Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 76,107
- 160,001
Mikoa ya Lindi, Mtwara, Tanga, Pwani, Dar es Salaam, Visiwa vya Mafia, Unguja na Pemba vinatarajiwa kukumbwa na upepo mkali wa kasi ya kilometa 40 kwa saa kwa muda wa siku nne mfululizo. kuanzia Januari 20 hadi 23 mwaka huu.
Utabiri uliotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini TMA inaonesha kuwa upepo huo unaoipiga pwani ya bahari ya Hindi utaambatana na mawimbi makubwa ya bahari yanayoifikia urefu wa mita mbili.
Akitoa taarifa za utabiri huo, Mchambuzi wa Hali ya Hewa wa TMA Rose Senyagwa amesema, upepo huo utaathiri shughuli za usafirishaji katika sekta ya bahari na kuleta athari katika makazi ya watu yatakayofikiwa na hali hiyo.!