JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 685
- 1,124
Mchele mbichi una Bakteria hatari wa Bacillus Cereus ambao husababisha sumu ya chakula 'food poisoning'. Vilevile una misombo kadhaa ambayo husababisha matatizo katika hatua mmeng'enyo wa chakula. Lectini, aina ya protini ambayo hupatikana katika mchele huo hupunguza uwezo wa mwili kunyonya virutubishi
Hamu ya kula mchele mbichi inaweza kuwa ni ishara ya 'Pica' matatizo ya kisaikolojia yanayopelekea kupoteza nywele, maumivu ya tumbo, uchovu na upungufu wa anemia ya chuma. Inashauriwa kula mchele uliopikwa "wali" maana una virutubisho zaidi kuliko mchele mbichi