Usedcountrynewpipo
JF-Expert Member
- Aug 1, 2012
- 3,636
- 2,728
Makampuni au wataalam wengi wanapofanya decision huwa wanaforecast environmental changez zinazoweza ku affect maamuzi yao. Lakini Sio kwa hapa Bongo.
Juzi juzi tu tumeona makampuni ya vinywaji yakilalamika kuhusu kuongezeka kwa ushuru wa hadi asilimia 20 ihali bunge likipitisha asilimia 10 tu!
Hali ndivyo ilivyo kwenye biashara ya uagizaji magari.
Mwezi wa Tano/ Sita sio mwezi mzuri kuagiza gari kwa mantiki ya ushuru. Serikali imekuwa haitabiriki kwamba ushuru utakuwaje. unaweza ukaandaaa milioni tano za kulipia ushuru, mara ukaambiwa ushuru umebadilika na unatakiwa kulipa Milioni saba! Hapo hujaacha gari bandarini bado?
Kwa nini mwezi wa sita?
Mzunguko uko hivi, zoezi la kuulizia gari mpaka malipo yafanyike huchukua wiki moja, kubook meli mpaka gari lipakiwe huchukua takrabini wiki mbili, gari mpaka lifike kutoka Japan huchukua wiki nne, na zoezi la ku clear bandarini huchukua angalau wiki moja. Jumla hapo ni wiki nane. Sawa na miezi miwili.
kwa hiyo kama umenunua gari kuanzia mwezi wa tano hadi wa sita, hesabu maumivu kwenye suala la kodi.
Ni bora kuagiza gari mwezi wa nne kabla kodi kubadilika, au kungoja mpaka uone kuwa utatakiwa kuzichanga kiasi gani.
La sivyo unaweza ukatelekeza gari lako zuri bandarini!