Mjanga
JF-Expert Member
- Feb 13, 2011
- 1,238
- 324
Napenda kutoa tahadhari kubwa sana kwa wanafunzi wa UNIVERSITY OF DAR ES SALAM wanaoishi Mabibo Hostel na watu wengine wanaokaa maeneo hayo. kuna kijana ambaye anajifanya ni fundi Computer hasa Laptops na vifaa vingine vya electronics kama simu, pasi na vinginevyo. Huyu jamaa maarufu kama "RAS" ana ofisi yake karibu kabisa na Conner bar kwenye barabara inayoingia Hostel hizo. Ni mtu tapeli sana, ametapeli watoto wa wakulima waliojinyima ili angalau wapate laptops ili kuenenda na maendeleo ya sayansi na teknolojia na pia kufanikisha malengo yao yaliyowapeleka hapo chuoni, anaendelea na utapeli huo kila kukicha, na amekwisha kuwatapeli wengi zikiwemo simu na komputa mpakato (Laptops).
Hivyo nyie vijana wa Hosteli ya Mabibo kuweni macho na huyo tapeli.
Hivyo nyie vijana wa Hosteli ya Mabibo kuweni macho na huyo tapeli.