Gottee
R I P
- Sep 7, 2008
- 174
- 2
Kuna mengi yanazungumzwa mitaani kwa sasa masaa machache kabla ya Uchaguzi. Katika yanayosemwa kuna MBINU CHAFU inapangwa kuwakamata vijana wanaoonekana kuwa ni washabiki wa CHADEMA na kuwasweka Lupango kama Wazurulaji. Ombi kwangu ni kujaribu kuwa makini katika muda huu ikiwemo kurudi nyumbani mapema.
Inasemekana pia kuna kundi kubwa la vijana wamekosa majina yao kwenye daftari la wapiga kura. Vijana wengi wamekuwa hawafichi namna walivyochoshwa na Utawala wa CCM hivyo inawezekana kabisa majina yao yalikuwa yakiorodheshwa na huenda yamefanyiwa kazi.
Pia nimeambiwa kuwa ile karatasi ya kupigia kura ina walakini. Unapoikunja baada ya kumaliza kupiga kura inasemekana mgombea wa CHADEMA na mgombea mwingine (Sio CCM) wanatazamana kwa hiyo inawezekana kabisa ie alama uliyoweka kwa mgombea wa CHADEMA inaweza kuonekana pia kwa mgombea mwingine na kwa maana hiyo kura itakuwa imeharibika. Naomba tuwe makini kwani SAA YA UKOMBOZI IMEWADIA
Nawasilisha