend kwa yule aliyetengeneza mfumo huo ila nyie mnaliwa tu.

Ukija kwenye biashara zenye sura ya upatu kama forever na nyinginezo nazo hamna jipya chini ya jua, ninauzoefu nayo na nimeifanya simaanishi ni biashara mbaya bali uwezo wa kufanikiwa ni mdogo sana wala hatipaswi kudanganyana. Ni vema mtu unapomhamasisha ajue kwamba biashara hiyo ni nzuri ila pia ni ngumu sana kwa mfano unapewa bidhaa/virutubisho uuzie watu ili wanunue na kwa sababu utawaaminisha kwamba zitawasaidia halafu wao wananunua na haziwasaidii au unamuunganisha mtu kuingia kwenye biashara hiyo kwa zaidi ya Tsh210, 000/= Za kianzio ambapo akishaingia anawaza tu kuwa tajiri bila kujua kwamba wakati mwingine hata bidhaa alizopewa kwa kuanza nazo wakati mwingine hata hazipati wateja! Mwishowe unavunja urafiki naye na kuwa maadui,.

Ni heri sisi tubadilike na tujue biashara zinazoendelea mitandaoni zinamaliza na kukausha fedha tunazozitafuta kwa nguvu na jasho letu na hizo fedha zikiteketea huko tunabakia hatuna wa kumlaumu zaidi ya kuumia mioyoni mwetu tu.

Nawaomba ndugu zangu tufanye kazi kwa bidii na tuwe wabunifu kwa kutengeneza vyanzo sahihi vya fedha na usihadaike na kudanganywa kuingia kwenye biashara ya mtandaoni bila kuwa na elimu ya kutosha kwani huko unaweza kuishia kulia tu.

ASANTENI SANA.
 
Upvote 65
Unashangaa $3k wakati watu wanachoma hadi $80k juzi bro mmoja hivi kachoma hiyo pesa. Yani kwenye forex na indices ukipoteza ndo imeenda hivyo..
Alitaka kuwa tajiri ndani ya muda mchache.
Mtu wa mtaji huo hatakiwi hata ariski zaidi ya $300-800 to every trade.
Risk management ndiyo inayokuza akaunti. Na si mengine.you are risk manager
 
Alitaka kuwa tajiri ndani ya muda mchache.
Mtu wa mtaji huo hatakiwi hata ariski zaidi ya $300-800 to every trade.
Risk management ndiyo inayokuza akaunti. Na si mengine.you are risk manager
Ni kweli mkuu Risk Management ndo nidhamu ya kwanza kwenye hii industry.
 
T14 Armata karibu BARAZA LA WAZEE TANZANIA na hongera [emoji122]
Inaumiza kichwa sana. Huo muda ukiamua usome blogging, adobe, content writing na vitu kibao unajikuta unajua madude na unapata angalau hela ya kuishi kwa siku. Sasa unasoma Forex msuli wake hata daktari ni kama chekechea alafu hupati faida. Huwezi kuwa na nuru, unajaa hasira na fake expectations, unapoteza muda, unakula hasara kibao
 

Pole sana, ila ninachoweza kusema kwa uzoefu wangu ni kwamba kila biashara inahitaji uzoefu na akili ili kutoboa.

Ukiwa na akili ya short-cut kwamba nitatoboa fasta ndani mwezi mmoja hapo ndo ni rahisi kukata tamaa na kuwa frustrated.

Mfano kati ya Forex na Kubeti bora kubeti. Hizo biashara mbili zote ni kamari, ila forex ni kamari ambayo haichezwi kwa uwazi kama mechi za soka. Na kwa Tanzania Forex haina ulinzi kwa kuwa haiko regulated. Mchezeshaji anaweza akatokomea na pesa zenu msijue hata pa kuanzia. Maana ile ni kama benki tu, mnaweka hela zenu kwa mtu awatunzie.

Na pili hapo ulipoongelea Jackpot ndo nimeona unjuka wako. Jackpot achana nazo kabisaaaaa. Zile ni mtego wa kuvuna hela. Na mikeka pia achana nayo chagua mechi moja ya uhakika kila siku.

Siri ya kubeti ni akili. Akili ikishachoka kuchambua mechi kwa sbb unatengeneza mkeka mreeefu ndo hapo unapoliwa. Ila ukiwa unatafuta mechi moja moja kila siku na kuongezea ulipoishia jana yake ni rahisi kupata milioni 80 ndani ya mwezi mmoja tu.

Mengine ni nenda mdogo mdogo. Kubeti kunahitaji angalau mwaka mmoja wa uzoefu (yaani upate uzoefu wa ligi mbalimali) ndo utaanza kupiga hela. Kwa hiyo sio umeanza tu unaweka madau ya elfu kumikumi au ada ya shule kama madenti wanavyofanya. Anza na madau ya jerojero. Utaliwaliwa kama mwaka mzima hivi ndo unajifunza. Laki mbili inatosha kwa kujifunzia mwaka wa kwanza. Baada ya mwaka utakuwa unajua mambo mengi sana kama vile mechi za uhakika za kubetia ni zipi, na ubeti nini ktk mechi hizo; kampuni gani zina odds nzuri, na muhimu zaidi ni uzoefu wa kuchambua mechi na mitandao ya kutumia ili kupata data.
 
Mbali na kushiriki mimi naamini mada zinazotolewa si za kupuuza kwani ukizisoma utapata lolote la kukusaidia ndugu yangu hatushiriki ili kushinda tu bali hata kuelimishana.
Unaelimisha katika kitu ambacho hukijui.Forex unaita short cut , unapotezaje dola 200 ndani ya dk 20, kama umepoteza hivyo maana yake hujui risk management, hufahamu utumie lot size ya kiasi gani ,hufahamu stop loss uwake wapi , yaani ulipanga usd 200 ikupe faida ya usd 200 ndani yamuda huo unaopoteza yaani forex ulifanya kama betting.

Kushindwa kwako ktk forex kumetokana na attitude yako ,wengi mnadhani forex ni bishara ya kuimaster ndani ya mwezi na kutengeneza hela, haiko hivyo kijana.Watu wanatumia miaka mitatu hadi mitano or more kupata uzoefu na kuwa profitable. Ukiwa master mtaji sio tatizo hata usd 10 unaweza ifanyia maajabu.

Pia fahamu kwamba wanaokuwa wanafanikiwa ktk mambo mbalimbali si kwamba huwa hawakutani na changamoto, ila wako tayari kuinuka na kuendelea mbele haijalishi watashindwa mara ngapi. Soma mfano kitabu cha Think and Grow Rich kuna kitu utajifunza kwa watu wanofanikiwa
 
Forex kuisoma tu na kuijua inavyofanya kazi haitoshi, inatakiwa uifanye muda mrefu ambapo hasara haikwepeki, hivyo ndo namna itakupa uzoefu.
Na uzoefu wako kwenye market ndo unaitajika, knowledge, signals haziwezi kukupa faida yoyote
 
USD 3000 kuichoma ni kutokuwa na risk management, aliruhusu emotion zimuendeshe kwamba ameona mambo yanaenda akatumia leverage kubwa, na yenye risk kubwa.

Kwa kosa hilo hata USD 10000 unaweza kuichoma ndani ya siku moja.

Forex baada ya kupata knowledge kinachofuata ni nidhamu, nidhamu, nidhamu
 
Unashangaa $3k wakati watu wanachoma hadi $80k juzi bro mmoja hivi kachoma hiyo pesa. Yani kwenye forex na indices ukipoteza ndo imeenda hivyo..
Mwambie aweke dola 1,000 niifikishe dola 2,000 halafu anipe dola 500 tu then kila mtu achukue hamsini zake.

Asinijue na nisimjue.
 
Forex kuisoma tu na kuijua inavyofanya kazi haitoshi, inatakiwa uifanye muda mrefu ambapo hasara haikwepeki, hivyo ndo namna itakupa uzoefu.
Na uzoefu wako kwenye market ndo unaitajika, knowledge, signals haziwezi kukupa faida yoyote
Hizi kauli hutolewa milele na milele, kila mtu akifeli Forex hupewa sababu nyingi sana. Huwezi nionesha mtu aliyefanikiwa kwa Forex Tanzania hii, ina maana wote ni vilaza
 
Mwambie aweke dola 1,000 niifikishe dola 2,000 halafu anipe dola 500 tu then kila mtu achukue hamsini zake.

Asinijue na nisimjue.
Eboo mtu katoka kupoteza usd elfu themanini ndo uje kumpa hiyo mia tano tu? Haupo serious mkuu..
 
Wengi wana maneno ya ujasiri kama yako na kuamini wanao pata hasara hawajui hiyo biashara uwe mkweli hii biashara ni ngumu na kuwini ni ngumu hata kama una elimu kiasi gani we mwenye elimu ya kutosha tuletee ushuhuda wako ili na wengine wanufaike kwako.
 
Sina sababu ya kuleta ushahidi kwa yoyote sababu sifanyi kwa ajili ya yoyote, ila uache upotoshaji, kama unaweza poteza usd 200 ndani ya dk 20 wewe sio trader ni mcheza forex.(Waeleze hao uliokusudia kuwafikishia ujumbe unapotezaje usd 200 ndani ya dk 20 ) tofautisha binary option na forex trading.

Kushindwa kwako wewe haimaanishi haiwezekani.Sijasema kwamba forex sio ngumu ila si kwamba haiwezekani,inategemeana na akili ya mtu.
 
Wimbo wa taifa wa Forex traders wa kibongo ni "sina sababu ya kuonesha ushahidi..."

Yani ujue hakuna haja ya wewe kuonesha ushahidi maana haupo. Biashara za mbao, nafaka, madini, kilimo, migahawa, nguo na nyingine zinawatoa watu na tunawaona mitaani. Unaweza kutaja uko mtaa gani Dar au wilaya gani ukatajiwa wafanyabiashara fulani wa niche fulani hapo location yako. Ila wewe hapo huwezi taja Forex trader MMOJA TU aliyefanikiwa kwa Forex popote Tanzania. Achana na wafundishaji hawa hata mimi naweza kuanza kufundisha wiki hii

Forex traders wako successful kwenye keyboard ila on the ground hayuko hata mmoja. Wale kina SomebodyFX
 
Kwanini mimi nikuoeneshe wewe mtu wa mtandaoni ushuhuda wa ninachofanya ikiwa hicho kitu nafanya kwa ajili yangu binafsi.Naomba nieleze ni vipi mtu anapoteza usd 200 ndani ya dk 20 , asante
 
Leo kuna mwingine ameibuka na P2P kwa wiki faida laki uwe na safal com laini na bongo voda com!
 
Eti.. "Siri nyingine nakuibia" Jinga sana.

Utaendelea kuwa masikini hohehahe while kuna watu wanakula kuku na mvinyo kwa hela zako huko Bahamas.
 
Mat@ko yako.
 
[emoji867][emoji867][emoji867][emoji867]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…