Halisi
JF-Expert Member
- Jan 16, 2007
- 2,802
- 614
Katika hali isiyo ya kawaida, majambazi wamejipanga kwa kuunda kikosi kazi (task force) ya kupambana na wenye mali (wananchi) hasa wale wenye kupenda kupiga kelele za "wezi hao!!!! Wezi hao!!!!".
Kazi ya task force hiyo imeanza kwa kasi na tayari baadhi yao wamo humu JF na wanawashughulikia wale wote wanaopiga kelele za mwizi.
Niliwahi kuona pale Kariakoo kibaka anapora simu na anapofukuzwa wenzake wanamsindikiza na kumgeuzia kibao aliyeibiwa na kuanza kumdunda kwamba ndiye mwizi na wakati mwingine mwenye mali huuwawa na kuchomwa moto.
Hali hiyo sasa imeingia kwa majambazi wakuu na sasa kazi imeanza kwa kasi na wale wote wanaopiga kelele za mwizi (akiwamo Mwanakijiji) wajiandae kugeuziwa kibao na kufukuzwa, wakati wao (familia zao) ndio walioibiwa na majambazi wakuu.
Majambazi hao wanakutana usiku na mchana na wana fungu kubwa kwa kazi hiyo ya kujilinda.