Tahadhari kwa wajasiriamali wenye mitaji midogo

Baba Nusa

New Member
Joined
Jul 3, 2011
Posts
2
Reaction score
0
Kufanya biashara na idara za serikali kuu na hata halmashauri is at your own risk,hawalipi kabisa,wanasema serikali haina hela,OC inauyopolekwa haitoshi!mambo yamebadilika sio kama zamani
 
watasemaje hela hakuna na tayari umeshawafanyia kazi yao? na wewe ulikubali vipi kuanza kazi bila kupewa hata advans?

na ni kweli hakuna au ndio mdudu wa ufisadi....!!
 
watasemaje hela hakuna na tayari umeshawafanyia kazi yao? na wewe ulikubali vipi kuanza kazi bila kupewa hata advans?

na ni kweli hakuna au ndio mdudu wa ufisadi....!!
Ni kweli anachosema mdau. Kwani wameweka taratibu kuwa hulipwi mpaka ukamilishe order. Lakini ukikamilisha ndio mtihani unapoanza. Mara pesa hazijafika, mara tunasubiri hazina/donor etc. Mara nyingi utakuta pesa ambazo wangekulipa wametumia kwa matumizi yao ya ofisi na wakati mwingine siyo ya lazima. Hapa ni kuwashitaki tu ndio dawa. Ingawa ukifungulia mashtaka serikali ndio mpaka upate kibali toka kwa Attorney General na utoe notisi ya miezi 3. Hapo ukimaliza hiyo kesi hutegemei tena kupata order toka serikalini. Yaani we acha tu.

Wakati wa Rais wa awamu ya tatu. Ilikua mtu hawezi pewa order kama hana LPO ambayo pesa zake pia zipo. Hivyo ilipunguza kasi ya kuchelewa malipo. Lakini sasa hivi ni mtihani.
 
ni kweli kabisa anachosema mdau.. Kwani ukikamilisha... Utaambiwa subiri bajeti.. Mara chq iko kwa mkuu wa idara haijasainiwa.... Yaani kwa kweli mzunguko na mlolongo ni mrefu mno hadi wanakatisha tamaa
 
watasemaje hela hakuna na tayari umeshawafanyia kazi yao? na wewe ulikubali vipi kuanza kazi bila kupewa hata advans?

na ni kweli hakuna au ndio mdudu wa ufisadi....!!

Ndugu yangu, ni mtihani mkubwa kufanya biashara na Serikali au Halmashauri maana baada ya kukamilisha kazi ndio utajua ni hasara kiasi gani umeipata kwa huo ususmbufu wa kulipwa. jaribu ili uone mambo yakoje labda kwa kusimuliwa uankuwa huelewi nini kinachoendelea.
 
watu wengi walikuwa wanafanya kazi na serikali kwa imani kuwa serikali lazima watalipa wakati wa awamu ya tatu rais aliweka utaratibu hamna kutoa kazi mpaka pesa za kazi ziwepo kazi ilifanyika na watu walilipwa lakini sasa hv unapewa kazi ukimaliza malipo yake ni kasheshe kwa wale wenye mitaji midogo wengi wanakufa kibiashara na bado wanataka ulipe kodi tra bado kodi ya ofisi ushauri wa mtoa mada ni kweli
 
Mimi mwaka mmoja kwenye miaka ya 90,chupu chupu wilaya ya kisarawe inifanye nifirisike!Sio siri kufanya kazi na serikali ni ishu
 
Mimi mwaka mmoja kwenye miaka ya 90,chupu chupu wilaya ya kisarawe inifanye nifirisike!Sio siri kufanya kazi na serikali ni ishu
Tatizo watendaji wengi (watumishi wa umma) ni wezi, wahujumu na mafisadi. ukienda TRA, Hazina, nk angalia kesi zilizo mahakamani hata ile inayohusisha hujuma shirika la UDA.Tatizo watu wamegeuza ofisi za umma kama viwe binafsi vya kuchuma mali kwa njia haramu.
 
Kuogopa huo usumbuf kuna network marketing nzuri ambazo unaweza kuifanya ukapata hela nzuri isiyo na longolongo, why all that? Pm to show you how
 
Kuogopa huo usumbuf kuna network marketing nzuri ambazo unaweza kuifanya ukapata hela nzuri isiyo na longolongo, why all that? Pm to show you how

Iweke peupe hiyo njia kama unajiamini, kama hujiamini kaa nayo huko huko. Hapa hatufichani maarifa.
 
penyeza rupia kwa DT baada ya sekunde chache tu utapewa hundi yako chezea fisadi wewe
 
watasemaje hela hakuna na tayari umeshawafanyia kazi yao? na wewe ulikubali vipi kuanza kazi bila kupewa hata advans?

na ni kweli hakuna au ndio mdudu wa ufisadi....!!

Unaelewa lakini procurement za serikali zinavyoenda?!!!
 
Kufanya biashara na idara za serikali kuu na hata halmashauri is at your own risk,hawalipi kabisa,wanasema serikali haina hela,OC inauyopolekwa haitoshi!mambo yamebadilika sio kama zamani

Ni kweli mkuu, kama una mtaji wa mawazo usifanye kazi na serikali, la sivyo fanya kazi zenye LPO pekee, hizo ina maana wanapo-alocate fund ina maana zipo hizo pesa na ukiona wanakucheleweshea ujua kutoa pesa tu!!
 
Wafanyabiashara ambao ni serious kufanya biashara na serikali ni kujimaliza,wao wana ka msemo kao kamoja,'tutakulipa pesa unayotaka kwa wakati tunaotaka',sasa ukirogwa tu kufanya nao business utajuta kuwafahamu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…