DOKEZO Tahadhari - Kampuni ya Upatu TIT

DOKEZO Tahadhari - Kampuni ya Upatu TIT

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Hii Kampuni ambayo inaonyesha kusajiliwa Tanzania, ina dalili zote za kitapeli kama makampuni mengi yahayojitangaza kufanya biashara ya Sarafu za kidigitali (BITCOIN).

www.titmining.com

Wameweka kwenye tangazo lao nyaraka za usajiri ili kuvutia watu lakini uzoefu kampuni za aina hii asilimia 99.99% ukiweka hela zako utapigwa tu!. Mwanzoni utapata kidogo na kuvutiwa kualika wengine hata kupata ushawishi wa kuongeza mtaji.

Kuna kampuni kama BestWay Capital Management (BCM) iliyokuwa na ofisi zake Masaki, ilikuwa na nyaraka za usajili na wafanyakazi lakini mwishowe imeondoka na zaidi ya TZS 16,000,000,000 za watanzania na wengi wakiwa ni wastaafu.

Muhimu tutambue, hakuna hela inayopatikana kirahisi kama wanavyotangaza. Wekeza kwenye mabenki, UTT, Bond za BOT na hisa zinazotangazwa na DSE au popote palikosajiliwa kwenye masoko ya mitaji. Kwa Tanzania CMSA.

Hela inatafutwa kwa taabu sana kuipoteza kirahisi itakuuma sana. kuweni makini
 

Attachments

Back
Top Bottom