Tahadhari: Giza limeota macho halafu lina masikio

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
301,577
Reaction score
754,412

Ndugu zangu hamkani si shwari tena...you are being watched n monitored!take care
Uhuru wa kupashana habari umeingia kitanzini... mitandao ya kijamii imebanwa mbavu.... mada nyingi zenye kukosoa utendaji hazidumu tena popote
Kamatakamata ya kimyakimya inaendelea....kama wewe ni mpenzi na mkereketwa wa siasa za upinzani..badili mtazamo wako sasa...kimenuka na kumenuka
Tunarudi kwenye zama za kuongelea chini ya zulia kunong'ona na kunong'onezana utafikiri mahaba ya wizi
Tunarudi kwenye zama za kuangalia kushoto na kulia mbele na nyuma juu na chini kabla hatujaongea dukuduku
Ni kama maji yenye kina kirefu sana..yametulia tuli lakini Usijaribu kuingia....!tutakupoteza mara

Kuna jicho kali katili kizani LIOGOPE...! Tena liogope hasa..koleo na bisibisi vipo tena vipo sana na vimekolezwa makali...! Lala ukijua hilo amka ukitafakari
Nilisema na naomba niseme tena wakimaliza juu wakimaliza katikati watakuja chini....hawako mbali sasa...hawaonekani kwa macho lakini mvumo wao unasikika...JIHADHARI
Where we dare to talk openly inaelekea kubaki story[emoji144] [emoji144] [emoji144] [emoji15] [emoji35] [emoji15] [emoji35] [emoji25] [emoji25] zinaumiza sana hizi hisia... tunaupa mwanga kisogo na kulikabili giza linaloogofya...! Giza lenye macho makali na masikio marefu

Wakati utaamua...! Wakati utasema...! Lakini kwasasa vuta handbrake...! You are being watched n monitored
 
Mshana unayoyasema ni sahihi kabisa. Toka jana ujumbe wa kuombeana na kuonyana imekuwa ikitembea katika social media. Ni lazima tuambiane, epuka kutoa comment hasi kwenye social zinazohusu POMBE hasa kama wapo wanaokutegemea. . Wanasiasa wanajuana, sio sisi makapuku... Ila pooa tu, wacha yatutese haya maan tuliipenda wenyewe....

Kuhama kazi hawataki, Ukiacha kazi hupati mafao....Pengine labda kwa kuwa umeanzisha hii thread wewe haitanyofolewa. Maana JF siku hizi post za kumkosoa JPM zinanyofolewa fasta.
 
Naomba hii isije ikatafsiriwa kwa muktadha wa kukosoa...haya ni manung'uniko ya kujifariji kujipa moyo na kujipa kampani....! Walioko vitandani saizi wanafaidi joto la kwao...tukeshao gizani tunatafakari mengi[emoji144] [emoji144] [emoji25] [emoji25] [emoji24] [emoji24]
 
Silaha yao kubwa ni hii hapa tunalazimishwa kufunga midomo yetu kwa kitisho cha bangili za chuma na chumba giza cha dirisha moja dogo la nondo
 
Ni hatari tena si hatari ndogo hata ya M7 yana ahueni. 😱😱😱😱😱😱😱😱

[emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji144] [emoji144] [emoji144] [emoji144] [emoji134] [emoji134] [emoji134] [emoji134] [emoji124] [emoji124] [emoji124] [emoji124]
 
Ni hatari tena si hatari ndogo hata ya M7 yana ahueni. 😱😱😱😱😱😱😱😱
Tunataka au tunaelekea kufanana na Burundi na Rwanda in terms of freedom of speech....
Kuna kitu kinajaribu kujengwa kwenye hii jumuiya.... Tanzania ndio ilikuwa kimbilio lakini sasa mmh!!!
Ya Uganda ya Kenya ya Burundi na Rwanda katika ujumla wake yameshapandikizwa kwetu tayari
Nini kinafuata?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…