Tahadhari: Nguo za Ndani Zachangia Ugumba kwa Wanaume

Tahadhari: Nguo za Ndani Zachangia Ugumba kwa Wanaume

Power G

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2011
Posts
3,884
Reaction score
1,198
TAFITI za kisayansi zimebaini kuwa nguo za ndani hasa zinazobana kwa wanaume na zile za aina ya nailoni (nylon) zinaathiri uwezo wa mbegu za kiume, hivyo kushindwa kutunga mimba.


Utafiti huo uliofanyika katika nchi za Ufaransa na Uingereza na kuchapishwa katika Gazeti la Daily Mail la Uingereza unabainisha kuwa, wanaume wanaovaa nguo za ndani zinazobana na zile zilizotengezwa kwa malighafi ya nailoni, mbegu zao za kiume (manii) huwa nyepesi na kupoteza uwezo wa kutunga mimba.


Vazi la ndani la wanaume linalojulikana kama boksa na nguo nyingine za ndani za kubana zenye asili ya nailoni, zinakuwa na athari kubwa zaidi hasa zinapovaliwa katika sehemu zenye joto, kama Dar es Salaam.


Kutokana na matokeo hayo, wanasayansi wameonya kuwa wanaume wanapaswa kuchukua tahadhari, hasa kutokana na tafiti nyingi za karibuni kuthibitisha kuongezeka kwa matatizo ya mbegu za kukosa uwezo wa kutunga ujauzito katika nyumba ya uzazi ya mwanamke.

Akizungumzia utafiti huo jana, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Wanawake na Uzazi katika Hosipitali ya Taifa Muhimbili, Dk Cyril Massawe, alisema una ukweli kutokana na mbegu za kiume kuwa nje ya mwili wa mwanamume tofauti na mwanamke ambaye kizazi chake kipo ndani.
 
Hii habari inatishia wale ambao hatujapata watoto, inabidi niifikishe kwa mr jinsi ilivyo bila kuifanyia editing yoyote, ili ikiwezekana asivae nguo ya ndani kabisaa.
 
Hii habari inatishia wale ambao hatujapata watoto, inabidi niifikishe kwa mr jinsi ilivyo bila kuifanyia editing yoyote, ili ikiwezekana asivae nguo ya ndani kabisaa.
Mshauri avae za cotton na zisiwe za kubana ili "vifaa" vipate hewa ya kutosha
 
Kwishney, ndo maana ktk utafiti uliofanyika ktk hosptl ya Muhimbili, 40% ya waliokwenda kupima Dioxyribonucleic Acid (DNA), Wamegundulika kuwa wanalea watoto wasiokuwa wao! Ahsante mkuu kwa hii thread, itawasaidia wengi, mimi nilishatoka huko!
 
heeeeeeeeeeeeeee ngoja nikatafute fasta nisije kukosa kababy asante kwa kunifahamisha mapema
 
hii habari inatishia wale ambao hatujapata watoto, inabidi niifikishe kwa mr jinsi ilivyo bila kuifanyia editing yoyote, ili ikiwezekana asivae nguo ya ndani kabisaa.
mshauri hata chu.. Asivae kwa usalama wake na wako pia.
 
Dah! Na mabinti wanavyovaa barabarani siku hizi full mifadhaiko imagine simu inakamata network halafu ndani kufuliless duh sipati picha!
 
Achilia mbali hizo tafiti, ukivaa nguo ya ndani inayobana inakunyima uhuru kiasi fulani, ila sipati picha kwa wale wanaume ambao jogoo huwika hata akisikia mlio wa upepo......Kwa niaba ya watafiti nawapa pole hawa
 
Duh afadhali nimemaliza kazi japo sijajua wangapi nidamu yangu katika wale wanne, potelea pote kitanda hakizai haram.
 
Mimi toka zamani nilikuwa mgumu sana kuvaa hivi vitu, huwa navaa kwa nadra sana katika utu uzima wangu nilionao na kama nikivaa(occassionally) ni boxer ya cotton ambayo haibani, ni muhimu sana kwa 'mkubwa na wanawe' kupata maximum ventilation kwa ustawi wa jamii!
 
Mimi toka zamani nilikuwa mgumu sana kuvaa hivi vitu, huwa navaa kwa nadra sana katika utu uzima wangu nilionao na kama nikivaa(occassionally) ni boxer ya cotton ambayo haibani, ni muhimu sana kwa 'mkubwa na wanawe' kupata maximum ventilation kwa ustawi wa jamii!
Mkuu wewe ulipata matokeo ya utafiti huu mapema, au ni machale tu?
 
Back
Top Bottom