Tahadhari: Dawa za Kichina Husababisha Saratani (kansa)

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
PERTH, Australia

UTAFITI uliofanywa hivi karibuni na timu ya wataalamu wa Chuo Kikuu cha Murdoch mjini hapa, umebaini kuwa dawa kadhaa za asili za China zina sumu hatari kwa wanyama na binadamu.

Kiongozi wa utafiti huo, Dk. Mike Bunce, alikiri kuwa dawa za Kichina hufanya kazi haraka, lakini akasema watu wanapaswa kuchukua tahadhari kutokana na vitu vinavyochanganywa kutengeneza dawa hizo.

Ili kupata matokeo hayo, watafiti walitumia vifaa vya kisasa kuchunguza nini hasa kilichomo ndani ya aina 15 tofauti za dawa asilia za China.

Bunce alisema walikuta aina
68 ya mimea tofauti ikiwamo ile ya sumu aina ya 'ephedra' na 'arum'. Alisema mtu anaweza kudhurika iwapo atakunywa dawa hizo au kama mwili wake hautakubaliana na dawa hizo.

Hakukuwa na usumbufu wala wasiwasi wowote kwa raia wa China wanaofanya biashara ya dawa hizo, kwa kuwa wanafanyha hivyo kihalali na kwa mujibu wa sheria kwani huhakikiwa na mamlaka husika nchini Australia.

Hata hivyo, Mkurugenzi wa Taaluma wa chuo hicho, Peter Farnsworth, alisema ingawa huenda waganga hao wa Kichina wako sahihi, si rahisi kwa mtu kununua dawa zao kwa njia ya mtandao. Tahadhari: Dawa za Kichina Husababisha Saratani

HAYA MUJIHADHARI NA MADAWA YA KICHINA YANALETA MARADHI YA KANSA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…