Tahadhari! Nyumba ya kuishi siyo Uwekezaji

Makirita Amani

JF-Expert Member
Joined
Jun 6, 2012
Posts
1,915
Reaction score
3,422
Rafiki yangu mpendwa,

Kwenye safari ya kujenga utajiri, uwekezaji ni kiungo muhimu sana.

Watu wengi wamekuwa wanachanganya kipato kikubwa (rich) na utajiri (wealth).

Wengi huwa na maisha mazuri pale wanapokuwa na kipato kikubwa, kinachokuwa kinatokana na kazi au biashara wanazofanya.

Lakini pale kazi au biashara hizo zinapoisha, huwa wanarudi kwenye maisha duni kwa sababu hawakuwa wamefanya uwekezaji wa kuyawezesha maisha yao kwenda.

Na siyo kwamba wengi wanaokuja kuwa na maisha duni baadaye hawakuwa na uwezo wa kufanya uwekezaji. Waliweza sana, lakini hawakuwa na maarifa sahihi ya nini ni uwekezaji na nini siyo uwekezaji.

Kwa mfano, watu wengi huwa wanadhani kujenga nyumba ya kuishi ni uwekezaji, kitu ambacho siyo. Nyumba unayojenga kwa ajili ya kuishi wewe, siyo uwekezaji. Haijalishi unaamini kiasi gani, ukweli ni siyo uwekezaji.

Kabla hujapatwa na hasira, maana ukiwa umeshajenga nyumba ukiamini ni uwekezaji halafu anatokea mtu na kukuambia siyo, hutajisikia vizuri. Tuangalie kwanza maana ya uwekezaji halafu turudi kuiangalia nyumba ya kuishi kama ina sifa hizo.

Uwekezaji ni kitu ambacho kinakuingizia wewe kipato bila ya kufanya kazi moja kwa moja. Yaani uwe umelala au unafanya mambo yako mengine, kipato kinakuwa kinaingia. Ukishahusika tu kwenye kufanya ndiyo kipato kiingie, tayari hapo siyo uwekezaji.

Tukianza tu na hiyo maana ya uwekezaji, tayari nyumba ya kuishi inakosa sifa.

Twende kwenye utetezi ambao utakuwa nao kwamba nyumba inachangia sehemu ya utajiri wako kwa kuthaminishwa kwake. Ndiyo, hilo ni kweli, lakini je unapanga kuiuza nyumba hiyo ili uvune utajiri huo? Jibu ni hapana, huwezi kuuza kwa sababu ndiyo unaishi.

Utetezi mwingine utakaokuwa nao ni kwamba unaweza kutumia nyumba kupata mkopo ambao utautumia kwa shughuli nyingine za uwekezaji. Hilo ni kweli, lakini huo mkopo utahitaji kuufanyia kazi na kufanya marejesho, kazi lazima iwekwe.

SOMA: Jinsi Ya Kujenga Utajiri Wa Mwendokasi.

Swali ni je watu wasiwe na nyumba? Jibu ni hapana, kuwa na nyumba kulingana na mipango yako. Mimi binafsi nina nyumba na nashauri kila anayeweza awe na nyumba.

Lakini nataka nikupe tahadhari kubwa, kwa thamani ile ile ambayo umewekeza kwenye nyumba yako ya kuishi, hakikisha pia unaiwekeza kwenye maeneo mengine yanayoweza kuzalisha faida bila ya wewe kufanya kazi moja kwa moja.

Ninachomaanisha ni kama una nyumba yenye thamani ya milioni 50, basi hakikisha una uwekezaji mwingine wa milioni 50 ambao unakuingizia faida bila ya kufanya kazi moja kwa moja. Utawekeza wapi hiyo milioni 50 nyingine ni juu yako, lakini muhimu ni uweze kuingiza kipato bila ya kufanya kazi moja kwa moja.

Na kama hujui wapi pa kuwekeza, basi nikushauri uwekeze kwenye masoko ya mitaji, yaani hisa, vipande na/au hatifungani. Huko kunakupa marejesho bila ya kufanya kazi moja kwa moja. Na japo marejesho yanakuwa madogo, lakini kwa muda mrefu unajenga utajiri mkubwa huku ukiwa unaendelea na mambo yako mengine.

Najua hili ulilojifunza hapa litakufanya usijisikie vizuri, kwa sababu kwa maisha yako yote umekuwa unaaminishwa nyumba ya kuishi ni uwekezaji. Fanyia kazi hili ulilojifunza hapa, kama tayari una nyumba ya kuishi, basi fanya uwekezaji wenye thamani sawa na nyumba hiyo ili ujiweke mahali pazuri.

Kwenye kipindi cha ONGEA NA KOCHA hapo chini nimefafanua zaidi hali hiyo ya nyumba ya kuishi kutokuwa uwekezaji na hatua za wewe kuchukua. Karibu ujifunze na kuchukua hatua ili uweze kujiweka vizuri kwenye eneo la fedha.

View: https://youtu.be/BctC4q91Zto

Nenda kayaweke haya uliyojifunza kwenye matendo ili uweze kujenga mafanikio makubwa kwenye maisha yako kwa kuiishi kila siku yako kwa mafanikio makubwa.

Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,

Kocha Dr. Makirita Amani,

Daktari |Mwandishi |Kocha |Mkufunzi

+255 678 977 007 / amakirita@gmail.com

www.amkamtanzania.com

MUHIMU; Rafiki, nikushukuru kwa kuendelea pamoja kupitia mafunzo haya ninayotoa. Karibu kwenye huduma zaidi ninazotoa, kuanzia 1. VITABU, 2. NGUVU YA BUKU, 3. KISIMA CHA MAARIFA, 4. CHUO CHA MAUZO na 5. BILIONEA MAFUNZONI. Kupata maelezo ya huduma hizi, tumia mawasiliano yaliyopo hapo juu. Karibu sana.
 
"Tahadhari! Nyumba Ya Kuishi Siyo Uwekezaji" hii kauli ya kinafki saana, mzee inategemea umejenga hyoo nyumba ukiwa katika situation gani, una watoto/wategemezi (apa nyumba haiepukiki kaka) unaelewa kwa nini huwa watu wanatafuta kumiliki pesa(the transaction motive, the precautionary motive, and the speculative motive.)

Hizi story za motivation speaker mnaharibu jamii saana,sio kila mtu yupo interested na mnavyotaka ninyi
 
SOMA; Jinsi Ya Kujenga Utajiri Wa Mwendokasi.

Mkuu hakuna yeyote anayeweza kutoa madai hayo ya kuwa nyumba ya kuishi ni uwekezaji, au mwenyewe uliwahi kusikia watu wakiongea hayo madudu?

Uwekezaji kwa jina jingine ni 'mradi'.
Nyumba ya makazi ni sawa na suruali uliyovaa mwilini mwako, sasa ni lini nguo uliyovaa mwilini mwako yaweza kukuletea faida?

Faida yake ni kukustiri mwenyewe na siyo kukuingizia pesa kama ilivyo kwa nyumba ya kuishi.

Kwa uwekezaji wa nyumba, ni nyumba za kupangisha ama guest house, ambavyo hivi haujavisema!

Kama ulivyosema, hati fungani ama account ya muda maalumu bank ni uwekezaji pia.

Lakini uelewe kuwa katika mambo ya uwekezaji watu wana vipawa na mbinu mbali mbali za utafutaji.

Sasa kwa sababu umeamua kusaidia watu, ungelikuja na theory za mbinu mbali mbali za kufanya miradi ya uwekezaji ili watu wavune maarifa, siyo kuishia kwenye hati fungani na UTT pekee.
 
"Tahadhari! Nyumba Ya Kuishi Siyo Uwekezaji" hii kauli ya kinafki saana, mzee inategemea umejenga hyoo nyumba ukiwa katika situation gani, una watoto/wategemezi (apa nyumba haiepukiki kaka) unaelewa kwa nini huwa watu wanatafuta kumiliki pesa(the transaction motive, the precautionary motive, and the speculative motive.)

Hizi story za motivation speaker mnaharibu jamii saana,sio kila mtu yupo interested na mnavyotaka ninyi
Fanya uwekezaji mkuu, ambao unaweza kukuingizia fedha bila ya kufanya kazi moja kwa moja.
Nini ambacho hakieleweki hapo?
Maana naona unakimbilia tu kusema vibaya motivational speakers.
Nimeshakuambia hapo mimi nina nyumba na nashauri kila mtu awe na nyumba, lakini usihesabie kama uwekezaji. Hakikisha unafanya uwekezaji sahihi, hilo ndiyo nasema hapa.
Ila ni kama umesoma mada na kuelewa, na siyo kukimbilia kucoment kwa heading pekee.
 
Mkuu hakuna yeyote anayeweza kutoa madai hayo ya kuwa nyumba ya kuishi ni uwekezaji, au mwenyewe uliwahi kusikia watu wakiongea hayo madudu?

Uwekezaji kwa jina jingine ni 'mradi'.
Nyumba ya makazi ni sawa na suruali uliyovaa mwilini mwako, sasa ni lini nguo uliyovaa mwilini mwako yaweza kukuletea faida?

Faida yake ni kukustiri mwenyewe na siyo kukuingizia pesa kama ilivyo kwa nyumba ya kuishi.

Kwa uwekezaji wa nyumba, ni nyumba za kupangisha ama guest house, ambavyo hivi haujavisema!

Kama ulivyosema, hati fungani ama account ya muda maalumu bank ni uwekezaji pia.

Lakini uelewe kuwa katika mambo ya uwekezaji watu wana vipawa na mbinu mbali mbali za utafutaji.

Sasa kwa sababu umeamua kusaidia watu, ungelikuja na theory za mbinu mbali mbali za kufanya miradi ya uwekezaji ili watu wavune maarifa, siyo kuishia kwenye hati fungani na UTT pekee.
Mkuu,
Asante kwa mchango wako mzuri,
Kama umesoma vizuri mada, nimeeleza specifically nyumba ya kuishi, kwa sababu ni changamoto ambayo nimekuwa naona wengi wanarelax waksihakuwa na nyumba za kuishi badala ya kuendelea kujenga uwekezaji wao, iwe ni kwenye majengo au masoko ya mitaji.
Ndiyo, naelimisha maeneo yote ya uwekezaji, lakini zaidi eneo la masoko ya mitaji ambalo ni rahisi watu kufanya uwekezaji ila hawana elimu ya kutosha.
Karibu.
 
Tafsiri yako ya uwekezaji imenishangaza. Kwamba ukishiriki sio uwekezaji. Mo anashiriki day to day pale Metl inamaana Metl sio uwekezaji? Manji pia alikuwa CEO pale Quality Group ina maana ule sio uwekezaji? Watu wengi duniani wana manage investment zao.
 
Back
Top Bottom