Elections 2010 Tahadhari Kwenu Vijana Wenzangu

Gottee

R I P
Joined
Sep 7, 2008
Posts
174
Reaction score
2
Kuna mengi yanazungumzwa mitaani kwa sasa masaa machache kabla ya Uchaguzi. Katika yanayosemwa kuna MBINU CHAFU inapangwa kuwakamata vijana wanaoonekana kuwa ni washabiki wa CHADEMA na kuwasweka Lupango kama Wazurulaji. Ombi kwangu ni kujaribu kuwa makini katika muda huu ikiwemo kurudi nyumbani mapema.

Inasemekana pia kuna kundi kubwa la vijana wamekosa majina yao kwenye daftari la wapiga kura. Vijana wengi wamekuwa hawafichi namna walivyochoshwa na Utawala wa CCM hivyo inawezekana kabisa majina yao yalikuwa yakiorodheshwa na huenda yamefanyiwa kazi.

Pia nimeambiwa kuwa ile karatasi ya kupigia kura ina walakini. Unapoikunja baada ya kumaliza kupiga kura inasemekana mgombea wa CHADEMA na mgombea mwingine (Sio CCM) wanatazamana kwa hiyo inawezekana kabisa ie alama uliyoweka kwa mgombea wa CHADEMA inaweza kuonekana pia kwa mgombea mwingine na kwa maana hiyo kura itakuwa imeharibika. Naomba tuwe makini kwani SAA YA UKOMBOZI IMEWADIA

Nawasilisha
 
Inasemekana pia kuna kundi kubwa la vijana wamekosa majina yao kwenye daftari la wapiga kura.

Majina yameshawekwa hadharani?

Pia nimeambiwa kuwa ile karatasi ya kupigia kura ina walakini. Unapoikunja baada ya kumaliza kupiga kura inasemekana mgombea wa CHADEMA na mgombea mwingine (Sio CCM) wanatazamana.......

NANI kakwambia? tupe sourse (ya uhakika).....Please
 
Ilishatolewa kauli kwamba Vijana wengi inaelekea hawaipendi thithiem, sasa hili likitokea itakuwa ni mbinu chafu ya kupata ushindi maana watafanikiwa kupunguza idadi kubwa ya wapigaji kura wa chadema.
 
watakamata wangapi????? hizo ni propaganda tu.kwanza polisi hawatoshi na tanzania kubwa sana.Cha muhimu vijana sikuku hiyo wawe makini kukaa kijiweni hadi wadumbukize kura ndo waanze kukaa vijiweni

SLAA NDIYO MPAKWA MAFUTA WETU.NDIYE ALIYEMPENDEZA BWANA MUNGU TUMSIKILIZE YEYE.
 
Mkuu, nimeshtuka na hii habari kwamba karatasi za kupigia kura zina utata!
Usihofu, ukikunja hawa watu hawatazamani, Karatasi ya mwaka huu unapiga kura pembeni ya mgombea na si chini ya mgombea hivyo autakunja in a way that JJ na WS wakatazamana. thanks
 
Hata mimi jina langu halipo kwenye orodha ya wapiga kura,nimefuatilia lakini hakuna nachoelezwa cha maana!!
 
Lumaga,

Hata wakikamata mmoja ni mtaji wa kutosha huo kumbuka wameanza kuwapunguza kwenye kura kwa kuanza kununua shahada zao. Sasa Wamewanyofoa kwenye daftari na huo mpango wa kuwasweka lupango. Rai yangu tena vijana wawe makini sana na masaa machache yaliyobaki. Kwa WENDAWAZIMU hawa lolote linawezekana. Viongozi wa CCM wamekuwa wakipita nyumba kwa nyumba wakiomba kura lakini kuna kazi ya ziada ya kuwajua pia wapinzani wao licha ya kununua kura hizo.

SLAA hawezi kuwa mshindi mpaka kura zitoshe na ili zitoshe ni kila tone la kura zetu tunalihitaji na kwa maana hiyo si DHAMBI kuwatafadhalisha jamaa zetu waepuke kukutana na WAPUMBAVU wasioitakia nchi yetu mema.

Consultant

Kwa hili sihitaji kutafuta source (ya uhakika) ndio maana nimetoa kama TAHADHARI aliyenielewa amenielewa asiyenielewa hajanielewa, lakini sihitaji kwenda kuhakikisha nje kuna Simba Mla watu kwa sababu simwamini jirani yangu aliyenipigia simu kuniambia yupo nje ya nyumba yangu au vipi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…