Tahadhari: Ugonjwa wa mlipuko Ubungo, Dar Es Salaam

benzemah

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2014
Posts
1,533
Reaction score
3,187
Mkurugenzi wa halmashauri ya manispaa ya ubungo, anawatangazia wananchi wote wa manispaa ya ubungo kuwa katika mkoa wa dar es salaam kuna mlipuko wa ugonjjwa wa kuharisha na kutapika.

Hivyo anawaomba wananchi wote kuchukua tahadhari kwa kufanya yafuatayo

1. Epuka kunywa maji yasiyochemshwa au yasiyowekwa dawa ya kutibu

2. Kula vyakula vya moto

3. Epuka ulaji holela wa vyakula vinavyoandaliwa kwenye mazingira hatarishi

4. Hakikisha unanawa maji tiririka na sabuni mara kwa mara

5. Epuka utiririshaji maji taka maeneo mbalimbali kuna wagonjwa wenye magonjwa ya kuharisha na kutapika wafike katika kituo cha afya kilichopo karibu

7. Epuka mikusanyiko isiyokuwa ya lazima ujumbe huu uwafikie wananchi wote na taasisi zote za serikali na binafsi kama mashuleni, vyuoni, makanisani, misikitini na maeneo yote yenye mikusanyiko

 
Mikusanyiko mfano kwenye daladala kumbe na yenyewe Ina ambukiza Cholera pandemic.......
 
Yaani kusema tu Kipindupindu wanaona aibu? Wakati mnazembea kutoa huduma za ukusanyaji taka mlikuwa hamjui kama kuna kipindupindu?
 
Kabla hajatutangazia haya matangazo atembelee maeneo machafu kwenye manispaa yake na achukue hatua, zaidi ya hapo ni failure yake, aanze na soko la urafiki!! Hadi aibu, kisima Cha huo ugonjwa
 
Sema ni pindua pindua tuu mbona inazunguka sana bwashee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…